BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,097
Ni kipi kilichomfanya huyu mama amshambulie Anne Kilango? Anne Kilango alizungumza nini kibaya ndani ya Bunge hata kikamgusa vibaya Anna Abdallah? Je, Anna Abdallah amewahi kushiriki kwenye ulaji wa kifisadi? Je, mumewe Pius Msekwa ambape aliwahi kuwa Spika wa Bunge na sasa Naibu Mwenyekiti wa CCM ni fisadi? aliwahi kushiriki kwenye ulaji au mradi wowote ambao machoni mwa Watanzania ulikuwa na harufu harufu ya kifisadi?
Anna Abdallah amshambulia Kilango
na Martin Malera, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya watu
MJADALA wa Bajeti ya 2008/09 jana uligeuka sehemu ya malumbano, baada ya mbunge na mwanasiasa mzoefu na kiongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuamua kujibu mapigo ya hoja zilizotolewa na mwanaCCM mwenzake.
Katika hali ambayo haikutarajiwa, Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah, alitumia muda wake mwingi kuchangia bajeti hiyo kujibu kauli kali zilizotolewa juzi na Mbunge mwenzake wa CCM, Anne Kilango Malecela (Same Mashariki) kuhusu wizi wa mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Benki Kuu (BoT).
Akionekana dhahiri kutofautiana na Kilango, mbunge huyo alipinga katakata kuwapo kwa watu wanaotisha wenzao au wabunge waoga kuchangia mjadala wa bajeti ndani ya bunge hilo.
Alisema suala la wizi wa fedha za EPA halipaswi kuwagawa wabunge kwani tukio hilo ni kilio cha kila mbunge na si cha watu wachache kwani hakuna mbunge anayeshabikia ufisadi.
Abdallah, ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alisema kila mbunge anataka fedha hizo zirejeshwe, lakini kinachowatofautisha ni kwa baadhi ya wabunge kuweza kuzungumzia suala hilo kwa mbwembwe.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge kwa nguvu kiasi cha kuvuruga hotuba yake mara kadhaa, mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambayo ni jumuiya ya CCM, alitaka suala hilo kutowagawa wabunge.
"Suala la EPA lisitugawe wabunge humu ndani. Kila mbunge anataka fedha hizo zirejeshwe, tofauti yetu ni kwamba wengine wanazungumza sana, tena kwa mbwembwe nyingi, wengine wanazungumza kwa upole, lakini nia yetu ni moja," alisema Abdallah.
Mbali ya hilo, aliwataka wabunge waliokuwa wakishangilia kwa nguvu kwa kupigapiga meza zao, kutulia kwani walikuwa wakimmalizia muda wake na kusema: "Jamani, nani hapa anaogopa? Hatuogopi kitu, tena hakuna anayetishwa kwani lengo letu ni moja." Abdallah ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na serikali, alivirukia vyombo vya habari kwa kuviweka kwenye kundi moja na kuviita chama cha siasa kisicho na usajili, kwa kuwa ndivyo vinavyofanya wabunge wanaonekana wana mtafaruku ndani ya Bunge, kwamba kuna kundi linashabikia ufisadi na lingine halishabikii.
Ingawa hakutaja jina la mbunge yeyote aliyedai kulizungumzia suala la EPA kwa mbwembwe, lakini ni dhahiri alikuwa akimlenga Kilango ambaye juzi alizungumzia fedha za EPA kwa ukali wakati akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti.
Akizungumza kwa kujiamini na sauti ya juu juzi, Kilango alisema yuko tayari kufa kupigania fedha za EPA ambazo ni zaidi ya sh bilioni 133, zirejeshwe kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete, vinginevyo bungeni ‘patakuwa hapatoshi'.
Kilango, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya CCM Taifa na mmoja wa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kulaani ufisadi katika kashfa ya Richmond iliyosababisha mawaziri watatu kujiuzulu, akiwemo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alizungumzia pia ufisadi mwingine wa zaidi ya sh bilioni 216 zilizokopwa mwaka 1992 kupitia Mpango wa Uagizaji Bidhaa Nje (Import Support), na kutaka nazo zirejeshwe mara moja.
Kilango ambaye pia ni mke wa mwanasiasa mkongwe, John Malecela, katika hotuba yake ya juzi iliyowafurahisha wengi, alisema vitisho dhidi yake haviwezi kamwe vikamfanya abadili msimamo wake kwa madai kuwa anafanya hivyo kwa maslahi ya serikali, chama chake cha CCM na kwa wananchi wa Jimbo la Same Mashariki, waliomtuma kuwawakilisha bungeni.
"Mheshimiwa Spika, Mwanafalsafa wa Kigiriki, Socrates siku moja alipokuwa sokoni, alihubiri kuwa watu wengi makini duniani huwa wako tayari kufa kwa ajili ya kile wanachokiamini, ukweli na haki. Alipotakiwa kuikana kauli yake, alisema hawezi, wakampa sumu, akanywa, akafa kwa kusimamia ukweli.
"Mheshimiwa Spika, tumebaki kulalamikia ufinyu wa mapato ya ndani, lakini tumesahau kuwa fedha nyingi zinaliwa na kikundi cha watu wachache, watu wameiba fedha za EPA, rais anataka fedha hizo zirejeshwe, na mimi nasema siogopi vitisho, fedha hizo zisiporudishwa, hapa patachimbika, patakuwa hapatoshi hapa, Mheshimiwa Spika," alisema Mama Kilango.
Katika hali inayoonyesha mgawanyiko wa dhahiri miongoni mwa wabunge wa CCM ndani ya Bunge, hasa linapofika suala la ufisadi mkubwa, baadhi ya wabunge waliozungumza na Tanzania Daima nje ya Bunge kwa sharti la kutotajwa majina yao, walishangazwa na hatua ya Anna Abdallah kuonyesha kutofautiana na Anne Kilango waziwazi katika suala la ufisadi wa fedha za EPA.
"Mama Anna kama angetaka kuunga mkono hoja ya Mama Kilango, asingesema eti wapo wanaozungumza kwa mbwembwe kuhusu suala la EPA. Hapo anaonyesha hakufurahishwa na hoja ya Mama Kilango ama kwa sababu za kutotaka kumjengea umaarufu zaidi au kwa sababu anazozijua," alisema mmoja wa wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hata hivyo, wabunge wengine waliungana na Mama Anna Abdallah na kumtetea.
Mbunge mmoja alisema ni kweli kwamba wabunge wote wa CCM wana uchungu, na kwamba hakuna sababu ya Mama Kilango juzi kuelezea kuwa yupo tayari kufa kana kwamba yeye pekee ndiye mwenye uchungu na fedha hizo.
Mjadala wa hotuba hiyo ya Bajeti ya Waziri wa Fedha, ilihitimishwa jana kwa Bunge kupitisha bajeti hiyo.