Anipendae simpendi ila nimpendae hanipendi nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anipendae simpendi ila nimpendae hanipendi nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mafanikio, Dec 7, 2010.

 1. m

  mafanikio Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 51
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mimi ni msichana wa zaidi ya miaka 30, ninafanya kazi nzuri, nina degree mbili lakini sijabahatika kupata mwenzi wa kweli mpaka sasa. Ingawa kuna vijana wasiopungua watano ambao wamekuwa wakidai wananipenda na wamefika bei kwangu, ninaamini kati anaweza kuwepo anaenipenda kwa dhati na huenda wengine wananipenda kwa sababu fulani fulani. Lakini cha ajabu kati yao ni mmoja tu anayenigusa moyo wangu lakini nina kikwazo cha kupishana imani pia kuna mambo anafanya yananikatisha tamaa.

  Ila kuna kijana ninampenda kwa moyo wangu wote lakini sioni kama yuko serious kwangu zaidi ya kudai ananipenda mdomoni ila matendo yake hayaendani na akisemacho. Na siku zote naamini hakuna jambo baya kama kuwa na mtu ambaye humpendi, nami sitaki kuwa na mtu nisiyependa kwa dhati maana rafiki nimtakaye sasa ningependa ndio aje kuwa barafu wangu wa moyo yaani mume wangu wa ndoa wa kufa na kuzikana.

  Naombeni ushauri nifanyanye nini jamani japo naendelea kuomba mungu anisaidie.
   
Loading...