Anguko la Ndugai: Somo la Katiba, viongozi na nchi

Hili nalo neno, nakubaliana nawe ingawa haliondoi ukweli kuwa shaka imetendeka wakati wa Mzalendo JPM. CAG anaweza kutusaidia zaidi kujua 1.5T na 70 B ilikuwaje wakati huo!
Usimuonee CAG peke yake. Wasomi, Wastaafu, CCM, Upinzani, Viongozi wa Dini mpo.
Nashukuru umeelewa pesa 1.5T au 70 B haziwezi kufungwa katika mabunda.

Nikusaidie kuelewa zaidi, kwamba, pesa zinazochukuliwa kinyume na utaratibu haziachi 'trails' .
Unachelewa kuelewa
Kufungua account kutaacha trail katika transaction hivyo usitegemee kuiona acc
Pesa haziibiwi ili zikakae kwenye acc... Pesa zinaonekana kwenye life style za wezi.
Bilions tu tuliweza kuziona inakuwaje kwenye mambo mengi.... Vituo vya mafuta, hotels, estates, migodi, mashamba, nk...
KWANINI TUSIONE HAYO KWA 1.5 T?
Ni kwa msingi huo wapo wanahoji pesa zilizopitia Ikulu kwa kuelewa hakuna audit
Kuhusu acc ninachosema ni kuwa hatuwezi kuzifikia ni account za watu au taasisi

Ndio maana CAG wapo duniani, ni watalaam si kila Tom, Dick anbd Harry ni CAG
Punguza Kasumba ya Duniani sijui, Wazungu, nk... Jenga Fikra huru.
Hapana hapa kuwa na utulivu unielewe. Construction, renovation , maintanance ni vitu tofauti na gharama zake zina vary pia.
Kwenye Kiswahili chochote kinachofanyika hapo ni UJENZI.
Hapa kuna mahesabu kidogo nisingependa kukuumiza kichwa chako
Unajilishsha upepo.
Mapungufu katika kiswahili hayabadili maana yake kama ilivyokusudiwa
Construction, renovation , maintanance.
Hakuna lugha yenye mapungufu. Lugha zote hujitosheleza.
Hapa sina ushauri zaidi ya kukutaka ufikiri katika umbali kidogo na ule wa pua, nina uhakika unaweza ! try. Anza na mita michache , km n.k.
Huo nao ni ushauri pia.
Yes Nyerere alifanya (construction) , AH Mwinyi akafanya ukarabati (maintanance)

Haya mambo ukiyasikia ghafla yanachanganya, kidogo kidogo nina uhakika utaelewa
JK inaweza kuwa Jakaya Kikwete, zingatia.
Eeeh hapa ndipo hoja ilipo na ndio maana tunauliza 1.5T , 70 B na mauza uza tunayoyaona
Waziri Mkuu Majaliwa katueleza 'pesa zilivyotumika MSD' .
Of course kisicho na majibu kunazua ''chuki''.
Sasa kwanini umeshikilia kauli hakujenga! SISI TUMERIDHISHWA NA MATUMIZI YA KODI ZETU kwa kiasi kikubwa kuliko awamu nyingi nyuma. Hatujawahi kuona matumizi makubwa ya kodi kama ya awamu ya tano.
Hili linatufanya tujiulize, Je, waliopita walizitumia wapi nyingi?
Well done! sasa unanena!
Una shida kubwa mahali. Ninakukumbusha tena, MGR NI TOFAUTI NA SGR. MGR imekarabatiwa.
SGR imeanza tangu tuta.

Rudi Tz uone kilichopo.
Added value katika SGR ipo, ni haraka na mzigo mkubwa kuliko mita reli.
Unaongeza kitu kwa kitu kilichopo tayari. Sasa tuambie added values za SGR zimeongezwa kwenye nini?
What? nawe unataka mkataba. Hivi si wewe uliyesema haya ''Kumbuka Mimi sio muumini wa Formalities za ajabuajabu''
Naji kasema nimetaka mkataba. Nimesema hatujapewa mkataba, Ila shaka Yetu ipo bado kutokana na nyendo zenu.
Lakini pia nimesema "za ajabuajabu" hope unatambua kuwa zipo ambazo si za ajabu ajabu.

Natambua pia kuwa si kila mkataba unaweza kuwekwa wazi, ninatambua pia kuwa si kila mtz anaweza kuelewa kilichomo katika mkataba.

Yes! watu wachote pesa tu ilimradi tuna ufanisi. Kwa mfano,tununue mfuko mmoja wa sementi 500,000 hakuna tatizo ilimradi tu daraja likamilike.
Yangetokea hayo Tungehoji tu, wala tusingesubiri CAG.

Miradi inafanyika ndani ya jamii, sio hewani. HATUJAWAHI KUTILIA SHAKA KUBWA HIVYO, na ni kwa sababu thamani ya miradi inajionesha wazi.

Punguza skipping ya hoja. Naona umeonea aibu suala la Korosho.

SGR na MGR nilikueleza vema kuwa ni Two different lines zinazo run alongside, bado unaleta vioja hapa.
 
Kwanza ni watetezi wa Magufuli hawana hoja, hata penye hoja hawawezi kuzitetea, hilo huwafanya wenye hasira, matusi na kuweka kinga ya 'Marehemu hasemwi, hawezi kujitetea n.k.'

JPM ni 'unconventional leader' hakufuata taratibu zilizotumiwa na Watangulizi

Watetezi wake wanapofanya 'argument '' wazingatie 'exceptionalism yake''

Kumlinganisha JPM na kiongozi kama Nyerere ni kosa, JPM hawezi ku fit vigezo
JPM hakuwahi kuchaguliwa kabla ya kuwa Rais wala kuwa kiongozi wa shina au tawi
JPM hana rekodi nyingine Uongozi, siasa, uchumi, utamaduni n.k.
JPM hana rekodi yoyote ya Diplomasia iwe ya ukanda, kanda au Kimataifa

Ukimlinganisha na JMK , BWM , AHM au JKN itabidi kwa vigezo, JPM hana vya ulinganifu.

Njia nzuri ya kumtetea JPM ni kutumia 'exceptionalism yake kama unconventional leader

Lakini pia ni muhimu kuyakubali mapungufu ya kibinadamu na kumfanya anaonekana binadamu
Rekodi ya JPM katika utu, ubinadamu na haki zipoje na zinatetewaje!
Kwanini watu wanatetea Udini na Ukabila aliouonyesha badala ya kuona ni mapungufu
Salamu za dini na hotuba za kanisani ni udini unawabagua wasioamini na wasio na dini
Kutaka kanda moja isubiri nyingine ni ukanda, kuna utetezi gani kwa hili?
Kutamka hakuna maendeleo walipochagua wapinzani ni ubaguzi, hivi hili linahitaji utetezi!

Kosa la pili ni ku pick up petty things wakavikuza. Vitu vinavyokuzwa ni vya kawaida kabisa. Huwezi kusema kajenga flyover ni mafanikio ya nchi !

Kwamba, JPM alipambana na rushwa si kweli. Plea bargain ni kurasimisha rushwa kwa malipo
Ni kwa msingi huo leo pesa za plea bargain hazijulikani zilikwenda wapi.

Kosa la tatu ni watetezi kutojadili rekodi ya JPM kwa ujumla na kumwacha na utetezi wa flyover.

Watetezi hawawezi kutetea rekodi yake kwa Uchumi, siasa au utamaduni
Inaeleweka ni kwa nini, lakini, jambo muhimu ni kukubali mapungufu ili kumjengea 'immunity'

Pesa haziibiwi ili zikakae kwenye acc... Pesa zinaonekana kwenye life style za wezi.
Bilions tu tuliweza kuziona inakuwaje kwenye mambo mengi.... Vituo vya mafuta, hotels, estates, migodi, mashamba, nk...KWANINI TUSIONE HAYO KWA 1.5 T?
Unakumbuka account za Swiss !
SISI TUMERIDHISHWA NA MATUMIZI YA KODI ZETU kwa kiasi kikubwa kuliko awamu nyingi nyuma.
Matumizi katika nini
Hatujawahi kuona matumizi makubwa ya kodi kama ya awamu ya tano.
Hili linatufanya tujiulize, Je, waliopita walizitumia wapi nyingi?
Matumizi ya kodi katika kufanya nini ambacho huko nyuma hakikufanywa
Ninakukumbusha tena, MGR NI TOFAUTI NA SGR. MGR imekarabatiwa.SGR imeanza tangu tuta.
Ninasema hivi Feasibility studies ilizingatia ile ya Germany 1905-1917.

Landscape au Topography haijabadilika na ni mkandarasi mpumbavu ambaye hatakwenda Germany kuiomba bali kuanza upya.
Tuta linajengwa tu kama la viazi, muhimu ni Feasibility studies
Sasa tuambie added values za SGR zimeongezwa kwenye nini?
Nasema hivi improvement ya MGR kwenda SGR kuna added values ndiyo maana kuna investment
Miradi inafanyika ndani ya jamii, sio hewani. HATUJAWAHI KUTILIA SHAKA KUBWA HIVYO, na ni kwa sababu thamani ya miradi inajionesha wazi.
Yes hakuna shaka kwa baadhi, kuna shaka kwa wengine.

Tumenunua ndege zipo zinaonekana
Malipo kwa cash, hatujui yalitoka account gani ya serikali. Tunaambiwa yalipitia Ikulu

''Ndege zipo bwana shida ipo wapi! hataka kama kuna Mabilioni nje ya malipo si ndege zinaonekana ndani ya jamii. Ndio madudu ya MSD yanayoonekana sasa! si vifaa vilinunuliwa''

Punguza skipping ya hoja. Naona umeonea aibu suala la Korosho.
Yes hoja ya korosho nimeonea aibu, ni moja ya mambo ya hovyo sana kufanyika

Kwanza ununuzi hakuwa sustainable au solution ya kudumu na pili bwana Zitto kasema zilimwagwa baharini , hakuna aliyemjibu.

Mradi unaotegemea maguvu ya mtu badala ya mipango si sahihi, kaondoka na mradi wa korosho.

Serikali haifanyi biashara inaweka mazingira mazuri ya biashara.
Biashara si misuli na mishipa ni akili na maarifa
 
Kwanza ni watetezi wa Magufuli hawana hoja, hata penye hoja hawawezi kuzitetea, hilo huwafanya wenye hasira, matusi na kuweka kinga ya 'Marehemu hasemwi, hawezi kujitetea n.k.'

JPM ni 'unconventional leader' hakufuata taratibu zilizotumiwa na Watangulizi

Watetezi wake wanapofanya 'argument '' wazingatie 'exceptionalism yake''

Kumlinganisha JPM na kiongozi kama Nyerere ni kosa, JPM hawezi ku fit vigezo
JPM hakuwahi kuchaguliwa kabla ya kuwa Rais wala kuwa kiongozi wa shina au tawi
JPM hana rekodi nyingine Uongozi, siasa, uchumi, utamaduni n.k.
JPM hana rekodi yoyote ya Diplomasia iwe ya ukanda, kanda au Kimataifa

Ukimlinganisha na JMK , BWM , AHM au JKN itabidi kwa vigezo, JPM hana vya ulinganifu.

Njia nzuri ya kumtetea JPM ni kutumia 'exceptionalism yake kama unconventional leader

Lakini pia ni muhimu kuyakubali mapungufu ya kibinadamu na kumfanya anaonekana binadamu
Rekodi ya JPM katika utu, ubinadamu na haki zipoje na zinatetewaje!
Kwanini watu wanatetea Udini na Ukabila aliouonyesha badala ya kuona ni mapungufu
Salamu za dini na hotuba za kanisani ni udini unawabagua wasioamini na wasio na dini
Kutaka kanda moja isubiri nyingine ni ukanda, kuna utetezi gani kwa hili?
Kutamka hakuna maendeleo walipochagua wapinzani ni ubaguzi, hivi hili linahitaji utetezi!
Nasi hivyo ndivyo tunavyowaona wenye chuki na Magufuli na mliobanwa mirija ya upigaji. HAMTUSUMBUI TENA, TUNAJUA TAYARI KUWA KIONGOZI SAHIHI WA TAIFA LETU ANAPASWA KUWA KAMA MAGUFULI.
Kosa la pili ni ku pick up petty things wakavikuza. Vitu vinavyokuzwa ni vya kawaida kabisa. Huwezi kusema kajenga flyover ni mafanikio ya nchi !
Mlishaambiwa Maendeleo ni msongamano Dar.
Hayo unayosema ni petty issues sisi HATUJAWAHI kuyaona katika upana wake wa sasa.
Kwamba, JPM alipambana na rushwa si kweli. Plea bargain ni kurasimisha rushwa kwa malipo
Ni kwa msingi huo leo pesa za plea bargain hazijulikani zilikwenda wapi.
Ndizo zilizonunua ndege labda, si umesema hujui za ndege ziliidhinishwa na nani!
Kosa la tatu ni watetezi kutojadili rekodi ya JPM kwa ujumla na kumwacha na utetezi wa flyover.
Ulishalitaja hapo juu, ukaita petty thing.
Watetezi hawawezi kutetea rekodi yake kwa Uchumi,
Hatutakaa tuamini tena Takwimu zenu za makaratasi. Ameondoka ameacha Lita ya mafuta ni around 2000 sasa ni 3000.... Nauli, tozo, Umeme, maji, vyakula, nk...

Hiyo ndiyo tafsiri ya sisi wakulima wa Korosho tunaijua.
Ukomo wa Western politics unakaribia.
au utamaduni
Usijitajie tu mambo.
Inaeleweka ni kwa nini, lakini, jambo muhimu ni kukubali mapungufu ili kumjengea 'immunity'
Hakuna anayesema Magufuli hakuwa na pungufu hata moja. Ila mnachokera ni aidha kulazimisha mapungufu, au kutumo dhaifu moja kufunika mengi yenye tija. Hasahasa BEZO ZENU.
Unakumbuka account za Swiss !
Ninakumbuka. Tuambie T zipo wapi?
Matumizi katika nini

Matumizi ya kodi katika kufanya nini ambacho huko nyuma hakikufanywa
Hilo swali ni la kitoto. Anayelima heka moja hawezi pata sifa sawa na was heka 10, japo wote wamelima.

Hoja yako ni ya kitoto katika hili.
Ninasema hivi Feasibility studies ilizingatia ile ya Germany 1905-1917.

Landscape au Topography haijabadilika na ni mkandarasi mpumbavu ambaye hatakwenda Germany kuiomba bali kuanza upya.
Acha kurukaruka, Hakuna mpumbavu anayeweza kutumia Feasibility Study ya miaka zaidi ya 100 nyuma, kufanyia mradi Leo. Hata teknolojia tu kubadilika ni driving factor ya kufanya upembuzi zaidi.
Zingatia pia SGR ina divert mara nyingi kutoka MGR line. Hivi ulisikia habari za Uchorongaji milima?
Tuta linajengwa tu kama la viazi, muhimu ni Feasibility studies
Wewe ni Kituko kweli. Tembelea mradi hata siku moja.
Nasema hivi improvement ya MGR kwenda SGR kuna added values ndiyo maana kuna investment
Sasa investment ndio nini hapo? Nani kakuambia MGR inakuwa improved?

MGR ipo na Itaendelea kuwepo sambamba na SGR. Wewe huo uzushi kakupa nani kwa malengo gani?
Yes hakuna shaka kwa baadhi, kuna shaka kwa wengine.
Hamtusumbui tena, ni mliozoea kufanya Tz shamba la bibi.
Tumenunua ndege zipo zinaonekana
Malipo kwa cash, hatujui yalitoka account gani ya serikali. Tunaambiwa yalipitia Ikulu
Ndizo hizo ulizosema ni rushwa na zisizoonekana labda. Walau zimefanya kinachoonekana.
''Ndege zipo bwana shida ipo wapi! hataka kama kuna Mabilioni nje ya malipo si ndege zinaonekana ndani ya jamii. Ndio madudu ya MSD yanayoonekana sasa! si vifaa vilinunuliwa''
Bei za ndege ziko wazi.
Yes hoja ya korosho nimeonea aibu, ni moja ya mambo ya hovyo sana kufanyika
Leo sisi huku tunatamani yangerudiwa kufanyika tena. Ajabu ni wewe mvuvi au mkulima wa kahawa au mtu wa utalii, kutusemea sisi. Njoo uulize wananchi
Kwanza ununuzi hakuwa sustainable au solution ya kudumu
Ndio, hakuna kinachoweza kuzuia serikali kuingilia kulinda maslahi ya RAIA wake. Pesa ilichelewa kufika kwa walio wengi, lakini hatimaye iliwafikia katika stahiki ya jasho lao tofauti na Leo.

Nikuambie tu, wengi walihamaki lakini Leo tunamuelewa na mwishowe tunatamani atokee wa kufanya Yale tena kwenye korosho.
na pili bwana Zitto kasema zilimwagwa baharini , hakuna aliyemjibu.
Zitto.
Mradi unaotegemea maguvu ya mtu badala ya mipango si sahihi, kaondoka na mradi wa korosho.
Mipango mnayo ninyi wapigaji na nguvu pia. Jeuri yenu haipo tena mmeamua kufidia miaka mitano nyuma, na hakika mnatunyoosha.
Ndio maana nimesema FURAHINI LEO.
Serikali haifanyi biashara inaweka mazingira mazuri ya biashara.
Propaganda na same copy and paste theories kutoka kwa wapuuzi wa magharibi.
Biashara si misuli na mishipa ni akili na maarifa
Ni kweli, na Leo tunaona maarifa hayo yanavyoimarisha Mfumuko wa bei.
 
Nasi hivyo ndivyo tunavyowaona wenye chuki na Magufuli na mliobanwa mirija ya upigaji.
Kujadili legacy ya JPM haiwezi kuwa chuki, ile ya Nyerere tunaijadili mwaka wa 23 sasa
Hii kauli ya chuki ni 'replacement ya ile ya Marehemu hasemwi, Marehemu hawezi kujitetea'
Kuna jitihada za kuzima rekodi ya JPM katika kila eneo isisemwe, tuimbishwe flyover tunazooo...
HAMTUSUMBUI TENA, TUNAJUA TAYARI KUWA KIONGOZI SAHIHI WA TAIFA LETU ANAPASWA KUWA KAMA MAGUFULI.
Magufuli alikuwa mtawala ndio maana hakupenda kukosolewa, hakupenda kusikia mbadala wala hakupenda kusikia awaye anamzidi kwa sifa. Ni mtawala aliyependa kupendezwa.

Kiongozi alikuwa Nyerere. Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawa walikuwa element za uongozi. Magufuli hakuwa kiongozi hata siku moja. Kiongozi anaamini katika 'SISI' , Magufuli anaamini katika 'MIMI' typical feature ya Mtawala at least.
Hayo unayosema ni petty issues sisi HATUJAWAHI kuyaona katika upana wake wa sasa.
Nyerere akiondoka aliacha Viwanda kwa maana viwanda 400. Tunaweza kuvitaja kwa majina na hadhi zake, si cherehani tulizoshuhudia wakati wa JPM. Hayo ni maendeleo!! flyover ??? please!

FYI ujenzi wa Flyover ni kazi za City council au Municipal huko duniani, Rais ana facilitate
Hatutakaa tuamini tena Takwimu zenu za makaratasi. Ameondoka ameacha Lita ya mafuta ni around 2000 sasa ni 3000.... Nauli, tozo, Umeme, maji, vyakula, nk...
Hizi ndizo naita ''petty and flimsy '' hivi Magufuli alikuwa na control ya Oil production duniani
Lakini pia kama kuna tatizo awamu hii ndio iliyokuwa yake. Hakuna kiongozi mpya hata mmoja, na kama ni failure basi architect wake ni JPM aliyeshindwa kutengeneza vitu au mambo sustainable
Hakuna anayesema Magufuli hakuwa na pungufu hata moja. Ila mnachokera ni aidha kulazimisha mapungufu, au kutumo dhaifu moja kufunika mengi yenye tija. Hasahasa BEZO ZENU.
Yes ! ndii maana mnasema marehemu hasemwi, mnasema watu wana chuki ilimradi tu wafungwe midomo. Ninyi hamuamini zama za watu kuimba tu zimekwisha!

Mengi aliyofanya hamuyaelezi mnachotuambia ni flyover. Inahitaji moyo kutetea rekodi yake
Hakuna mpumbavu anayeweza kutumia Feasibility Study ya miaka zaidi ya 100 nyuma, kufanyia mradi Leo. Hata teknolojia tu kubadilika ni driving factor ya kufanya upembuzi zaidi.
Zingatia pia SGR ina divert mara nyingi kutoka MGR line. Hivi ulisikia habari za Uchorongaji milima?
Yes lakini topography ni ile ile. Hujaelewa kitu hapa kwasababu hutaki
Ndizo hizo ulizosema ni rushwa na zisizoonekana labda. Walau zimefanya kinachoonekana.
Plea bargain ni kuuza haki za watu, ni ukatili. Watu walibambikiziwa kesi watoe pesa.
Bureau de change zikafungwa na pesa kuporwa! makampuni yakaanza kujiondokea
Haya hatusemi wanaosema ni VP, PM na Cabinet

Rekodi ni ngumu kuitetea kuna dhulma kubwa imefanyika
Huhitaji kununua vitu kwa pesa za dhulma. Pesa za plea bargain hazijulikani ziko wapi, zinazojulikana ni 70 Bilioni ambazo zilipelekwa Mwanza haijulikani kwa nini.
Bei za ndege ziko wazi.
Tusiende huko, tutafukua makaburi na ''marehemu hasemwi''
Propaganda na same copy and paste theories kutoka kwa wapuuzi wa magharibi.
Serikali haifanyi biashara, Nyerere alijaribu hakufanikiwa. Huo ni ukweli
Tuliona ATCL ikishadidiwa kwa kuua mashirika mengine leo wananchi wanalipa zaidi
Magufuli aliua competition bila kujua ilikuwa ni nzuri kwa performance ya airline industry nchini

Ile ATCL tuliyoambiwa inatengeneza faida, mwaka huu CAG anasema 'hasara tupu'
Ni kweli, na Leo tunaona maarifa hayo yanavyoimarisha Mfumuko wa bei.
Nguvu zilitumika wakati wa JPM kuliko maarifa! Korosho hazikusanywi kwa operesheni zinahitaji utaalamu wa Kilimo. Leo korosho huko kwingine nani anafanya!
 
Kujadili legacy ya JPM haiwezi kuwa chuki, ile ya Nyerere tunaijadili mwaka wa 23 sasa
Hii kauli ya chuki ni 'replacement ya ile ya Marehemu hasemwi, Marehemu hawezi kujitetea'
Kuna jitihada za kuzima rekodi ya JPM katika kila eneo isisemwe, tuimbishwe flyover tunazooo...
Tofautisha Bezo na Hoja.
Magufuli alikuwa mtawala ndio maana hakupenda kukosolewa, hakupenda kusikia mbadala wala hakupenda kusikia awaye anamzidi kwa sifa. Ni mtawala aliyependa kupendezwa.
Nyakati zinamuhitaji, awe alivyokuwa. Awe mtawala au kiongozi. Kimsingi ni wimbo wa kipuuzi tu mliokaririshwa.
Kiongozi alikuwa Nyerere. Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawa walikuwa element za uongozi. Magufuli hakuwa kiongozi hata siku moja. Kiongozi anaamini katika 'SISI' , Magufuli anaamini katika 'MIMI' typical feature ya Mtawala at least.
Uongozi ni UBUNIFU,Dhati, Ujasiri, Uthubutu, Mamlaka/Maamuzi, nk... Mfano wa Kikwete ana mangapi katika hayo yote?
Nyerere akiondoka aliacha Viwanda kwa maana viwanda 400.
Na bado utasema alifeli kwa serikali yake kufanya biashara.
Tunaweza kuvitaja kwa majina na hadhi zake, si cherehani tulizoshuhudia wakati wa JPM. Hayo ni maendeleo!! flyover ??? please!
Tuna vya Tiles Pwani, Sigara Moro, Mpunga, bati, nk
FYI ujenzi wa Flyover ni kazi za City council au Municipal huko duniani, Rais ana facilitate.
Una kasumba ya uduni, kwa umri wako bado una kauli eti za huko duniani. Huoni aibu?
Okey, KAMA HAPA SIO DUNIANI, BASI TAMBUA NI NYAKATI YA KUTENGENEZA DUNIA YETU SASA.
Hizi ndizo naita ''petty and flimsy '' hivi Magufuli alikuwa na control ya Oil production duniani
Wewe utuambie sasa.
Lakini pia kama kuna tatizo awamu hii ndio iliyokuwa yake. Hakuna kiongozi mpya hata mmoja, na kama ni failure basi architect wake ni JPM aliyeshindwa kutengeneza vitu au mambo sustainable
Unachekesha sasa, umesahau maombi yako kwetu kuunga mkono awamu hii? Kama ndivyo udaivyo, failure ya Magufuli ni IPI sasa?

Ukiwa muongo uwe na Kumbukumbu.
Yes ! ndii maana mnasema marehemu hasemwi, mnasema watu wana chuki ilimradi tu wafungwe midomo. Ninyi hamuamini zama za watu kuimba tu zimekwisha!
Hiyo ni imani yako wewe, usitusemee sisi. IMBENI TU, na kibwagizo cha kuupiga mwingi kinavutia sana, nadhani wananchi wanakifurahia.
Mengi aliyofanya hamuyaelezi mnachotuambia ni flyover. Inahitaji moyo kutetea rekodi yake.
Utajiwe mangapi uridhike, ili usije kusumbua tena. Taja idadi rasmi uitakayo.
Yes lakini topography ni ile ile. Hujaelewa kitu hapa kwasababu hutaki
Wewe usilazimishe uongo, kwa madai yako ni kwamba hakukuwa na Feasibility Study, nilichokuambia IPO. Lakini zako hazina msingi tena, ni kupotezeana muda tu.
Plea bargain ni kuuza haki za watu, ni ukatili. Watu walibambikiziwa kesi watoe pesa.
Bureau de change zikafungwa na pesa kuporwa! makampuni yakaanza kujiondokea
Haya hatusemi wanaosema ni VP, PM na Cabinet
Ni wazi waliofanya Tz shamba la bibi iliwalazimu kukimbia. Labda uniambie sasa KUWA Dhana ya Shamba la Bibi ni uongo.
Rekodi ni ngumu kuitetea kuna dhulma kubwa imefanyika
Rekodi ni ngumu kuichafua, kuna makubwa sana yamefanyika.
Huhitaji kununua vitu kwa pesa za dhulma. Pesa za plea bargain hazijulikani ziko wapi, zinazojulikana ni 70 Bilioni ambazo zilipelekwa Mwanza haijulikani kwa nini.
Wenye pesa zisizo za dhuluma hawakukimbia nchi.
Tusiende huko, tutafukua makaburi na ''marehemu hasemwi''
Kumbe unajitisha mwenyewe kwa kivuli chako.
Serikali haifanyi biashara, Nyerere alijaribu hakufanikiwa.
Na bado alimudu kuacha viwanda 400.
Sera za kukaririshwa zimewajaa vichwani.
Huo ni ukweli
Tuliona ATCL ikishadidiwa kwa kuua mashirika mengine leo wananchi wanalipa zaidi
Magufuli aliua competition bila kujua ilikuwa ni nzuri kwa performance ya airline industry nchini
Protectionism inafanywa na kila nchi kwa namna tofautitofauti tu. Ninyi ndio mnaoamini Ulaya hakuna mtu anayeweza kutumia products za Tz, wakati kuna wazagaao mtaani jobless. Kwanini tusipewe Uhuru wa kwanza kuwauzia Azam Embe?
Ile ATCL tuliyoambiwa inatengeneza faida, mwaka huu CAG anasema 'hasara tupu'
Na bado tumeagiza nyingine 5.
Nguvu zilitumika wakati wa JPM kuliko maarifa!
Maarifa huitaji Akili kuyaona.
Korosho hazikusanywi kwa operesheni zinahitaji utaalamu wa Kilimo.
Wataalamu wa kilimo ndio hao waliosubiri mpaka Magufuli kuwanyanyua wakulima.
Leo korosho huko kwingine nani anafanya!
Wakulima tunatamani angekuwepo afanye tena mwaka Jana.

Serikali ina wajibu wa kulinda maslahi ya umma hata kwa kuingilia taratibu Fulani.

AMKA.
 
Awe mtawala au kiongozi. Kimsingi ni wimbo wa kipuuzi tu mliokaririshwa.
Magufuli hakuwa kiongozi alikuwa Mtawala. Kuna tofauti baina ya hayo.

Kiongozi ana maono, anasikiliza wafuasi, anaratibu wafuasi, ana onyesha njia
(vision, listen, coordinate, lead)

Mtawala anataka kutawala, hataki kukoselewa, kusikiliza , kusahihishwa. Anajijali zaidi kuliko anaowatala. Hutumia muda mwingine kwa self aggrandize , ego, rudeness and unsympathetic
Uongozi ni UBUNIFU
Kweli, JPM alikuwa na ubunifu kama ule wa kuchemsha majani kama dawa ya COVID-19
,Dhati, Ujasiri,
Aliamini kwa dhati alichoamini, kwamba, kuna vita ya uchumi dhidi ya Tanzania.
Akaamini mask zimewekewa virus kama sehemu ya vita yake ya uchumi.

Alikuwa na ujasiri -mfano kutoka mbele ya Dunia na kusema Vipimo vya COVID-19 kwa ku test mafenesi havina usahihi, watu waendelee na maombi.
Uthubutu, Mamlaka/Maamuzi,
Yes JPM alikuwa na uthubutu wa mambo mengi tu bila kujali pros and cons
Alitumia mamlaka kuamuru fulani atandikwe na masaa machache akatandikwa risasi
Yes alikuwa na maamuzi bila kujali matokeo ya maamuzi.
Tuna vya Tiles Pwani, Sigara Moro, Mpunga, bati, nk
OK haya ndiyo mafanikio ya cherehani 3000 alizoita viwanda. Please
Una kasumba ya uduni, kwa umri wako bado una kauli eti za huko duniani. Huoni aibu?
Okey, KAMA HAPA SIO DUNIANI, BASI TAMBUA NI NYAKATI YA KUTENGENEZA DUNIA YETU SASA.
Ni hivi ''Flyover' ni mradi wa Mayor wa mji au Jiji huko Duniani si dunia ya JPM

Rais anapoeleza kama mafanikio kazi ya halmashauri kuna jambo! ni ushamba, flyover should never be a story! umewahi kusikia Kenya wakishadidia ushamba huo!
Unachekesha sasa, umesahau maombi yako kwetu kuunga mkono awamu hii? Kama ndivyo udaivyo, failure ya Magufuli ni IPI sasa?
Yes narudia tena na tena, kutangaza nchi kunakofanywa na Rais SSH ni jambo jema.
Nchi ni kama 'bidhaa' inahitaji kunadaiwa na kwa hili Serikali iungwe mkono! Yes iungwe mkono

Kujifungia kwasababu ya poor communication skills haikusaidia Taifa.
Ni wazi waliofanya Tz shamba la bibi iliwalazimu kukimbia. Labda uniambie sasa KUWA Dhana ya Shamba la Bibi ni uongo.
Hapana ni kweli, kuna shamba la bibi halafu likaja la Babu! taratibu tunajua nini kimetokea

Tofauti ni uwepo wa nguruwe Pori na nguruwe wa kufugwa, basically wote ni nguruwe.

CAG wote wametueleza jambo! Hatujui 1.5T zilipo, hatujui 70 Bilioni zilikwenda wapi
Rekodi ni ngumu kuichafua, kuna makubwa sana yamefanyika.
Yes nakubaliana nawe , rekodi ya Magufuli haichafuki. Hivi ulitegemea ichafuke vipi tena?

Rekodi haiwezi kutetewa isipokuwa kwa mwendawazimu!
Tunasikia kwa waliofanya naye kazi na wengine kama akina Nkamia.

Rekodi yake huwezi kuichafua kwasababu haitaonekana kuchafuka zaidi

Wenye pesa zisizo za dhuluma hawakukimbia nchi. Plea bargain ni dhuluma hatujui pesa zipo wapi
Protectionism inafanywa na kila nchi kwa namna tofautitofauti tu. Ninyi ndio mnaoamini Ulaya hakuna mtu anayeweza kutumia products za Tz, wakati kuna wazagaao mtaani jobless. Kwanini tusipewe Uhuru wa kwanza kuwauzia Azam Embe?
Kama protectionism ingalifanya kazi leo tusingeagiza chochote.
Narudia Nyerere aliacha viwanda 400 vikiwa na 100% protectionism.

Hakukuwepo kitu kinachoitwa private sector labda kwa shule chache za Taasisi.
Pamoja na hayo protectionism hakifaulu, tukaishia kubinafsisha

Protectionism zinazofanywa na wenzetu ni za maarifa si maguvu.

Kwa mfano, kuna nchi imeondoa kodi kwa bidhaa za ndani ili kuwe na competition.
Haikuzuia wengine bali ilifanya hivyo kulinda sekta ya Kilimo na mifugo.
Price competition and quality viliamua nani atawale soko

Magufuli alitaka kutengeneza monopoly kwa ATCL akijua ndio njia ya kusaidia shirika! wrong.

Uwepo wa mashirika kama fast jet na Precision kuliongeza ushindani na ubunifu

Magufuli alitakiwa kuunganisha nguvu za mashirika kwa kusaidiana.

Mfano, precision inaunganisha local and region destinations, ATCL inalenga International route.

Ushindani na ushirikiano ungesaidia sana kupunguza gharama!
Baada ya monopoly ya Magufuli ATCL sasa wanapanga bei wanavyotaka!
Maarifa huitaji Akili kuyaona.
Nadhani unamaanisha ''huhitaji'', ikiwa ni hivyo wanaosema hakuwa na maarifa wametumia akili kuona hayakuwepo!
 
Magufuli hakuwa kiongozi alikuwa Mtawala. Kuna tofauti baina ya hayo.
Hakuna tofauti hiyo Kiutendaji, ila tu kwa watumiao akili ndogo kufikiri.
Wapo muwaitao viongozi wapumbavu, wapo pia watawala wapumbavu.

To hell with your Siasa za Maneno. HAMTUDANGANYI TENA. Aitwe Kiongozi au Mtawala, sio muhimu kwetu.
Kiongozi ana maono, anasikiliza wafuasi, anaratibu wafuasi, ana onyesha njia
(vision, listen, coordinate, lead)
That is JPM.
Mtawala anataka kutawala, hataki kukoselewa, kusikiliza , kusahihishwa. Anajijali zaidi kuliko anaowatala. Hutumia muda mwingine kwa self aggrandize , ego, rudeness and unsympathetic
Kwa umri wako tunatwgemea Tafakari, sio mawazo ya kukaririshwa.
Kweli, JPM alikuwa na ubunifu kama ule wa kuchemsha majani kama dawa ya COVID-19
Hizi ndio Chuki na Bezo. Wenzako tunapiga nyungu mpaka Leo hii, na tupo safi.

Peleka mwili wako wakaufanyie majaribio ya chanjo nyingine.

Tulishaonya na kusema, hakuna Uhuru kwa wapumbavu, hamkutusikia.
Aliamini kwa dhati alichoamini, kwamba, kuna vita ya uchumi dhidi ya Tanzania.
Akaamini mask zimewekewa virus kama sehemu ya vita yake ya uchumi.
Porojo na kujitoa akili. Tulishakuelekeza hili.
Alikuwa na ujasiri -mfano kutoka mbele ya Dunia na kusema Vipimo vya COVID-19 kwa ku test mafenesi havina usahihi, watu waendelee na maombi.
Upofu wako tu kutoona Ujasiri wake.
Yes JPM alikuwa na uthubutu wa mambo mengi tu bila kujali pros and cons
Alitumia mamlaka kuamuru fulani atandikwe na masaa machache akatandikwa risasi
Yes alikuwa na maamuzi bila kujali matokeo ya maamuzi.
Uwe na ushahidi. Lakini pia si kosa KUUA mpumbavu anayeligharimu Taifa. NA HAKUANZA YEYE.
OK haya ndiyo mafanikio ya cherehani 3000 alizoita viwanda. Please
NAKUTAJIA VIWANDA, WEWE UNAJITOA AKILI SASA.
Ni hivi ''Flyover' ni mradi wa Mayor wa mji au Jiji huko Duniani si dunia ya JPM
Uko na mental enslavement kwa wazungu. Unatia huruma na aibu.
Rais anapoeleza kama mafanikio kazi ya halmashauri kuna jambo! ni ushamba, flyover should never be a story! umewahi kusikia Kenya wakishadidia ushamba huo!
Kenya hao ambao kila mwaka wanakufa njaa?
Yes narudia tena na tena, kutangaza nchi kunakofanywa na Rais SSH ni jambo jema.
Nchi ni kama 'bidhaa' inahitaji kunadaiwa na kwa hili Serikali iungwe mkono! Yes iungwe mkono
Ni wapi tuligusia kutangaza nchi? Unarukaruka tu na hoja.
Kujifungia kwasababu ya poor communication skills haikusaidia Taifa.
Leo tumeifungua, na matokeo tumeyaona Ngorongoro. Masai wamepata nyumba bora kabisa.
Hapana ni kweli, kuna shamba la bibi halafu likaja la Babu! taratibu tunajua nini kimetokea
Hilo ni lako jipya, Umma haujui hilo. Jifariji.
Tofauti ni uwepo wa nguruwe Pori na nguruwe wa kufugwa, basically wote ni nguruwe.

CAG wote wametueleza jambo! Hatujui 1.5T zilipo, hatujui 70 Bilioni zilikwenda wapi
Lete ushahidi wa uwepo wake kwanza kabla hazijapotea.
Yes nakubaliana nawe , rekodi ya Magufuli haichafuki. Hivi ulitegemea ichafuke vipi tena?
SITEGEMEI ICHAFUKE, ILA KWA WAPUUZI TU.
Rekodi haiwezi kutetewa isipokuwa kwa mwendawazimu!
Yes, nao ni shangazi, bibi, wajomba, babu,mama, na wadogo, kaka na Dada wa ninyi WASOMI, WASTAAFU, CCM, WAPINZANI NA WAONGOZA KONDOO.
Tunasikia kwa waliofanya naye kazi na wengine kama akina Nkamia.
Aliporopoka mwanzo ulitilia shaka Utashi wake, Leo huna shaka na utashi wake.

Werevu wanaona kuwa kumbe shida IPO kichwani mwako, si kwa Nkamia.
Rekodi yake huwezi kuichafua kwasababu haitaonekana kuchafuka zaidi
Fukuza upepo.
Wenye pesa zisizo za dhuluma hawakukimbia nchi. Plea bargain ni dhuluma hatujui pesa zipo wapi
Zimenunua ndege na kujenga Chato.
Kama protectionism ingalifanya kazi leo tusingeagiza chochote.
Narudia Nyerere aliacha viwanda 400 vikiwa na 100% protectionism.
Kama haikufanya kazi, aliwezaje kujenga viwanda 400 na vyote kufanya kazi?
Hakukuwepo kitu kinachoitwa private sector labda kwa shule chache za Taasisi.
Pamoja na hayo protectionism hakifaulu, tukaishia kubinafsisha
Uzembe wa mtu haubatilishi Sera.
Protectionism zinazofanywa na wenzetu ni za maarifa si maguvu.
Wenzenu ndio kina nani? Poor!
Kwa mfano, kuna nchi imeondoa kodi kwa bidhaa za ndani ili kuwe na competition.
Haikuzuia wengine bali ilifanya hivyo kulinda sekta ya Kilimo na mifugo.
Price competition and quality viliamua nani atawale soko
Kwa akili zako nyingi kweli unafikiri Mkulima wa Tz anaweza compete sokoni na Mchina? Wanafanana nini? Je, ni teknolojia au mtaji? TUMIENI VICHWA VYENU VIZURI WANDUGU.

UCHUMI HURIA HAUKO KUMNUFAISHA MNYONGE, MILELE.
Magufuli alitaka kutengeneza monopoly kwa ATCL akijua ndio njia ya kusaidia shirika! wrong.

Uwepo wa mashirika kama fast jet na Precision kuliongeza ushindani na ubunifu

Magufuli alitakiwa kuunganisha nguvu za mashirika kwa kusaidiana.

Mfano, precision inaunganisha local and region destinations, ATCL inalenga International route.

Ushindani na ushirikiano ungesaidia sana kupunguza gharama!
Baada ya monopoly ya Magufuli ATCL sasa wanapanga bei wanavyotaka!
Hujiulizi kwanini Precision bado wapo. Why ni FastJet tu?
Nadhani unamaanisha ''huhitaji'', ikiwa ni hivyo wanaosema hakuwa na maarifa wametumia akili kuona hayakuwepo!
Wapo wapumbavu wajivuniao Upumbavu wao. Fact ni kuwa, hilo ndio kundi la wengi.
 
Hakuna tofauti hiyo Kiutendaji, ila tu kwa watumiao akili ndogo kufikiri.
Wapo muwaitao viongozi wapumbavu, wapo pia watawala wapumbavu.
Hatuangalii nani kiongozi au mtawala mpumbavu kwa ujumla.
Tunasema hivi Nyerere alikuwa kiongozi , Magufuli alikuwa mtawala

Kiongozi anaongelea 'usisi' . Mtawala anaongelea 'umimi'.
Kiongozi ana ndoto , maono na mipango, mtawala ana 'ego' tu!
Wenzako tunapiga nyungu mpaka Leo hii, na tupo safi.
Hakuna tatizo , linakuwa tatizo pale mnapotaka liwe suala la kitaifa.
Ni tatizo mnapotumia kodi zetu kupeeleka ndege Madagascar kubeba mavumba na mchaichai
Linakuwa tatizo pale mnapowanyima wengine fursa za kufanya wanachotaka (vaccination)

Ni ukatili usiomithilika mtu kwa kinyongo tu na matamanio ya nafsi yake anapozua uongo kuwanyima wengine fursa ya matibabu

Kwanini tuaminishwe nyasi za Magufuli lakini tuzuiwe chanjo iliyotengenezwa na wale waliotengeneza ya Tetanus, TB, DPT, Polio na Hepatitis.

Tunakubali chanjo hizo bila shaka yoyote halafu tunaamini wanataka kutuua na chanjo ya COVID tena wengine wakiamini ni 'vita ya uchumi''.

Huu upuuzi unazingatiwa na wapuuzi tu, wenye akili wanauita upuuzi kama upuuzi mwingine na ni upuuzi zaidi kwa vile unafanywa na tusiowatarajia

Wiki hii shirika la Afya Duniani limetangaza uwepo wa ugonjwa wa Polio nchini Malawi.
Nchi jirani na za Afrika ikiwemo Tanzania zinachanja Watoto. Hatujasikia watu wakitilia shaka!

Tunajua shaka ya COVID ilienezwa kwa uongo na ushamba tu! kwa bahati mbaya Taifa letu halina upungufu wa majuha, wale waliomeza ujinga wakiamini TB , Tetanus etc si COVID!

Hatuna upungufu wa wajinga wanaoamini Tanzania ipo katika 'vita ya uchumi'! tukapima mafenesi

Peleka mwili wako wakaufanyie majaribio ya chanjo nyingine.
Yes chanjo ikiwepo nitachanja sihitaji kibali cha mtu lakini pia ni ukatili kuninyima haki kwasababu za uongo. Hakuna vita ya uchumi na wala hakuna hujuma.
Kilindi cha elimu duni na ushamba kisiwe chanzo cha mateso kwa wengine.
Upofu wako tu kutoona Ujasiri wake.
Ujasiri wa kupima mafenesi! na kutegemea matokeo sahihi! tafadhali bwana!!
Lakini pia si kosa KUUA mpumbavu anayeligharimu Taifa. NA HAKUANZA YEYE.
Yes! kwa wakatili kuitoa nafsi ya kiumbe si shida. Hiki ni kipimo cha utu na ubinadamu.
NAKUTAJIA VIWANDA, WEWE UNAJITOA AKILI SASA.
Ni hivi hakuna kiwanda kwa maana ya kiwanda, kuna vyerehani 3000! umeelewa
Uko na mental enslavement kwa wazungu. Unatia huruma na aibu.
Flyover si suala la Kitaifa ni miradi ya City na Municipals !
Kenya hao ambao kila mwaka wanakufa njaa?
Huwasikii hata sikumoja wakipiga debe flyover kama mwenda! njaa ya Kenya ni ukame
SITEGEMEI ICHAFUKE, ILA KWA WAPUUZI TU.
Nakuhakikishia rekodi ya Magufuli haiwezi kuchafuka zaidi! itachafuka wapi tena palipobaki?
Kama haikufanya kazi, aliwezaje kujenga viwanda 400 na vyote kufanya kazi?
Protectionism wakati wa Nyerere haikufanya kazi kwasababu viwanda vilitegemea ruzuku
Serikali iliposhindwa vikaanza kushindw kazi
Viwanda havikuwa na innovation kwasababu ya kukosa ushindani.
Siasa ikachukua nafasi ya utaalamu
Kwa akili zako nyingi kweli unafikiri Mkulima wa Tz anaweza compete sokoni na Mchina? Wanafanana nini? Je, ni teknolojia au mtaji? TUMIENI VICHWA VYENU VIZURI WANDUGU.
Yes tunaweza! tatizo ni uduni wa kufikiri. Tukibadili mind set zetu, tukajua kilimo ni kitu gani, tukawekeza, tukaweka insurance kwa wakulima wakubwa halafu tukawapa unafuu wa kodi nani atanunua vitu kutoka nje. Sasa kama wewe ni mmoja wa policy maker wa JPM haya utayazaje
UCHUMI HURIA HAUKO KUMNUFAISHA MNYONGE, MILELE
Mkulima asiyetaka competetion atabaki na jembe la mkono. Uchumi huria unafungua fursa kwa wanaotumia akili. China wakomunist wameukubali na wanatamba duniani.

Hujiulizi kwanini Precision bado wapo. Why ni FastJet tu?
Chuki tu ya Mwenda, hakuwa na maono alitaka makampuni yapndoke abaki na ATCL
Kaua ushindani sasa watu wanalipa zaidi kwasababu monopoly ya ATCL inawaumiza
 
Hatuangalii nani kiongozi au mtawala mpumbavu kwa ujumla.
Tunasema hivi Nyerere alikuwa kiongozi , Magufuli alikuwa mtawala
Ndio, usisahau na Kikwete nae.
Kiongozi anaongelea 'usisi' . Mtawala anaongelea 'umimi'.
Yes, ni wao katika umoja wa mchwa wenye njaa Kali ya kuibia Taifa.

Majina yao tu serikalini yametamalaki, nawe unajitia upofu.
Kiongozi ana ndoto , maono na mipango, mtawala ana 'ego' tu!
Ndoto, Mipango, Maono, sio Kinyume cha Ego. Wapo waliopanga Richmond, Maono ya EPA, Leo was Mafuta, Umeme, Mfumuko wa Bei, nk....

Hakuna tatizo , linakuwa tatizo pale mnapotaka liwe suala la kitaifa.
Ni tatizo mnapotumia kodi zetu kupeeleka ndege Madagascar kubeba mavumba na mchaichai
Hata Upuuzi wa Chanjo unatumia kodi zetu.
Linakuwa tatizo pale mnapowanyima wengine fursa za kufanya wanachotaka (vaccination)
Ni upumbavu kumpa Uhuru mpumbavu kuishi Upumbavu wake. Hakuna kiongozi mwerevu atakyeruhusu hilo.
Ni ukatili usiomithilika mtu kwa kinyongo tu na matamanio ya nafsi yake anapozua uongo kuwanyima wengine fursa ya matibabu
Thibitisha kwamba ni Uongo.
Kwanini tuaminishwe nyasi za Magufuli lakini tuzuiwe chanjo iliyotengenezwa na wale waliotengeneza ya Tetanus, TB, DPT, Polio na Hepatitis.
WEWE NI MUONGO ULIYEBOBEBEA, NYUNGU ZIPO HATA KABLA HUJAZALIWA. NA NYUNGU SI NYASI TU, na inawezekana bibi yako ametumia sana.
Nikuambie tu, TULIITIKIA NYUNGU, NA HOFU YA KORONA HAIPO TENA.
Tunakubali chanjo hizo bila shaka yoyote halafu tunaamini wanataka kutuua na chanjo ya COVID
Werevu hawatumii akili kama zako KUPOKEA TU KILA KINACHOLETWA.
tena wengine wakiamini ni 'vita ya uchumi''.
Dhana ya vita ya Uchumi usijiaibishe zaidi.
Huu upuuzi unazingatiwa na wapuuzi tu, wenye akili wanauita upuuzi kama upuuzi mwingine na ni upuuzi zaidi kwa vile unafanywa na tusiowatarajia
Tunafahamu, Elimu Yetu na Wasomi Wetu ndio ANGUKO letu kuu. Nawe ni mfano sahihi.

Mko brainwashed na programmed to Uzungu.
Wiki hii shirika la Afya Duniani limetangaza uwepo wa ugonjwa wa Polio nchini Malawi.
Nchi jirani na za Afrika ikiwemo Tanzania zinachanja Watoto. Hatujasikia watu wakitilia shaka!
Ni wewe tu Usiyetilia shaka, nikuambie tu wapo wengi wasiopeleka watoto wao kuchanja huo ujinga. Mimi ni miongoni mwao.
Kilichokufanya usisikie ni kwasababu, Sauti zenu ni nyingi.
Tunajua shaka ya COVID ilienezwa kwa uongo na ushamba tu! kwa bahati mbaya Taifa letu halina upungufu wa majuha, wale waliomeza ujinga wakiamini TB , Tetanus etc si COVID!
Safi kabisa Mzungu mweusi. IPO shida kubwa katika Elimu Yetu... Nawe ni mfano sahihi.
Hatuna upungufu wa wajinga wanaoamini Tanzania ipo katika 'vita ya uchumi'! tukapima mafenesi
Kaa chini, Kichwa chako hakitoshi kutafsiri Dhana hiyo, kimezidiwa na mahaba.
Yes chanjo ikiwepo nitachanja
Duh, kumbe unapotosha watu tu humu nawe hujachanja bado? Unaogopa nini?

Mnafiki sana wewe!
sihitaji kibali cha mtu lakini pia ni ukatili kuninyima haki kwasababu za uongo.
Hakuna haki ya mpumbavu kuishi upumbavu wake.
Hakuna vita ya uchumi na wala hakuna hujuma.
Kaa Chini.
Kilindi cha elimu duni na ushamba kisiwe chanzo cha mateso kwa wengine.
Chanjo IPO karibia mwaka sasa, kwanini bado unateseka sasa?
Ujasiri wa kupima mafenesi! na kutegemea matokeo sahihi! tafadhali bwana!!
Msomi wewe umekosa hata huo.
Yes! kwa wakatili kuitoa nafsi ya kiumbe si shida. Hiki ni kipimo cha utu na ubinadamu.
UTU SIO HURUMA ndugu, Muafrika alipompokea na kumkarimu Mkoloni, ule haukuwa UTU bali Upumbavu.
Ni hivi hakuna kiwanda kwa maana ya kiwanda, kuna vyerehani 3000! umeelewa
Wewe ni mlevi wa chuki zako. Tembelea vyerehani vya Tiles Pwani-Mkuranga.
Flyover si suala la Kitaifa ni miradi ya City na Municipals !
Hilo linabatilisha nini kwahiyo?
Huwasikii hata sikumoja wakipiga debe flyover kama mwenda! njaa ya Kenya ni ukame
Tembelea hata humu kwenye jukwaa la Kenya. Sijui kwanini unapenda kusema uongo.
Nakuhakikishia rekodi ya Magufuli haiwezi kuchafuka zaidi! itachafuka wapi tena palipobaki?
Ndio, ni CHAFU 100% kwa vipofu. Busara inasema, wapuuzwe tu.
Protectionism wakati wa Nyerere haikufanya kazi kwasababu viwanda vilitegemea ruzuku
Serikali iliposhindwa vikaanza kushindw kazi
Viwanda havikuwa na innovation kwasababu ya kukosa ushindani.
Siasa ikachukua nafasi ya utaalamu
Vilifikaje 400 kama alifeli, na kwanini vilikufa baada ya yeye kuondoka?
Yes tunaweza! tatizo ni uduni wa kufikiri.
Na ninyi ndio wasomi Wetu.
Tukibadili mind set zetu,
Nani wa kuzibafilisha, na kwa namna gani? Hivi mfano wako wewe na Mindset yako juu ya Uzungu, na ni msomi, Unajikomboaje? Unawezaje kufuta utumwa wa KUSUJUDIA vya mzungu? Utaanzaje?
tukajua kilimo ni kitu gani, tukawekeza, tukaweka insurance kwa wakulima wakubwa halafu tukawapa unafuu wa kodi nani atanunua vitu kutoka nje.
Hao wakulima wakubwa unawatoa wapi, na utawapataje wasio chini ya MNC's za hao wazungu wako?
Tangu Nyerere ni karibia muaka 40, kati ya hiyo ni miaka 5 tu ndio tulikuwa chini ya mtawala,miaka 35 chini ya viongozi. KWANINI BADO HATUKUPIGA HATUA?
Sasa kama wewe ni mmoja wa policy maker wa JPM haya utayazaje
Kwamba umewaza jambo kubwa ubadhani? Hivi unaijua vizuri mitego ya Umasikini Wetu au?

Umizeni kichwa, ndio maana huwa mnashindwa kuwaelewa werevu wachache.

Unasemea Bima eti, China na Tz ni Serikali ipi yenye uwezo wa kutoa BIMA yenye Nguvu kwa mkulima wake?
Nilipokuambia hatuwezi kufanana Mitaji, ulipaswa kutafakari, sio kukurupukia joja tu.
Mkulima asiyetaka competetion atabaki na jembe la mkono. Uchumi huria unafungua fursa kwa wanaotumia akili. China wakomunist wameukubali na wanatamba duniani.
Uchumi huria ni njia tu ya kujihakikishia mirija ya unyonyaji. Ni mpumbavu tu anayeweza kufikiri watu wanaotofautiana;
Mindset yao na wateja kwao,
Technology,
Exposure,
Government Support,
Research Power,
Na kila kitu, kwamba ukiwaacha huru hiyo itakuwa ni Fair Competition.

Sijui mmelishwa matakataka gani kukubali upuuzi huu hakika.

Chuki tu ya Mwenda, hakuwa na maono alitaka makampuni yapndoke abaki na ATCL
Kaua ushindani sasa watu wanalipa zaidi kwasababu monopoly ya ATCL inawaumiza
Kwanini ni FastJet tu na so Precision Air?
Mengine yahabaki kuwa hisia zako tu.
 
Ndio, usisahau na Kikwete nae.
Mafanikio au makosa ya Kikwete hayawezi kuwa utetezi kwa Magufuli.
Kila mara nakwambia kwamba rekodi ya Magufuli haiwezi kujitetea au kutetewa

Kila zama na kitabu chake, sasa ni kitabu cha Magufuli mbele ya umma! Kinasomwa , kinachambuliwa! rekodi ipo mubashara itasemwa tu! au '' Marehemu hasemwi'!
Ndoto, Mipango, Maono, sio Kinyume cha Ego. Wapo waliopanga Richmond, Maono ya EPA, Leo was Mafuta, Umeme, Mfumuko wa Bei, nk....
Kila zama na kitabu chake. Rekodi ya JPM haitetewi na Richmond au EPA
Rekodi inatetewa na majibu , wapi zilipo 1.5T na 70 B? Rekodi inatetewa na haki za binadamu na utu. Rekodi inatetewa na uchumi si vita ya uchumi isiyokuwepo
Hata Upuuzi wa Chanjo unatumia kodi zetu.
Chanjo zilitolewa bure ! na pesa za UVIKO pia. Unakumbuka Bilioni 27 za EU?
Ni upumbavu kumpa Uhuru mpumbavu kuishi Upumbavu wake. Hakuna kiongozi mwerevu atakyeruhusu hilo.
Mtawala atasafisha watu anaodhani ni wapumbavu kwasababu anadhani na pengine kuhisi ni tishio. Kiongozi atawalinda wapumbavu katika upambavu wao.
NYUNGU ZIPO HATA KABLA HUJAZALIWA. NA NYUNGU SI NYASI TU, na inawezekana bibi yako ametumia sana. Nikuambie tu, TULIITIKIA NYUNGU, NA HOFU YA KORONA HAIPO TENA.
Yes hofu haipo tena! kuna aliyedhihaki hadi kanisani, well! the rest is history
Nyungu ni upumbavu uliokithiri. Mabanda ya Muhimbili yapo wapi?
Nchi ikawa na viongozi ' laughing stock' ya dunia wakijua nyungu ni 'dupe'. Wakafanya kwa ukatili
Kwamba nyasi zinatibu tu bila kujua ni nyasi gani! ilimradi tu zinapatikana uani!
Dhana ya vita ya Uchumi usijiaibishe zaidi.
Hakuna vita ya uchumi! kama ipo mbona hatuisikii. Ilikuwa delusion tu!
Ni wewe tu Usiyetilia shaka, nikuambie tu wapo wengi wasiopeleka watoto wao kuchanja huo ujinga.
Yeah kama mtu hapeleki mtoto kuchanjwa Tetanus, TB, DPT ,Polio , Hepatitis etc ni ujinga tu.
Mwisho wa siku atakwenda Hospitali kupewa dawa zinazotengenezwa na hao hao na huenda akapoteza maisha.
Mimi ni miongoni mwao.
Kama hucjachanjwa baki ulivyo, waache wanaotaka kuchanjwa wachanjwe.
Duh, kumbe unapotosha watu tu humu nawe hujachanja bado? Unaogopa nini?
Nimechanja sana na ikibidi nitachanja tena! mimi si miongoni mwa walioamini sala na maombi yanaponya bila kuvaa mask au chanjo.
Waliohubiri nyasi za ukumbini zinatibu COVID. Wakapima mafenesi na mbuzi kuridhisha nafsi zao
Msomi wewe umekosa hata huo.
Sina PhD .
Ndio, ni CHAFU 100% kwa vipofu. Busara inasema, wapuuzwe tu.
Rekodi ni chafu, inahitaji kujitoa akili kuitetea.
Vilifikaje 400 kama alifeli, na kwanini vilikufa baada ya yeye kuondoka?
Hapa ni somo tofauti wakati ukifika nitakueleza
Tangu Nyerere ni karibia muaka 40, kati ya hiyo ni miaka 5 tu ndio tulikuwa chini ya mtawala,miaka 35 chini ya viongozi. KWANINI BADO HATUKUPIGA HATUA?
Kwani kipi amefanya Magufuli zaidi ya alichofanya Nyerere?
Umizeni kichwa, ndio maana huwa mnashindwa kuwaelewa werevu wachache.
Werevu au Walevi? unaweza kuhubiri nyasi zinatibu tu bila ushahidi ukawa Mwerevu na si mlevi
Unasemea Bima eti, China na Tz ni Serikali ipi yenye uwezo wa kutoa BIMA yenye Nguvu kwa mkulima wake?Nilipokuambia hatuwezi kufanana Mitaji, ulipaswa kutafakari, sio kukurupukia joja tu.
Ukishatengeneza inferiority complex utaishi nayo tu
Kwanini ni FastJet tu na so Precision Air?
Mengine yahabaki kuwa hisia zako tu.
Hujuma zinawabebesha wananchi gharama kwasababu ATCL ina monopoly uliotengenezwa na JPM. Hii ndiyo hoja iliyopo mezani.
 
Mafanikio au makosa ya Kikwete hayawezi kuwa utetezi kwa Magufuli.
Kila mara nakwambia kwamba rekodi ya Magufuli haiwezi kujitetea au kutetewa

Kila zama na kitabu chake, sasa ni kitabu cha Magufuli mbele ya umma! Kinasomwa , kinachambuliwa! rekodi ipo mubashara itasemwa tu! au '' Marehemu hasemwi'!

Kila zama na kitabu chake. Rekodi ya JPM haitetewi na Richmond au EPA
Rekodi inatetewa na majibu , wapi zilipo 1.5T na 70 B? Rekodi inatetewa na haki za binadamu na utu. Rekodi inatetewa na uchumi si vita ya uchumi isiyokuwepo

Chanjo zilitolewa bure ! na pesa za UVIKO pia. Unakumbuka Bilioni 27 za EU?

Mtawala atasafisha watu anaodhani ni wapumbavu kwasababu anadhani na pengine kuhisi ni tishio. Kiongozi atawalinda wapumbavu katika upambavu wao.

Yes hofu haipo tena! kuna aliyedhihaki hadi kanisani, well! the rest is history
Nyungu ni upumbavu uliokithiri. Mabanda ya Muhimbili yapo wapi?
Nchi ikawa na viongozi ' laughing stock' ya dunia wakijua nyungu ni 'dupe'. Wakafanya kwa ukatili
Kwamba nyasi zinatibu tu bila kujua ni nyasi gani! ilimradi tu zinapatikana uani!

Hakuna vita ya uchumi! kama ipo mbona hatuisikii. Ilikuwa delusion tu!

Yeah kama mtu hapeleki mtoto kuchanjwa Tetanus, TB, DPT ,Polio , Hepatitis etc ni ujinga tu.
Mwisho wa siku atakwenda Hospitali kupewa dawa zinazotengenezwa na hao hao na huenda akapoteza maisha.

Kama hucjachanjwa baki ulivyo, waache wanaotaka kuchanjwa wachanjwe.

Nimechanja sana na ikibidi nitachanja tena! mimi si miongoni mwa walioamini sala na maombi yanaponya bila kuvaa mask au chanjo.
Waliohubiri nyasi za ukumbini zinatibu COVID. Wakapima mafenesi na mbuzi kuridhisha nafsi zao

Sina PhD .

Rekodi ni chafu, inahitaji kujitoa akili kuitetea.

Hapa ni somo tofauti wakati ukifika nitakueleza

Kwani kipi amefanya Magufuli zaidi ya alichofanya Nyerere?

Werevu au Walevi? unaweza kuhubiri nyasi zinatibu tu bila ushahidi ukawa Mwerevu na si mlevi

Ukishatengeneza inferiority complex utaishi nayo tu

Hujuma zinawabebesha wananchi gharama kwasababu ATCL ina monopoly uliotengenezwa na JPM. Hii ndiyo hoja iliyopo mezani.
Kila la heri ndugu. Endelea na kasumba zako.
Ushauri tu, Dunia imejaa Viini Macho vingi. Wachache wavionavyo hufanywa kuwa si kitu.
 
Ahsante ! nami pia nasema kila la kheri

Yes! viini macho vipo sana.
Kutumia moshi ya nyasi kuponya mapafu yaliyoharibiwa na Virus ni kiini macho
Kuzusha vita isiyokuwepo nacho ni kiini macho
Kuwa na cherehani nyingi na kuziita viwanda ni kiini macho
Kupima mbuzi na mafenesi kwa kipimo kisicho rasmi ni kiini macho

Orodha inaendelea ....
 
Usije sahau na wadaio kulinda Miili na Afya zao wakati Fikra zao ni mfu tayari. Wanafanya kazi bure.
 
Kuna mzee anaitwa Hasim Rungwe juzi kasema Magufuli hakujenga kiwanda ingawa alikuwa na sera ya viwanda. Mzee huyu amekosea wapi?
Tumeuliza hapa jamvini tukaambiwa kajenga kiwanda cha Tiles Mkuranga! Tiles!!

Tuonyesheni kimoja tu kama Urafiki
 
Hao ndio watu wenye Fikra mnzaoweza kuzijadili, nyingine zimewazidi kimo.

Fikra za Watu wa Ubwabwa na Pilau ndizo zipatazo nguvu kwenu.
 
Hoja hapa ni moja Mzee Rungwe kama wlaivyo Watanzania wengine kauliza , viwanda vya Magufuli ambavyo tuliambiwa vipo 3000 vipo wapi? Hebu tuonyeshe 3 tu kikiwemo cha Tiles! Tiles Mkuranga !
 
Baada ya vitatu utaongeza vinne, kisha kumi na kuendelea.
Asiyeshiba kwenye sinia.....

Mtu anayediliki kusema HAJAJENGA CHOCHO/HATA CM MOJA, HANA JIPYA LOLOTE, NYASI, MSHAMBA..... Aoneshwe nini zaidi kukidhi haja ya hulka zake zaidi kuitikia tu matamanio yake!?
 
Of course kila kiongozi atatembea na legacy yake

Legacy ya Nyerere ni pana hailinganishwi na kitu kingine
Mapungufu ya Nyerere; kuingiza siasa katika kazi na uchumi, kuua vyama vya ushirika

Legacy ya Mwinyi ni kufungua Uchumi na kuleta mageuzi ya siasa za nchi
Mapungufu; kuacha mchwa na wezi kutamalaki , kukosa dira ya uchumi

Legacy ya Mkapa ni kukuza uchumi ! mafanikio ya sasa ni matokeo ya legacy yake
Mapungufu; kuuza na kubinafsisha mali za umma hovyo

Legacy ya Kikwete; kukuza demokrasia ! katiba mpya ingalikuwa legacy y kama asingeharibu
Mapungufu: alizingirwa na makundi , alikuwa mdhaifu kusimamia masilahi ya umma

Legacy ya Magufuli ni kufuatilia miradi kwa ukaribu
Mapungufu ; kutojali utu na maisha ya watu, kutenda bila plan,kuligawa taifa kidini na ukanda

Nikijibu bandiko lako, kama unadhani si kweli tuonyeshe cm 1 ya reli aliyeojenga siyo kukarabati. Tuonyeshe barabara aliyejenga siyo kukarabati

Nyasi: alihubiri watu wafukize minyasi isiyojulikana kwa jina la nyungu. Watu waliokuwa na maradhi mengine (underline disease) kama asthma (pumu) moyo na pressure walifukiza tu hatujui hatma zao.

Kuna mambo kama vita ya uchumi ni ushamba tu, hakuna kitu hicho. Alizua tu!
 
Of course kila kiongozi atatembea na legacy yake

Legacy ya Nyerere ni pana hailinganishwi na kitu kingine
Mapungufu ya Nyerere; kuingiza siasa katika kazi na uchumi,
Aliyekuambia vinatenganishika amekudanganya. Amka, usikariri.
What matters ni Mazingira na Nyakati husika.
kuua vyama vya ushirika
Vilianzishwa na nani?
Legacy ya Mwinyi ni kufungua Uchumi na kuleta mageuzi ya siasa za nchi
Werevu wanahoji Tija na Nafasi Yetu.
Mapungufu; kuacha mchwa na wezi kutamalaki , kukosa dira ya uchumi
Yote haya ni Kutosimamia Maslahi ya Umma.
Legacy ya Mkapa ni kukuza uchumi ! mafanikio ya sasa ni matokeo ya legacy yake
Alikuzaje?
Mapungufu; kuuza na kubinafsisha mali za umma hovyo
Kote ni Kukiuka Masilahi ya Taifa.
Legacy ya Kikwete; kukuza demokrasia !
Haijawahi kuwepo duniani, Ni kiini Macho. Alikuza kiini macho labda.
katiba mpya ingalikuwa legacy y kama asingeharibu
Hukuwa na haja ya kuitaja sasa.
Mapungufu: alizingirwa na makundi , alikuwa mdhaifu kusimamia masilahi ya umma
Usimsafishe, hakuzingirwa na makundi, Bali alijitengenezea makundi ya upigaji mengi. Hakuwa dhaifu, Bali ALIJUA ANACHOKIFANYA.
Legacy ya Magufuli ni kufuatilia miradi kwa ukaribu
Umejitahidi kujitutumua.
Mapungufu ; kutojali utu na maisha ya watu, kutenda bila plan,kuligawa taifa kidini na ukanda.
Umesahau kumuongezea na mapungufu ya wengine wote hapo juu.

Kutolinda rasilimali za Taifa, wizi, makundi, dhaifu, kuua mahusiano, kutokuwa na dira ya uchumi, nk
 
What matters ni Mazingira na Nyakati husika.
Nyerere alianza uongozi wakati mgumu kuliko wote waliofuata.
Hakuwa na wasomi, hakuwa na infrastructure na hakuwa na resources za kutosha

Tukiangazia mengi aliyofanya na ni 'kashfa' kubwa kumweka katika mizani na mwingine.
Rekodi ya Nyerere katika taifa hili ni 'unique'

Kuchukua nchi yenye dini tofauti na makabila tofauti na kuiuanganisha ni jambo gumu sana

Nigeria na majirani Kenya au Uganda, miaka 60 bado zimwi la ukabila na udini linawatesa sana. Tanzania tulishaondoka huko aliyeanza kuturudisha huko ni Magufuli

Ukishaanza kuwatazama wananchi kwa jicho la dini na makabila tayari unawagawa
Mfano rahisi tu, JPM alikuwa na salam za kidini. Hili ni jambo baya sana , Tanzania ni SECULAR country. Kuna dini tofauti , watu wenye dini za asili, Wasio na dini na Wasioamini

Kusalimia kwa Ukristo na Uislam ni kutenga makundi mengine na kuyajengea makundi mawili umuhimu usio na sababu wala maana. Nchi yetu ina raia wenye dini lakini serikali haina dini.

Kilichoshangaza wakati wa JPM kila jambo lilihusisha viongozi wa dini.
Hili likajenga utamaduni wa kuamini Wakristo na Waislam, utaratibu unaoiumiza Nigeria

Lakini pia teuzi zake zilitiliwa shaka, kuna kiongozi mmoja alitoa takwimu (kukamatwa) akionyesha namna udini ulivyotamalaki. Ingawa nia yake haikuwa na dhamira njema lakini likuwa ngumu kumpinga alikuwa na takwimu!!

Nyerere, katika kumaliza ukanda udini na ukabila alianzisha mifumo ya elimu iliyokuwa ghali lakini leo tunaona manufaa yake.

Watoto wa Mkoa wa Mara walisoma Tanga, wale wa Kilimanjaro walisoma Dodoma, Wa Mwanza walikwenda Mtwara , na wa Kigoma walikwenda Mbeya.

Mchanganyiko huu uliwafanya watu waone ni wamoja na wanaweza kuishi sehemu yoyote Tanzania bila tatizo. Ndiyo maana leo kuna Wasukuma Kilimanjaro na Wabondei Shinyanga.

JPM alikuja na sera ya chuki dhidi ya kanda ya kaskazini akiwataka ''wasubiri maendeleo'
Hilo limeamsha hasira si kwa kanda moja bali nyingine wakihisi kuwa Rais kutoka eneo fulani ana influence maendeleo ya eneo jingine '' positive au negative'' na si nchi kwa ujumla

Kulikuwa na sababu gani za Rais wa nchi anayetegemewa kuwaleta wananchi pamoja kutoa kauli ya kibaguzi namna ile?

Hivi ikitokea vita kama ile ya Kagera kuna kuchagua nani aende? Kwanini basi watu watengwe.

Na kuna kosa gani watu wa eneo fulani kujiletea maendeleo?

Tukiachilia mbali Nyerere kafanya nini kwa kitu kimoja kimoja, kuunganisha Taifa ilikuwa kazi muhimu sana inayomtofautisha na waliomfuata, hawakuwa na kazi hiyo na pengine walianza kuibomoa kwa kauli za reja reja na za kibaguzi

Kumweka Nyerere na mwingine katika mizani kuna matokeo mawili;
Kumtusi sana Nyerere au kumdhalilisha sana aliyesimama katika mizani na Nyerere

Back
Top Bottom