Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 37,162
- 85,133
Nilikua nimekaa pembezoni mwa bwawa la kuogelea huku nikitumi kinywaji bariiidi, jirani na nilipokuwepo palikuwa na vijana kama wa tatu pia walikua wanaogelea huku wakichezea maji hapa na pale, ndipo alipopita dada mmoja pembezoni mwa lile bwawa akiwa amevaa vizuri, kapendeza. Ghafla wale vijana wakamsukumia kwenye maji huku yule dada akitapatapa na wale vijana wakiendelea na vicheko. Ndipo niliamua kuchumpa majini na nikafanikiwa kumtoa yule mdada majini.
Dada alienda kushtaki kwa afisa muajiri, na chakushangaza namimi akanijumuisha kwenye lalamiko lile (kudhalilishwa kijinsi) na wote tukafukuzwa kazi.
Mwanzoni mwa wiki huyu dada alikuwa kati ya wasahiliwa kwenye kampuni niliyopo, na mimi ni kati ya watu wanne tuliokuwa tukifanya utahini.
Kinacho nipasua kichwa ni huyu dada amekua akiwasiliana na mimi kila mara akiniomba nimpendekeze achukuliwe kwenye nafasi hiyo iliyo wazi, na mimi nina uwezo wa kumpendekeza na akachukua kazi.
Nishaurini wanajamvi.