Anguko la Rais Samia Suluhu Hassan lipo mikononi mwetu, tusimuangushe, tupambane kwa pamoja kukuza uchumi wetu kwa kuchapa kazi

Yazidu Hamza Bitika

New Member
Jul 22, 2022
4
1
Habari za wakati huu enyi walimwengu wa Karne ya mwisho wa dunia, mliopo katika ardhi yenye baraka ya Tanzania, na hata msiokuwa Tanzania.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Awali ya yote nipende kukushukuru wewe unayesoma makala hii kwa kutenga muda wako ili uweze kutengeneza maarifa mapya kupitia kusoma makala hii, hakika hutajutia muda wako.

Napenda ufahamu kuwa hapa duniani kunamataifa mengi sana, lakini Tanzania ni taifa la pekee sana, kuanzia kwenye historia yake na baraka tele zilizojaaliwa katika ardhi yake na kila Mlimwengu ni shahidi wa hili. Mungu azidi kuibariki Tanzania.

Katika ardhi hii ya Tanzania pamekua panatokea mambo mengi yenye kufurahisha na mengi ni kama baraka tu za mwenyezimungu lakini tusipokua makini, tutajikuta tunaziharibu wenyewe, kwani sisi tumebarikiwa rasilimali nyingi ikiwemo madini na ardhi yenye rutuba, lakini zaidi tunatunu za taifa, ikiwemo amani, hii ni baraka Kubwa sana kwetu tuitunze.

Naomba nianzie kuizungumzia awamu ya Tano ya Tanzania iliyokua na weledi mkubwa wa utendaji kazi na umakini wa kusimamia mambo, ambayo imedumu kwa miaka takribani sita pekee na kufanya makubwa kanakwamba ilikaa miaka ishirini ni baraka Kubwa tuliyonayo ya kupata viongozi Bora na si bora viongozi, hakika Watanzania mnamjua kuchagua, ni awamu iliyowafungua macho watu katika mambo mengi sana, na kwa kidogo watu wakajua muelekeo wa taifa lao na mambo yanakwendaje, tulifurahia uongozi huo, baadae Mwenyezimungu muumba alimchukua mja wake ambaye ndiye aliyekua Kiongozi wa taifa hili katika awamu hiyo kwa ahadi yake ileile ya kuwa "kila nafsi itaonja mauti" hata Mimi na wewe tutafuatia baada yake kwani sisi ni wa Mwenyezimungu na kwake tutarejea.

Nawaomba watanzania wengi wafahamu kuwa kila jambo alifanyalo Mwenyezimungu linamakusudio yake, kwani tumeachiwa zawadi kubwa sana ambayo ni ngumu kuigundua kwani bado ipo kwenye kasha lake siku ikijakufunguliwa hadharani Wenda ukanielewa, hebu jaribu kumfuatilia Rais wa awamu ya sita na aliyekua makamu wa Rais wa awamu ya tano Mama Samia Suluhu Hassan kwa ukaribu zaidi Wenda ukanielewa.

Kuanzia mfumo wa utawala Bora uliopo, ushirikiano wa ndani na nje ya nchi, ushirikishwaji na kuwajali raia wake, ama kweli tumebahatika.

Sema sikitiko langu ni kwa baadhi ya Watu watakaoweza kumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kubaki kuwa mabingwa wa lawama aidha kwa mihemko ama propaganda, unajua watanzania tunapaswa kuwa makini sana na siasa na wanasiasa wenyewe, maana kunawatu wengi wanaweza kukuza mambo na kuyatengenezea propaganda ili tu kutimiza malengo yao ya kisiasa hivyo yatupasa kuwa makini.

Hivyo basi Rais wa taifa hili anawahitaji zaidi Watanzania katika maendeleo kuliko watu wengine, kama mjuavyo Rais Samia Suluhu Hassan amechukua kiti Cha urais nchi ikiwa katika hali ngumu sana, nchi hii ilikua katika hatihati ya kushuka kiuchumi kwani tulikua tumeshuka mpaka asilimia nne na pointi, bado muda huohuo janga la Uviko-19 lilikua limeshamiri lakini Mwanamama huyu alipokea nchi na kupambania na ameweza kwakweli.

Nasema ameweza kwasababu ukitazama uchumi umepanda tena hadi sasa tupo kwenye asilimia Tano pointi sita na janga la uviko limekabiliwa kwa kiasi kikubwa. Anguko la Rais Samia Suluhu Hassan lipo mikononi mwetu, tusimuangushe, tupambane kwa pamoja kukuza uchumi wetu kwa kuchapa kazi, Tanzania ni nchi Kubwa na yenye rasilimali za kutosha , tuzitumie kwa kuzalisha mazao mbalimbali tukauze kwenye masoko ya ndani na nje na tuache lawama zisizo na msingi. Kwani ili adui asituingilie na tufanikiwe kama taifa lazima tuwekeze kwenye kufanya kazi kwa bidii , tusimuangushe Mwanamama shupavu kwani anguko la Mama Samia Suluhu Hassan lipo mikononi mwetu, Tusimuangushe!!!! na Kazi iendelee!

Nadhani kwa kumalizia niwaombe vijana wa Tanzania nzima wawe wabunifu na wawe na macho ya kutazama fursa zilizopo ndani ya jamii yetu, kwasababu tukikaa tu bila kujishunghulisha tutatumiwa sana na watu waovu na tutaliharibu taifa letu wenyewe, tulipende taifa letu, tuwapende viongozi wetu tuwaunge mkono katika kila jambo jema natumai tutafika.

Nipende kukushukuru kwa kuwa Nami mwanzo hadi mwisho wa makala hii, karibu kwa maoni ama maswali.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Kazi iendelee.
 
Rais hakuchaguliwa na wananchi ameingia madarakani akaanzisha vita na marehemu ambaye alikuwa karibu naye na ndio wananchi wengi wameendelea kumchukia Sana
 
Nashukuru kwa mchango wako katika mada hii, naomba unielewe sehemu moja, ninaona Watanzania baadhi wakiwa na Imani Kama uliyokuwanayo wewe, lakini hiyo ni dhana tu, hata Mwenyezimungu muumba anatuamrisha kuwa tusiwadhanie watu vibaya kwasababu hakuwahi kukutamkia kuwa hamuungi mkono Rais wa awamu iliyopita ama la, nataka nikuthibitishie kuwa Mama yetu Samia Suluhu Hassan anamuunga mkono aliyekuwa Rais wa awamu ya Tano, kwanza kwa kaulimbiu, Magufuli alikuja na kaulimbiu ya kazi huku akisema "hapa kazi tu!" na Rais wa awamu ya sita akaendeleza kazi kwa kusema "kazi iendelee!" Kwahiyo mpaka hapo nahisi utakua umeona ni namna gani anamuunga mkono kwahiyo awamu ya sita imeanzia pale ilipoishia awamu ya Tano na maneno haya amekua akiyazungumza mara kwa mara Rais Samia Suluhu Hassan
Nashukuru......
 
Back
Top Bottom