a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,386
- 1,316
Hii ligi ya nani bora umeianzisha wewe, na wewe ndio unayeiendeleza.Nyerere alianza uongozi wakati mgumu kuliko wote waliofuata.
Hakuwa na wasomi, hakuwa na infrastructure na hakuwa na resources za kutosha
Tukiangazia mengi aliyofanya na ni 'kashfa' kubwa kumweka katika mizani na mwingine.
Rekodi ya Nyerere katika taifa hili ni 'unique'
Kuchukua nchi yenye dini tofauti na makabila tofauti na kuiuanganisha ni jambo gumu sana
Nigeria na majirani Kenya au Uganda, miaka 60 bado zimwi la ukabila na udini linawatesa sana. Tanzania tulishaondoka huko aliyeanza kuturudisha huko ni Magufuli
Ukishaanza kuwatazama wananchi kwa jicho la dini na makabila tayari unawagawa
Mfano rahisi tu, JPM alikuwa na salam za kidini. Hili ni jambo baya sana , Tanzania ni SECULAR country. Kuna dini tofauti , watu wenye dini za asili, Wasio na dini na Wasioamini
Kusalimia kwa Ukristo na Uislam ni kutenga makundi mengine na kuyajengea makundi mawili umuhimu usio na sababu wala maana. Nchi yetu ina raia wenye dini lakini serikali haina dini.
Kilichoshangaza wakati wa JPM kila jambo lilihusisha viongozi wa dini.
Hili likajenga utamaduni wa kuamini Wakristo na Waislam, utaratibu unaoiumiza Nigeria
Lakini pia teuzi zake zilitiliwa shaka, kuna kiongozi mmoja alitoa takwimu (kukamatwa) akionyesha namna udini ulivyotamalaki. Ingawa nia yake haikuwa na dhamira njema lakini likuwa ngumu kumpinga alikuwa na takwimu!!
Nyerere, katika kumaliza ukanda udini na ukabila alianzisha mifumo ya elimu iliyokuwa ghali lakini leo tunaona manufaa yake.
Watoto wa Mkoa wa Mara walisoma Tanga, wale wa Kilimanjaro walisoma Dodoma, Wa Mwanza walikwenda Mtwara , na wa Kigoma walikwenda Mbeya.
Mchanganyiko huu uliwafanya watu waone ni wamoja na wanaweza kuishi sehemu yoyote Tanzania bila tatizo. Ndiyo maana leo kuna Wasukuma Kilimanjaro na Wabondei Shinyanga.
JPM alikuja na sera ya chuki dhidi ya kanda ya kaskazini akiwataka ''wasubiri maendeleo'
Hilo limeamsha hasira si kwa kanda moja bali nyingine wakihisi kuwa Rais kutoka eneo fulani ana influence maendeleo ya eneo jingine '' positive au negative'' na si nchi kwa ujumla
Kulikuwa na sababu gani za Rais wa nchi anayetegemewa kuwaleta wananchi pamoja kutoa kauli ya kibaguzi namna ile?
Hivi ikitokea vita kama ile ya Kagera kuna kuchagua nani aende? Kwanini basi watu watengwe.
Na kuna kosa gani watu wa eneo fulani kujiletea maendeleo?
Tukiachilia mbali Nyerere kafanya nini kwa kitu kimoja kimoja, kuunganisha Taifa ilikuwa kazi muhimu sana inayomtofautisha na waliomfuata, hawakuwa na kazi hiyo na pengine walianza kuibomoa kwa kauli za reja reja na za kibaguzi
Kumweka Nyerere na mwingine katika mizani kuna matokeo mawili;
Kumtusi sana Nyerere au kumdhalilisha sana aliyesimama katika mizani na Nyerere
Hasa unapolazimisha Nyerere na Magufuli sijui unatoa wapi hoja hiyo.
Lakini pia hilo kwavile linapita sana kichwani mwako ulipaswa ujiulize mara mbilimbili KWANINI MAGUFULI Vs NYERERE, na si Mwinyi, Mkapa wala Kikwete?
Binafsi sijawahi sikia Mkapa/Mwinyi wala Kikwete Vs Nyerere, ila tu Magufuli na Nyerere.
Katika nafasi zao na nyakati zao tofauti, hao ndio viongozi pekee walioonesha kujali, kuheshimu na kulinda Rasilimali za Taifa kwa kiasi kikubwa sana kuliko wengine.
Nafasi ya Nyerere haiwezi kukaliwa na MTU mwingine yeyote, lakini chini yake hutamkosa Magufuli. Huo ukweli mnaujua ila tu mnamchukia, mnaumia.
Atazaliwa Tena na Tena.