Aniponza nikafukuzwa kazi, leo anahitaji nimsaidie

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
36,775
83,955
Nilikua nimekaa pembezoni mwa bwawa la kuogelea huku nikitumi kinywaji bariiidi, jirani na nilipokuwepo palikuwa na vijana kama wa tatu pia walikua wanaogelea huku wakichezea maji hapa na pale, ndipo alipopita dada mmoja pembezoni mwa lile bwawa akiwa amevaa vizuri, kapendeza. Ghafla wale vijana wakamsukumia kwenye maji huku yule dada akitapatapa na wale vijana wakiendelea na vicheko. Ndipo niliamua kuchumpa majini na nikafanikiwa kumtoa yule mdada majini.
Dada alienda kushtaki kwa afisa muajiri, na chakushangaza namimi akanijumuisha kwenye lalamiko lile (kudhalilishwa kijinsi) na wote tukafukuzwa kazi.
Mwanzoni mwa wiki huyu dada alikuwa kati ya wasahiliwa kwenye kampuni niliyopo, na mimi ni kati ya watu wanne tuliokuwa tukifanya utahini.
Kinacho nipasua kichwa ni huyu dada amekua akiwasiliana na mimi kila mara akiniomba nimpendekeze achukuliwe kwenye nafasi hiyo iliyo wazi, na mimi nina uwezo wa kumpendekeza na akachukua kazi.
Nishaurini wanajamvi.
 
Tupa kule kashakuja na huko ngoja akufukuzishe tena kazi ohooooo!! Ibilisi kakufata na huko bado unataka kumkaribisha mwepuke ,kaa mbali, kimbia weweweweeeeeeeeee!!!!
 
Msaidie tu,halafu usikaribishe mazoea kabisa(najua itakuwa ngumu),ila jitahidi.
 
Everything happens for a reason, I believe u r in a better position now than your previous job, if not the best is coming, only if u pass this test.
 
Mtendee wema ili na yeye ajifunze kutoka kwako namna ya kuwa na roho nzuri kwa wengine.. Ukimfanyia mtima nyongo hataweza kujifunza chochote hivyo hutakuwa umemsaidia kwa lolote......

Be good to people who are bad to you. It hurt them!
 
Tupa kule kashakuja na huko ngoja akufukuzishe tena kazi ohooooo!! Ibilisi kakufata na huko bado unataka kumkaribisha mwepuke ,kaa mbali, kimbia weweweweeeeeeeeee!!!!

Mkuu, punguza povu, lakini asante kwa ushauri
 
Everything happens for a reason, I believe u r in a better position now than your previous job, if not the best is coming, only if u pass this test.

Sawa mkuu, let me forgive and forget
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom