Anguko la uchumi Tanzania: Kampuni binafsi zapunguza wafanyakazi kutokana na hasara

Kwa jinsi hali inavyokwenda, Kama ikiendelea hivi mpaka January, nashauri wafanyabiashara wajipange, siyo lazima kufanya biashara Tanzania, kuna nchi majirani zetu ambazo mazingira ya kufanya biashara ni very friendly

Kenya, Uganda, Rwanda, Congo, Comoro, tena wanatuheshimu sana.hakuna haja ya kukomoana hapa, nchi ikishatulia kibiashara tutarejea, Home sweet home,
Kuja kuangalia ndugu na jamaa tu otherwise Tz si nchi ya kufanya biashara labda ufanye uwizi tu
 
Ili kuongeza ufanisi, na kuongeza faida, huwa kuna vitu muhimu vya kufanya.
1. Kuongeza uzalishaji
2. Kupunguza gharama (ambayo njia mojawapo ni kupunguza wafanyakazi)
3. Kubadilisha teknolojia (ambayo hii pia inaweza changia kupunguza wafanyakazi)
So kinachotokea siyo cha ajabu. Jambo la ajabu ni Kuchagua kuajiliwa badala ya kuajili au kujiajili

Kuajiliwa=kuajiriwa
Kujiajili= kujiajiri
 
Hiyo namba tatu pia ni ya muhimu walijazana ofisini unnecessarily " kuwa na wanyakazi wengi zaidi ya uwezo wa kampuni"
 
Cha ajabu kuna vichwamaji watakuja kukejeli hii taarifa na kuibeza.nachelea kusema humu ndani kuna watu wametumwa special kwa ku-crush chochote kinachosemwa ambacho kipo against matakwa ya mabwana wale..binafsi taarifa nakubaliana nayo haswa since it's the reality with evidence na sio porojo..hata pale mkuki house kuna jamaa yangu alitaka ku-rent na aliweka order tokea mwaka jana lakini mambo yalivyobadilika akagairi..last time alipigiwa simu akiombwa ku-rent since wa ku-rent hawapo sababu ya hali ya uchumi lakini akapiga chini kwa kuwa wanunuzi wenyewe hawapo
 
Kenya ni mahali salama kabisa kwa investment.
Uhakika 100% no usumbufu wa kijingajinga kama Tz.
Mimi ni mtz na nimeinvest Kenya naona tofauti
wanasiasa wa kenya watazozana majukwaani sana tu,huwezi sikia wanaharibu bandari ya mombasa,au kuvuruga biashara,kwenye hayo ya uchumi wanaungana na kuwa wamoja kabisa

Siasa ya kenya inaheshimu uchumi
 
je kampuni binafsi unayofanya kazi ina hali gani?

unaweza kupost hapa kutufahamisha ili wanauchumi wa nchi hii watoke chini ya kapeti walikojificha na kujifanya hawaoni

iwe ulikuwa unafanya hotelini,kampuni ya kitalii,tax dreva,boda boda,benki na popote pale

andika hapa ili hali halisi ifahamike
Mkuu upo sahihi last week nilimleteeni uzi kama huu watu wakaona ni dhihaka.
 
Ili kuongeza ufanisi, na kuongeza faida, huwa kuna vitu muhimu vya kufanya.
1. Kuongeza uzalishaji
2. Kupunguza gharama (ambayo njia mojawapo ni kupunguza wafanyakazi)
3. Kubadilisha teknolojia (ambayo hii pia inaweza changia kupunguza wafanyakazi)
So kinachotokea siyo cha ajabu. Jambo la ajabu ni Kuchagua kuajiliwa badala ya kuajili au kujiajili
Li, Li, Li...Tia R
 
Na kupunguza wafanyakazi kwenye makampuni.ni agizo la magufuli?
Acha akili ya nyumbu yeye JPM ndiye aliyetengeneza mazingira haya ya Nchi kuwa na hali mbaya ya uchumi. Hivi nikuulize yaliyotokea bandarini mpaka mizigo ikakosekana ni kosa la nani kama sio jpm kutoza VAT mizigo inayopita kwenda nje ya Nchi. Acha ujinga
 
Serikali inabidi ipunguze wafanyakazi kuongeza ufanisi. Wengi wamejazana tu Hakuna kitu wanafanya maofisini
Tuliambiwa serikali pamoja na kufanya uhakiki itapitia taasisi zake zote ili kuona kama inaweza ikazirestructure hasa zile zenye majukumu yanayofanana n.k lakini mpaka sasa hili hatukuliona kwani kuna overstaffing ya ajabu kwenye baadhi ya taasisi na bado wanaendelea kuajili hivi wage bill itapunguaje hapo, tafadhalini waserikali pitieni upya muundo wa taasisi zenu ikama nk ili muweze kureallocate watumishi kwani ikiwa kuna taasisi zina watumishi zaidi ya wanaohitajika kuna nyingine zina upungufu so chukueni walikozidi wapelekeni walikopungua na sio kuajili wapya. Hii itawasaidia kupunguza wage bill na kuboresha huduma za jamii.
 
Atbadilisha bodi za TRA mpaka achoke ila yale malimbikizi yamekwisha na sasa ataanza yeye kuisoma namba ya makusanyo mapya.
 
je kampuni binafsi unayofanya kazi ina hali gani?

unaweza kupost hapa kutufahamisha ili wanauchumi wa nchi hii watoke chini ya kapeti walikojificha na kujifanya hawaoni

iwe ulikuwa unafanya hotelini,kampuni ya kitalii,tax dreva,boda boda,benki na popote pale

andika hapa ili hali halisi ifahamike
Habari umeokoteza halafu unataka watu watoe maoni kuhusu kampuni zao
Utapata wapi uhalisia wakati Id zimefichwa
 
nakumbuka kipindi cha uchaguzi mke wangu alikuwa akiweke kale kawimboo kazuuri ccm mbele kwa mbele huku akininengulia mauno akijua kabisa inanikera maana sijawahi kuikubali ccm hata wakimsimamisha malaika maana nnaamin atageuka na kuwa shetani ila Leo ni zamu yangu kumuwekea ua sikilize japo kwa sasa hataki hata kuusikia maana na yeye alipata kazin kwake wakati Wowote anafungashiwa virago akawe mama wa kushinda nyumbani
 
Mpaka vipofu nao wametengenezewa namba zao zile za kupapasa kwa mikono nao WANAZISOMA NAMBA KWAKUPAPASA na mikono tena kwauzuri kabisa wanaelewa kuanzia moja mpaka laki moja
 
Umaskini uliokithiri miongoni mwa Watanzania umeongezeka kwa asilimia kubwa ifikapo June 2017.
 
Back
Top Bottom