Angry MPs reject Karamagi’s Energy petrolium Bill

Jamani Wabunge wa CCM si ni wanasiasa? wamejifunza kuhusu shavu waliokula Dr. Slaa na Zitto. Sasa kila mmoja anajifanya anajututumua. Mi nathani huu ni usanii tu. EL atawaita na kuwashikisha adabu wote hiyo kesho. Then case closed. Mabadiliko ndani ya CCM ni magumu maana kuna walioshika mpini(walioko serikalini) na walioshika makali. Biti you hao wabunge ni ndogo tu " Tuone kama jina lako litarudi 2010" wote wanafyata mkia na kuunga mkono.The bottom line ni kuwanyima kura tu 2010 Basi.
 
Yeah, amejitolea sasa nilikuwa natoa pendekezo tu kwani huo utakuwa ni ujumbe mzito kabisa wa yeye kujitoa mhanga kwa ajili ya Taifa lake.
 
Naomba Mungu asikilize maombi ya huyo mbunge wapungue maana ni wengi wasiotusaidia kwa lolote,ni mzigo usio na sababu kwa walipa kodi walalahoi wa bongo.

Nasikia el anakutana na wabunge mafisadi kama kamati so huu moto mwisho wake ni kesho. We won't hear hbr kama hizi kwa muda unless mtu yuko tayari kujitoa mhanga na kiti chake pia.

Kitu kingine kibaya kuna heresays kwamba el na hao wabunge mafisadi wataijadili report ya Richmond kabla ya kujadiliwa bungeni. What is this jamani hii nchi ni yao peke yao kiasi wanaweza kufanya watakavyo?Me nimechoka nauza uraia, ukisikia mtu anataka uraia wa tz aje nitamuuzia just let me know kwa kweli.
 
jealous-fisherman.jpg

Brazameni,

Sasa hiyo ndio ndoano ya huyo Mbunge ajitungike ili afe au vp? Cant get it!

By the way welcome back na mbona umeibuka blue monday? si ungesubiri hadi ijumaa ili mambo yakawa mambo...
 
..tatizo tukipewa estimates za kuifanyia marekebisho TANESCO tutasema ni bora pesa hizo zingetumika kujenga hospitali, mashule, etc etc.

..katika hoja kama hiyo Mbunge alipaswa kutoa mapendekezo ya nini kifanyike.

..zaidi alipaswa kuchambua hoja yake, akizingatia gharama, vyanzo vya fedha,na faida za muda mfupi na mrefu.

..kwenye nchi za wenzetu, serikali ikiwasilisha mswada, basi wabunge nao wanaweza kuwasilisha mswada-mbadala[alternative bill].
 
Heshima wakuu..... Kwanza nampongeza ndugu yetu Mheshimiwa kwa kutuonyesha kwamba kweli kuna watu wako tayari kurudisha ile G57 (mnaikumbuka wakuu ile miaka ya 90???). Hii ikirudi nadhani kidogo imani na Bunge letu Tukufu itarudi especially wakati huu wa MAFISADI......

Kuhusu issue ya TANESCO, hii kuna thread watu walikuwa wameshaitolea hoja za nguvu (kwa kweli ni nyingi na ni nzuri) hivyo nadhani hoja ya TANESCO izungumziwe kule kwenye uchumi (kama sikosei)...... Siwezi sema mengi sababu kwa kweli ripoti yenyewe haipo ila ni ripoti ya Wahandishi wa habari ambao hoja kuu kwenye hili haikuwa TANESCO bali Mbunge kupinga hoja... Wenye Data tunaomba mtuletee hii ripoti ili tuone kunani humo ndani yake!!!?????
 
Nikipiga picha ya Tanzania ijayo nachanganyikiwa sipati picha Watanzania wenzetu watakavyokuwa, tumeuza viwanda, madini sasa tunauza vinu vya umeme tumewauzia wageni ambao watakuwa wanagonganisha glasi za mvinyo na serikali ikiwa `house boy na house girl` wananchi nao wakibakia kuwa watumwa`` ilisema sehemu ya ujumbe huo uliosomwa na Dk. Mwakyembe.

Alitaka serikali ibaki na vinu na vyanzo vya kuzalisha umeme na wawekezaji waruhusiwe kusambaza.

Huyu mbunge naheshimu sana mawazo yake...bila shaka darasa limetumika na sio ulafi wa utajiri wa haraka haraka.
 
Nina omba mjue kwamba ni baada ya makelel ya JF na baadhi ya mijadala ya watu wenye usongo kwenye TV prog za hapa nyumbani na Dr.Slaa na Zitto na watu kuanza kuwazomea na kuwatukana kwa uwazi ndiyo maana wachache wameanza kuamka . Wanawasikia wananchi wanayo yasema na hata Kenya wamejionea wenyewe so nadhani they are serious kama si danganya toto . Unajua madongo ya JF wanapekewa live wengine wana watoto wao humu humu na ndugu zao . Sasa JF ndiyo macho na masikio ya watanzania . JF baada ya akina Zitto ndiyo chombe pekee tunapo anika hata kama ni speculations mwishowe huwa ni ukweli sasa wanakwama kabisa . Tuendelee kukata issue kwa nguvu hapa tuache mchezo .

JF ni kiboko ya njia ndio maana inakua kila kukicha maana ukichungulia tu hapa basi utataka kujiunga ili ushiriki katika mapambano dhidi ya ufisadi maana kwa namna moja au nyingine utakuwa umeguswa na ufisadi unaondelea. JF is no perfect but is far better off as compared to chama cha mafisadi~CCM.

Mungu ibariki Tanzania
 
Sijui hata mnachowasifu hao wabunge ni kitu gani hapo?bill imewekwa hapo for discussion na kama wana cha kuongeza/kupunguza waweke maana ndio kazi yao lakini kukataa flat out hata kuiongelea sijui ni kwa faida ya nani? maana hata sheria za sasa kuhusiana na Petrol zina loopholes za rushwa na hazisaidii nchi kwa hiyo ndio tuendelee nazo? na what i know hii bill mpya kuhusu energy ingeondoa monopoly ya Tanesco kitu ambacho ni kikwazo kikubwa sana kwa serious investors,kama wako serious na wanatutakia mema si bora wangekuja na cha maana kuliko kukataa kuongea na sijui kama investors wana interest ya kununua hilo shirika,investors wanachotaka ni haki ya kuzalisha,kusambaza na kuuza ambapo sheria za sasa haki hiyo ni ya Tanesco peke yake...na tukiendelea na hii sheria umeme tusahau,free market rules sio monopoly ambazo ni kikwazo kwa maendeleo.
 
Back
Top Bottom