Anna Abdallah: Ubunge rushwa tupu, atolea mfano wa Mbunge (Chadema), Cecilia Paresso hakuna rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anna Abdallah: Ubunge rushwa tupu, atolea mfano wa Mbunge (Chadema), Cecilia Paresso hakuna rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa ulingo wa wanawake nchini, Mh. Anna Abdallah

  Mwenyekiti wa Ulingo wa Wanawake nchini, Anna Abdallah, amesema hakuna mgombea ubunge asiyetoa rushwa katika chaguzi, hali ambayo inayosababishwa na mfumo wa uchaguzi uliopo.

  Akizungumza katika semina ya wabunge iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa jana, Abdallah ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema kwa kupata utaratibu mpya wa kuwachagua wabunge, kutawezesha kuepuka masuala ya rushwa.

  Alitolea mfano wa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Cecilia Paresso, alivyopatikana na kwamba hakukuwa na rushwa kwa kuwa uteuzi huo umetokana na orodha ya majina iliyowasilishwa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


  "Mfumo wa sasa unawafanya wabunge kutoa rushwa, si kwa uchaguzi mkuu wala mdogo," alisema Abdallah na kufafanua kuwa hakuna jambo ambalo litamsikitisha ikiwa Katiba Mpya itakuja na kasoro ambazo zinamfanya mwanamke kubaguliwa.


  Pia alisema utaratibu mpya wa kuwapata wabunge utawajengea heshima wabunge wote tofauti na mfumo uliopo hivi sasa ambao mbunge wa viti maalum amekuwa akibaguliwa.


  Alisema mfumo huo umekuwa ukimbagua mbunge wa viti maalum kupata nafasi ya uwaziri mkuu kwa kuwa katiba imeainisha kuwa waziri mkuu atatokana na mbunge kutoka jimboni.


  Kadhalika, Abdallah alisema jambo ambalo limekuwa likimkera ni wanawake kutoteuliwa ndani ya vyama vya siasa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

  "Hakikisheni mnagombea kwa wingi katika chaguzi na sisi kama ulingo tutazungumza na viongozi wakuu wa vyama vya siasa," alisema.

  Akifungua semina hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, alitoa wito kwa wabunge kutumia muda wao kwa kuwa makini ili kujenga msingi wa uelewa wa hatua mbalimbali za mabadiliko ya Katiba.


  Alisema kwa kupata msingi huo, kutawawezesha kutoa michango yenye tija wakiwa kama jicho la kijinsia.


  "Sote tunatambua kuwa masuala ya kikatiba ni ya kitaalamu na yanahitaji uelewa mzuri zaidi ili kutoa mchango wetu kwa jamii hususan wanawake, kwani sisi tukielewa vizuri basi tutawafikia jamii kwa kujiamini zaidi na hivyo kupata maoni yao kiurahisi," alisema.


  Wakichangia kwenye semina hiyo, wabunge hao wametaka wanawake nchini kuwaunga mkono kwa kuwapa kura wanawake wanaowania ubunge ili washinde nafasi wanazowania.


  Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Mariam Msabaha, aliwataka wanawake kuwaunga mkono wagombea wanawake wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi.


  Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Fatuma Mikidadi, alisema ingawa haki za mwanamke zimekuwa zikidaiwa tangu uhuru, lakini hadi sasa bado si yote yamekamilika.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Yeye Mwenyewe alikuwa anaupata sababu ya watu kumuogopa na kumchagua sababu ya Jina Lake; watu wapya ni vigumu kuchaguliwa bila kutoa chochote
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Inna maana anakubali kwamba na yeye katoa rushwa? PCCB iko wapi?
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hawa walevi wa madaraka ya bure wanataka wagawe nyabi wapewe na uwaziri mkuu? Ukiwa ccm ni janga la taifa, watu tuna mpango wa kupendekeza viti maalumu vifutwe wao wanaomba wapewe na upm? Pthuuuuuuuuu!
   
 5. J

  John W. Mlacha Verified User

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  huu utaratibu wa jina la nani linafuata haujakaa sawa ..m mama akishaona kuwa anakaribia kuwa mbunge anaweza kumuua muheshimiwa ili zamu yake ifike
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280
  ...Magamba wanaanza kuweweseka na kusema kile ambacho Watanzania wengi tulikifahamu miaka mingi iliyopita. Katika katiba mpya Ubunge uwe ni wa awamu mbili tu kama ulivyo Urais ili kupunguza rushwa iliyokithiri katika chaguzi za Wabunge na kiwekwe kipengele kwamba Mbunge yeyote yule atakayebainika kutoa rushwa ya aina yeyote ile ili apate Ubunge basi atapandishwa kizimbani na akikutwa na hatia atafungwa si chini ya miaka 10, kazi ngumu na kulipia gharama zote za kesi.
   
 7. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Marehemu Regia alichaguliwa kihalali na aliungwa mkono na kinamama wengi Ifakara pamoja na kinababa pia. Ila TUME ya uchaguzi ilimpora ushindi wake waziwazi. Hata ukiwa mwanamke, ukiwania ubunge kupitia upinzani adui namba moja TUME haitakuacha. Ni bora wangesisitiza TUME huru kuliko kubembeleza wakinamama kuwaunga mkono.
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huyu mama alitakiwa awe anaongoza kuajiri watanzania kutokana na kukaa madarakani kwa muda mrefu na si kuendelea kubana nafasi bungeni bila kufanya chochote cha maana!! Haki za wanawake haki za wanawake, au ndiyo tayari kampeni za uarais zimeanza, I just have the feeling that CCM wanataka kusafisha njia za rais mwanamke. M4C
   
 9. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,832
  Likes Received: 2,771
  Trophy Points: 280
  Huyu mama kila nikimsikia huwa ananikumbusha miaka ya '70 tukiwa watoto wakati huo kule Nassa, Magu alikipata cha moto! Tunasimuliwa alikimbia U-DC baada ya Wasukuma kumrudi, nyamb..f zake anastahili kupumzika apishe na wengine, leo ni miaka zaidi ya 40 bado yuko madarakani?! Shit!
   
 10. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu mama ni mnafki
  ang'atuke lo! Miaka yote hiyo
   
 11. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  'mwenyekiti wa ulingo wa wanawake'???????
   
 12. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika kusoma kwangu historia, sijawahi kuona chomba fedhuli na dhalimu, fisadi kikadumu, Huwa kinajitafuna chenyewe mpaka kuanguka, kama ukuta wa Yeriko. Rushwa inaimaliza CCM.
   
 13. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  acha porojo rudi mtwara kalipe wakulima pesa zao za korosho ww si ndiye m/kiti wa bodi ya korosho?
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Walikuwa hawajui mchimba kisima sharti aanze yeye kutumbukia kwanza. Wanachimba shimo ambalo wao ndio wa kwanza kujitumbukiza. Wanashituka leo kuwa mambo sio mambo.
   
 15. mbwigule

  mbwigule JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 235
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Rushwa ndani ya serikali na chama cha CCM ni kansa isiyoweza tibika na mtu yeyote na ndiyo itakayokifuta chama hiki katika historia ya siasa. Wapinzani waiombee CCM izidi kujichanganya katika hili ili 2015 wawe kama wanamsukuma mlevi. Inasikitisha, lakini ndvyo ilivyo; kwamba hakuna kitu kikaendelea ndani ya chama hiki bila ya kuingiza corruption hebu tazama hili suala la ubunge wa Afrika Mashariki; ofisi ya spika ndiyo iliyoanza ku corrupt kwa kugawa nafasi nyingi kuliko ilivyotakiwa kwa CCM, kisha wagombea bila haya wala fedheha wakigawa rushwa nje nje bila ya kukemewa na hilo dude mnaloliita TAKUKURU ambalo kwa kweli ni mzigo tu wa taifa. Taifa zima limetekwa na huu mzimu wa rushwa na hakuna wa kumwamini kuanzia rais hadi tarishi! Watanzania ni lazima tufike mahali sasa tuseme HAPANA kwa CCM.
   
 16. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kumbe CHADEMA wanastahili pongezi kwa uamuzi wao wa kijasiri wa kujitoa kwenye uchaguzi wa fedheha huu. Sasa ni wazi watakaochaguliwa ubunge wa Afrika mashariki woote watakuwa wezi, vibaka na wala rushwa wakuu kuwawakilisha si watanzania, bali chama chao cha wezi na majambazi. Lakini Historia itawahukumu CCM.
   
 17. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Huyu inabidi akanyee debe keko kwanza
   
 18. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​huyu bibi kumbe bado yupo
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hata yeye naye anatoa rushwa ili achaguliwe?
   
 20. R

  Rev. Damasus Mkenda Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  How comes that a prominent figure like her can speak such words?? She has been an MP for many years also has been Minister in Different Ministries today she declares her evils, it like confession of SIN openly. Now we have proved beyond doubt that Bribe and Corruption has has its rootcourse from the Top. God help TZ. But the time has come and the time is now, the Bible says in Exodus 3:7-10, God heard the cries of the children of Israel and he saw their sufferings then he sent his servant to deliver them from the Bondage. God is delivering TZ. Amen!!
   
Loading...