Anna Kilango na mamilioni yaliyo porwa ilikuwaje?

Mitomingi

Senior Member
Jan 15, 2008
130
0
Kwanza nampa pole Ana Kilango kwa kuumwa na apate nguvu mapema arudi nyumbani.Natoa hongera kwa JF kuweza kuwapo tena baada ya Mwema kuamua kutaka kutuzima na mwisho poleni sana na Hongereni Mike na Marc.

Nimeona ni muda muafaka sasa na kuweza kuuliza hapa JF.Sote tunajua historia ya Anna Kilango kuporwa cash 200m .Anasema alivamiwa na zikapotea.Je kuna ukweli katika hili ? Pia napenda kuuliza yeye alikuwa kazitoa wapi hizi pesa na akawa anazipeleka kwa nani ? Hizi pesa zilikuwa zake binafsi za kampuni fulani ?Maswali ni mengin lakini kwanza naomba kuanzia hapa tu .Tafadhalini naombeni msaada .Anna Klango ni kiongozi nadhai ni vyema tukajua honest na intergrity yake .
 
Labda swali la kwanza kama ni kweli, hizo mil 200 kazipata wapi? na iweje asafiri na pesa nyingi kiasi hicho? tukipata majibu ya hayo ndio twende kwenye hilo la pili maana kuna habari kuwa "the whole saga was stage managed" na "Babu" kapigwa bao la "kisigino"
 
Kwanza nampa pole Ana Kilango kwa kuumwa na apate nguvu mapema arudi nyumbani.Natoa hongera kwa JF kuweza kuwapo tena baada ya Mwema kuamua kutaka kutuzima na mwisho poleni sana na Hongereni Mike na Marc.

Nimeona ni muda muafaka sasa na kuweza kuuliza hapa JF.Sote tunajua historia ya Anna Kilango kuporwa cash 200m

Unamaanisha wewe na nani hapa unapotumia neno sote na wingi?

.Anasema alivamiwa na zikapotea.Je kuna ukweli katika hili ? Pia napenda kuuliza yeye alikuwa kazitoa wapi hizi pesa na akawa anazipeleka kwa nani ? Hizi pesa zilikuwa zake binafsi za kampuni fulani ?Maswali ni mengin lakini kwanza naomba kuanzia hapa tu .Tafadhalini naombeni msaada .Anna Klango ni kiongozi nadhai ni vyema tukajua honest na intergrity yake .

Hizi habari ni za wapi na ulizipata lini na aliyasemea wapi haya?

Source pleaase?!
 
naona Mama Malecela anawaweka tumbo moto mafisadi na kila siku kuzusha mambo ...... huyu mama hamtaweza hapa labda muende kule darhotwire or namchukiamamamalecelakwavilenimchapakazikwahiyonitamzushiakashfa.co.majungu
 
wrong thread alert!?

naona aliyeanzisha mada amegundua udaku wake na ameingia mtini... sijui kama nitalaumiwa nikishauri hii kwenda kwenye udaku!
 
naona Mama Malecela anawaweka tumbo moto mafisadi na kila siku kuzusha mambo ...... huyu mama hamtaweza hapa labda muende kule darhotwire or namchukiamamamalecelakwavilenimchapakazikwahiyonitamzushiakashfa.co.majungu

Mwafrika wa Kike
Badala ya kumvaa mitomingi nadhani soma tena uelewe anacho uliza .Ni kweli huyu Mama aliwahi kuporwa kiasi kikubwa sana cha pesa it was in the media kila mahali Tanzania .Wewe labda ulikuwa Kenya ama Uganda ama mbali hukujua lakini hata mimi nilisoma na kuanza kujiuliza maswali mengi.Sasa msaidieni mitomingi kwa maswali yake haya badala ya sis kumvaa.

Uzoefu wangu hapa si kila habari inakuwa na source .Zingine zinakuwa plain na zikawa za kweli .Source namsaidia sasa ni yeye mwenyewe na magazeti yaliyo elezea tukio hili .Haya nadhani nimesha kusaidia wewe na wengine wenye maswali na mawazo ya aina yako kuelewa .Tuendelee sasa
 
Haya mambo yalishajadiliwa hapa na hitimisho lilifikiwa kuwa hakuwa na kiasi hicho cha pesa. Walioanzisha haya mambo hapa pia hawakuwa na ushahidi na waliishiwa kuingia mtini kama mitomingi leo.

Search jina la Mama Malecela na utakuta thread yenye mambo hayo!
 
Mwafrika wa Kike
Badala ya kumvaa mitomingi nadhani soma tena uelewe anacho uliza .Ni kweli huyu Mama aliwahi kuporwa kiasi kikubwa sana cha pesa it was in the media kila mahali Tanzania .Wewe labda ulikuwa Kenya ama Uganda ama mbali hukujua lakini hata mimi nilisoma na kuanza kujiuliza maswali mengi.Sasa msaidieni mitomingi kwa maswali yake haya badala ya sis kumvaa.

Uzoefu wangu hapa si kila habari inakuwa na source .Zingine zinakuwa plain na zikawa za kweli .Source namsaidia sasa ni yeye mwenyewe na magazeti yaliyo elezea tukio hili .Haya nadhani nimesha kusaidia wewe na wengine wenye maswali na mawazo ya aina yako kuelewa .Tuendelee sasa

Lunyungu,

Hebu weka wazi kidogo hayo magazeti yaliporipoti hili suala walisema kuna pesa ziliporwa? na je ni kiasi gani nadhani tukipata majibu hayo mjadala utakuwa mtamu zaidi
 
Lunyungu,

Hebu weka wazi kidogo hayo magazeti yaliporipoti hili suala walisema kuna pesa ziliporwa? na je ni kiasi gani nadhani tukipata majibu hayo mjadala utakuwa mtamu zaidi

atapata wapi source kama walioleta wakati ikiwa live walikosa source za kuweka?
 
I second you on that mwafrika wa kike..there is something fishy going on ever since JF imereturn..the threads have changed and they show stand out...na ni nyingi kama mtu na forward vile...still investigating (kama report ya ernt n young vile lol)..
 
Kapinga haya yote yalitegemewa so dont worry coz we are still here and the second phase has just started!

Nakuhakikishia kuwa Mwakyembe na Mama Kilango watakuwa subject ya attacks toka kwa mafisadi hapa hadi ushangae. Ukifuatilia magazeti ya mkoloni na mwizi hatari kabisa Tanzania -Rostam Azizi basi utagundua ninachoongelea hapa.
 
kama kweli kuna magazeti yaliripoti basi weken nakara hadharani hapa tuzione,msiwe mnazungumza habari za katika vijiwe vyenu vya kahawa na karata hapa jf,then watu wakaanza kumsemea mama wetu mfichua mafisadi,kwa utaalaam wangu naona huyu jamaa aliyeanzishwa hii mada anataka watu wamuone mama anna kilango naye fisadi,kwani milioni 200 kitu gani anaweza akameki tu,ww kama umetumwa na fisadi au ww ni fisadi ila hatukufahamu ingia humu kwa stail nyingine sio hizo za kutoka vijiwe vya kahawa .
 
Haya mambo yalishaongelewa hapa mkuu na hakuna aliyekuja na huu uthibitisho wa haya madai. Huu ni udaku na unastahili kuwa kwenye forum yake muafaka - ya udaku.
 
Just to set the record straight

From the Bunge's record Hansard, Hotuba ya (then) Waziri wa Ulinzi Professor Philemon Sarungi

http://72.14.205.104/search?q=cache...ma+kilango+majambazi&hl=en&ct=clnk&cd=2&gl=us

Mheshimiwa Spika, ningelipenda pia kuwapa pole
Waheshimiwa Dkt. Abdallah na Dkt Aisha Omar Kigoda kwa
kufiwa na Baba yao mzazi Marehemu Omar Kigoda. Mwenyezi
Mungu awape moyo wa kustahimili na subira. Napenda kutoa pole
pia kwa Mhe. Parmukh Singh Hoogan na Mhe. Dkt Lawrence Gama
kwa kufiwa na watoto wao wapendwa. Tunamuomba Mwenyezi
Mungu azipumzishe roho za marehemu wote mahali pema peponi
Amina. Napenda vile vile kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge
wenzetu waliokumbwa na mikasa mbalimbali nikianza na
Mheshimiwa Anne Kilango Malecela aliyevamiwa na majambazi,
majambazi ambayo yalipora mali na kumjeruhi kijana wao na
dereva.
Tunashukuru kuwa majambazi hayo yamekwisha naswa
na yanashughulikiwa kulingana
na sheria

Pia

http://www.ipp.co.tz/ipp/nipashe/2004/06/09/12818.html

Mke wa Malecela avamiwa na majambazi

2004-06-09 08:10:41
Na Said Mmanga,PST Morogoro

Majambazi yakiwa na bunduki na mapanga, yamevamia gari la mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Bi. Anne Kilango Malecela na kuwajeruhi mtoto na dereva wake na kupora mali pamoja na fedha taslimu.

Tukio hilo lilitokea jana saa 11.45 alfajiri katika eneo la Maseyu, mkoani Morogoro, Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Morogoro, akiwa safarini kuelekea mkoani Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kilichoanza jana.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walikolazwa majeruhi, Bi. Kilango alisema uvamizi huo ulitokea baada ya gari lao aina ya Toyota Land Cruiser T 208 AAR kupata pancha tairi la nyuma.

Alisema wakati dereva wa gari hilo, Bw. Habibu Rajabu aliposhuka na vifaa kwa ajili ya kubadilisha tairi hilo, alitokea mtu mmoja akiwa na kishoka, ambapo baadaye liliongezeka kundi la watu wengine wakiwa na silaha bunduki aina ya SMG, mapanga na shoka.

Bi. Kilango alisema kundi hilo lilimfuata na kumtaka atoe fedha ambapo aliwaelekeza katika kiti cha mbele ambako kulikuwa na mkoba na briefcase, vitu ambavyo majambazi hayo yalivichukua.

Alisema majambazi hayo pia yalimpora fedha taslimu na simu tatu za mikononi.
Hata hivyo, hakutaja kiasi cha fedha hizo.

Alisema majambazi hayo yalimshambulia mtoto wake Nyange Kilango (18), ambaye alijaribu kukataa kuwapa majambazi simu yake.

Pia walimjeruhi kichwani dereva wake Bw. Rajabu.
Hata hivyo, alisema yeye hakujeruhiwa katika mkasa huo. Polisi mkoani Morogoro ilithibitisha kutokea tukio hilo,ambapo ilisema inaendelea kuwasaka majambazi hao.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Mkoa wa Morogoro na polisi mkoani hapa, ulifika katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro kuwapa pole majeruhi hao.

Baadhi ya waliofika kutoa pole hiyo ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw.Paul Chikira na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Bi. Catherine Ndahani.

Eneo la Maseyu lililopo katika Barabara Kuu itokayo Dar es Salaam hadi Morogoro, limekuwa likikabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya uporaji wa kutumia silaha.
 
Bi. Kilango alisema kundi hilo lilimfuata na kumtaka atoe fedha ambapo aliwaelekeza katika kiti cha mbele ambako kulikuwa na mkoba na briefcase, vitu ambavyo majambazi hayo yalivichukua.

Alisema majambazi hayo pia yalimpora fedha taslimu na simu tatu za mikononi.
Hata hivyo, hakutaja kiasi cha fedha hizo.

Hakutaja kiwango cha pesa ni sentensi muhimu sana katika hii story.
 
Mwafrika wa kike
Hapa hatuangalii eti kwasababu mtu amefanya jambo jema, then mabaya yake yafichwe, Hapana na si kawaida ya JF kufanya hivyo
Kama mama Malecela anayo mabaya aliyofanya lazima yazungumziwe na sio tu, kwa sababu katusaidia katika Richmonduli basi yake yanyamaziwe, kila Fisadi atapitiwa kwa muda wake.
Sio kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!

BabaH,

Usidhani kuwa mimi namtetea Mama Malecela kwa sababu tu ya issue ya zitto na richmonduli. Ninafanya hili kama vile ambavyo nimekuwa namtetea Nyerere hapa ingawa mimi si mwanaccm.

Sihitaji kuwa Mkulu FMES kujua kuwa hii story na hizi habari za millioni mia mbili si za kweli.

Hii habari haina uthibitisho na hicho ndicho kinasukumwa hapa (at least from my side).
 
Watanzania mnanishangaza sana...yaani mnaona hii topic sio valid eti kwa sababu ilishawahi kujadiliwa hapa..na hakuna aliyewahi kuleta source!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom