Anguko la mabenki: PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa riba katika amana za bilioni 440 TPA

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
1,768
2,766
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
 
Duuh I thick this is beyond my scope maana nimetoka patupu.Mtakao elewa mtanipa summary.
 
hii ina itwa weka mbali na majungu na siasa hapo ni patamu wezee wa cpa njooni huku mtufafanulie hati fungani ndio nn wa mtumbatu aelewe
 
Nilihisi hilo namie pia.
Waliambiwa kiutu uzima na mchezo huo ni wa muda mrefu saana Tangu enzi za Mwinyi ndio uliibuka kwa kasi ya kutisha.
Sasa kila alieingia kwenye upande huo alikuta kwamba kuna system ipo na vigogo wameisimamia inabidi uwe mpole ufuate hali ilifivyo na rhythm ya deal ilivyo.

Na ndio maana nasema kwamba kuna Banks nyingi lazima zilie kipindi hiki.Na wahusika wanajua kwanini hali inaelekea hivi na ndio maana hata Banks zenyewe hazijitoi kusema hali za banks zao,maana wanajua nini kimewafikisha hapo na Safari yao inaelekea wapi.

Aisee,sasa hivi waliokuwa wanatesa sasa naoa wanateseka,yaani mtu anaishi Jumba la maana wala hana raha kabisa ya maisha.Hahaha,Maana mifumo inabuma kwa kasi ya ajabu
 
Tatizo hata mfanyeje ila kama maskini hawapati mikopo. Madawa hakuna ajira hakuna..
Hata mpate mapato trilion 102 kwa mwezi.
Wananchi hawaelewi kitu na hakuna lolote ni porojo tu
 
Ila nchi ilifika pabaya. Kuna jamaa mtumish wa umma Na mke Wake walinunua apartment saba za NHC kwa kesh kabla ya uchaguz October 2015. Na apartment hizo alizonunua siyo chini ya million 200.
 
PAC yaagiza ukaguzi maalum ufisadi wa Riba katika amana za bilioni 440 TPA; Wizi hufanyika hivi!

Kamati ya fedha za serikali (PAC) imemuagiza CAG na BOT kukagua ubadhirifu wa riba/faida ya akaunti za muda maalum kiasi cha shilingi Bilioni 440 za Mamlaka ya bandari, zilizowekwa katika benki zifuatazo CRDB,NBC,NMB na Standerd Charterd bank.

-Kiasi hicho cha 440 Bil. Kimewekwa katika fixed deposit ya mwaka na kuzaa Bilioni 17 tu sawa na wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.

Uhalisia kwa riba za kawaida kwa ‘fixed deposit’ chini ya milioni 100 ni asilimia 8 mpaka 10, lakini pesa zinapoongezeka huongezeka hadi kufikia asilimia 15 ili benki ivutie amana zaidi ambazo kimsingi huziwekeza kupitia mikopo na kununua hati fungani za serikali. Tuseme, benki zitoe riba ya asilimia 13 kwenye amana za Bilioni 440 Bandari ingepata si chini ya shilingi Bilioni 57.2 kabla ya kodi (51.7 Bilioni baada ya kodi), kwa hiyo serikali (wananchi wameibiwa takribani Bilioni 40 kwa mwaka 2014/2015.

Mbaya zaidi pesa hizi bilioni 440 zinapokuwa kwenye mabenki ya biashara, serikikali hukopesha pesa hizi (pesa zake) kupitia ‘treasury bills’/hati fungani kwa riba ya hadi asilimia 15 kwa mwaka. Hivyo wananchi hilipa mabenki haya riba ya hadi shilingi Bilioni 66 kwa hela ambayo ni ya kwa wenyewe. Sasa ukijimlisha hasara kamili kwa mwaka utakuja wananchi/serikali inapata hasara ya Bilioni 66+ Billioni 40 (riba inayopunjwa na benki kwa pesa zilizoko kwenye ‘fixed deposit’= 106 Bilioni, sasa chukua mashirika mengine kama EWURA, TANAPA, SUMATRA,na mamaka mbalimbali utagundua ni kiasi gani wananchi wanaibiwa kupitia mabenki kila mwaka. Hapa huhitaji kuambiwa uzalendo wa JPM na Waziri wa Fedha Dr. Mpango.

Jinsi gani wizi huu unatekelezwa;
Maafisa wa benki (treasury/dealers/CEOs) na maafisa wa bandari huungana kufanya wizi huu kwa makusudi. Benki za biashara hutenga fungu/kasma maalumu kwa ajili ya kuwalipa maafisa wa mashirika ya umma ambao watafanikisha wao kupata fedha hizi ili kufikia malengo yao kibiashara. Kuna sera maalum kabisa, unakuta asilimia 10 ya faida (57.2) ni ‘commision’ ya maafisa wa serikali na asimia 10 nyingine hulipwa kama ‘bonus’ kwa maafisa wa benki kwa kufikia malengo ya biashara (target); kwa hiyo hela hizi kwa benki hutoka kama matumizi ya kawaida na wanajua jinsi wanavyogawia maafisa wa serikali. Ni ngumu kwa benki inayofuata maadili kupata biashara hii, hata uwe na maafisa masiko wazuri vipi, hata benki yako itoe ofa ya interest rate ya 15 kwa fixed deposit kamwe hutapata amana hizo huu ni mtandao wa wizi.

Vile vile maafisa hawa wa benki huungana na maafisa wa serikali kuibia serikali kupitia mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni. Kanuni ni ile ile. Ikiwa serikali inataka kununua fedha za kigeni, bei hutolewa ya juu mfano badala ya kuuza dola moja kwa shilingi 2100 serikali inauziwa dola moja kwa shilingi 2200, fikiria kama serikali inafanya manunuzi ya dola milioni 20, huishia kupata hasara ya shilingi milioni 200.

Baadhi ya wati sasa wataelewa ni kwanini baadhi ya wakuu wa baadhi ya benki na mashirika ya umma walipiga kelele pale Raisi alipoamuru fedha zote za taasisi za umma zirejeshwe benki kuu. Si kwamba walimaanisha, hapana walijua mwisho wao umefika. ‘Performance’ yao halisi itajulikana kwani walitumia fedha za rushwa kufanya biashara na kupata faida kubwa. Benki nyingi zinapitia uhalisia,zimekwama njia pekee iliyobaki ni kubuni mbinu mpya haswa bidhaa mpya kwa ajili ya wananchi na si kuvizia matrilioni ya serikali. Serikali ni mteja na ana haki ya kuchagua mahala pa kuweka fedha zake na kiutamaduni benki ya serikali ni Benki kuu si benki za biashara.Hawa wote ni wateja wa mahakama ya mafisadi.

Mtandao huu una nguvu, umetumia ukwasi huu kuwalipa waandishi wa habari kupotosha mengi ili kuficha ukweli. Nampongeza Raisi Dr.Magufuli, hajakubali kugeuka jiwe,siku hata siku mambo yao yanaanikwa hadharani na ripoti za CAG, ukweli haupendi kupuuzwa.Tunataka Tanzania Mpya.
Hapo ni nihuyo kiongozi hapo juu Chadema .vinginevyo hapo ni wanaende sehemu nyeti za chama tawala .utasubiri sana kuona hatua zikichukuliwa na zikichukuliwa utaona vile chama kitakavyo pauka
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom