Anguko la uchumi Tanzania: Kampuni binafsi zapunguza wafanyakazi kutokana na hasara

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
IMG-20161122-WA0078.jpg

Hali inaonyesha kwamba baadhi ya kampuni sasa zimelemewa na hali ngumu ya uchumi na sasa zimeamua kupunguza wafanyakazi ili kudhibiti hasara kubwa wanayopata.

Kampuni hizo zimekuwa zikiandika barua kwa unyonge mkubwa kwa watumishi wake,na kuwaeleza kwamba hazina jinsi nyingine,bali tu kuwarudisha nyumbani japo zinawahitaji.

NB: Watarudi kuishi vipi na familia zao? watalipaje kodi za nyumba na bili mbalimbali? je nchi sasa ni rasmi iko kwenye recession na hakuna austerity measures(njia za kudhibiti uchumi usizidi kuporoma)

View attachment 4
Na hii imo japo ni ya serikali.

==========

UPDATES;

TSN yakanusha hii habari ya kupunguza wafanyakazi wake. Kwa habari zaidi soma=>TSN kupunguza wafanyakazi kuanzia Novemba 30, 2016? Kampuni yakanusha
 
Attachments

  • IMG-20161122-WA0085.jpg
    IMG-20161122-WA0085.jpg
    34.3 KB · Views: 126
  • IMG-20161122-WA0082.jpg
    IMG-20161122-WA0082.jpg
    29.3 KB · Views: 122
je kampuni binafsi unayofanya kazi ina hali gani?

unaweza kupost hapa kutufahamisha ili wanauchumi wa nchi hii watoke chini ya kapeti walikojificha na kujifanya hawaoni

iwe ulikuwa unafanya hotelini,kampuni ya kitalii,tax dreva,boda boda,benki na popote pale

andika hapa ili hali halisi ifahamike
 
Jamani haya mbona ni maagizo yaliyotolewa na JPM siku ya uzinduz wa Bombardier mpya za ATCL.
Kweli akili za nyumbu zipo miguuni mwa nyumbu aliyetangulia!
 
Nilikuwa na jumla ya wahudumu 42 ktk bar zangu ambazo ziko maeneo tofauti, mwezi wa 8 nilipunguza 20, na kwa jinsi hali inavyokwenda mwishoni mwa huu mwezi nitawapunguza 10 ili wabaki 12 tu, na hao 12 tumekubaliana mishahara Yao pia itapungua, sababu kuna amri ya mkuu wa mkoa ya kufungua saa 10 jioni na kufunga mwisho saa 6 usiku,

Kabla ya awamu hii ya Makonda mauzo yalikuwa ni wastani wa milioni 9 kwa Siku, sikuwa na matatizo na TRA, sasa hivi mauzo ni Kati ya laki 7 mpaka laki 9, sasa naona TRA ni kama hawaniamini. Nawaonea huruma hawa wahudumu, hata zile tip za soda hakuna! Nasubiri tu msimu huu wa sikukuu upite, nihamie Kenya, siwezi kuendelea kukisuburi kifo huku nakiona,
 
Tatizo la kuendesha nchi kimhemko linaelekea kuiharibu kabisa nchi yetu hii nzuri.
 
Jamani haya mbona ni maagizo yaliyotolewa na JPM siku ya uzinduz wa Bombardier mpya za ATCL.
Kweli akili za nyumbu zipo miguuni mwa nyumbu aliyetangulia!
Kwa hiyo alitoa maagizo sao hill wapunguze wafanyakazi, tsn wapunguze wafanyakazi tumia akili yako hata kidogo siyo kila kitu unameza tu
 
Kwa jinsi hali inavyokwenda, Kama ikiendelea hivi mpaka January, nashauri wafanyabiashara wajipange, siyo lazima kufanya biashara Tanzania, kuna nchi majirani zetu ambazo mazingira ya kufanya biashara ni very friendly

Kenya, Uganda, Rwanda, Congo, Comoro, tena wanatuheshimu sana.hakuna haja ya kukomoana hapa, nchi ikishatulia kibiashara tutarejea, Home sweet home,
 
Nilikuwa na jumla ya wahudumu 42 ktk bar zangu ambazo ziko maeneo tofauti, mwezi wa 8 nilipunguza 20, na kwa jinsi hali inavyokwenda mwishoni mwa huu mwezi nitawapunguza 10 ili wabaki 12 tu, na hao 12 tumekubaliana mishahara Yao pia itapungua, sababu kuna amri ya mkuu wa mkoa ya kufungua saa 10 jioni na kufunga mwisho saa 6 usiku,

Kabla ya awamu hii ya Makonda mauzo yalikuwa ni wastani wa milioni 9 kwa Siku, sikuwa na matatizo na TRA, sasa hivi mauzo ni Kati ya laki 7 mpaka laki 9, sasa naona TRA ni kama hawaniamini. Nawaonea huruma hawa wahudumu, hata zile tip za soda hakuna! Nasubiri tu msimu huu wa sikukuu upite, nihamie Kenya, siwezi kuendelea kukisuburi kifo huku nakiona,
Bora ukae kimya.utaambiwa wewe mpiga dili.
 
Ili kuongeza ufanisi, na kuongeza faida, huwa kuna vitu muhimu vya kufanya.
1. Kuongeza uzalishaji
2. Kupunguza gharama (ambayo njia mojawapo ni kupunguza wafanyakazi)
3. Kubadilisha teknolojia (ambayo hii pia inaweza changia kupunguza wafanyakazi)
So kinachotokea siyo cha ajabu. Jambo la ajabu ni Kuchagua kuajiliwa badala ya kuajili au kujiajili
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom