Angry MPs reject Karamagi’s Energy petrolium Bill

Slowly this wabunge are coming to their senses.

They have to learn from Slaa and others.

Nasikia tangazo la naibu spika kuwa spika wa bunge amesitisha safari na anarejea bungeni kesho.
 
Nina omba mjue kwamba ni baada ya makelel ya JF na baadhi ya mijadala ya watu wenye usongo kwenye TV prog za hapa nyumbani na Dr.Slaa na Zitto na watu kuanza kuwazomea na kuwatukana kwa uwazi ndiyo maana wachache wameanza kuamka . Wanawasikia wananchi wanayo yasema na hata Kenya wamejionea wenyewe so nadhani they are serious kama si danganya toto . Unajua madongo ya JF wanapekewa live wengine wana watoto wao humu humu na ndugu zao . Sasa JF ndiyo macho na masikio ya watanzania . JF baada ya akina Zitto ndiyo chombe pekee tunapo anika hata kama ni speculations mwishowe huwa ni ukweli sasa wanakwama kabisa . Tuendelee kukata issue kwa nguvu hapa tuache mchezo .

Lunyungu:

Sikumoja mtaniuliza how does that work? And I will show each details kwanini JF inachangia kubadilika kwa hali ya kijamii ya Taifa TZ. Haionekani moja kwa moja but contribution is massive! Lets be sensible..passistent...and focused..MAFISADI Tutawapiga chini!!!
 
Ushirombo;

Nasikia Mama alitoka mzimamzima! With all her heart..emotionaly and physiacly! Usiombe kumuona mwanamke akiwa kwenye hiyo state!!!

Azimio Jipya,

Yaani woga ukiwatoka wabunge wetu mambo ya 'Kishenzi na Kijinga hawawezi pita kilaini, Bunge ni muhimili mkubwa katika kuleta mabadiliko, tuendelea kuwa na wabunge wa kutia mihuri maamuzi yoyote ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi, ni wakati pia akina Mudhihiri wakubali kuichallenge serikali maana wananchi ndo wanaoweza kuwarudisha bungeni, wakipigwa longo longo basi wa cross boarder napenda mbunge anayeka maslahi ya nchi mbele bila kujali anatoka chama kipi ndo maana narudia kusema I Love mama Anne Kilango Malecela.....
 
Jamani hii habari mimi sina tatizo nayo, tatizo langu ni hapo inaposema "the seminar Charman, Dr Harrison Mwakyembe" na hapo inaposema "the seminar chairperson, Ms Anne Malecela ".

Jee seminar ilikuwa na wenyeviti wangapi? au sijaelewa vizuri naomba nifahamisheni.
 
Mambo ya lugha tu hapo ....grasp the content ndugu, chairman ama chairperson is not an issue...
 
I think Karamagi didn't see this coming.... poor Karamagi!!!

he wouldnt see it coming if u attached a torch to it!The guy is not a politician,he is a businessman.

Kama mtu unaweza kuzika watu kwenye biashara,unadhani kweli akiwa waziri atawajali wananchi???
 
Hivi vikao vya Wabunge wa CCM ndiyo vitawamaliza na si ajabu wakitoka huko watakuwa ni wengine kabisa!
____________________________________

CCM MPs to discuss position on Richmond

-PM Lowassa to chair crucial caucus meeting ahead of next week's debate

THISDAY REPORTER
Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) legislators are set to hold a crucial caucus meeting here tomorrow, ahead of the upcoming parliamentary debate on the final report of a Bunge committee assigned to investigate the controversial Richmond power generation deal.

Insiders have told THISDAY that the meeting will also discuss the Bank of Tanzania (BoT) special audit findings, whose report is also expected to come up for debate in the House next week.

The meeting, to be chaired by Prime Minister Edward Lowassa by virtue of his position as the official leader of government business in the National Assembly, is expected to seek a common ground on both sensitive issues.

The regular caucus meetings of ruling party MPs usually determine matters of policy, parliamentary strategy and tactics, and even disciplinary measures to be taken against ’disobedient’ or rebel MPs who do not tow the party line.

’’We have already been notified that there will be a meeting on Tuesday (tomorrow) to discuss what our position as CCM lawmakers should be on the Richmond and BoT audit debates next week,’’ one ruling party MP, who asked not to be named, told THISDAY.

The secretary of the CCM parliamentary caucus, Ali Ameir Mohamed (Donge-CCM), also confirmed that the meeting would be held tomorrow, but insisted that it was just a normal meeting held regularly, and was not being specifically convened to discuss the Richmond and BoT issues.

It has been suggested that even though the caucus may try to bring maverick lawmakers in line beforehand, several senior government officials should expect a ’’serious telling off’’ from ruling party MPs when the Richmond and BoT debates come up in parliament.

’’President Kikwete has given us the go-ahead to reprimand even ministers who have become a burden to the government - and we intend to do just that,’’ said another CCM lawmaker.

Although findings of the parliamentary committee on the dubious Richmond deal have not yet been made public, well-placed sources are already describing the report as a ’’bombshell.’’

To demonstrate the seriousness of the matter, the Speaker of the National Assembly, Samwel Sitta, who flies to the US this week, has put a temporary hold on the much-anticipated House debates on Richmond and BoT until he returns next week.

Sitta has instructed the Deputy Speaker, Ms Anna Makinda, not to allow MPs to debate either of the two topics during his absence because he wants to personally preside over the matter.

He assured THISDAY that both debates will now take place during the third and final week of the current Bunge session (February 11 to 15).

The parliamentary committee that investigated the controversial, 172.9bn/- Richmond power generation deal was chaired by Dr Harrison Mwakyembe (Kyela-CCM). Other members were Ms Stella Manyanya (Special Seats-CCM) as vice-chairperson, Lucas Selelii (Nzega-CCM), Herbert Mntangi (Muheza-CCM) and Mohamed Mnyaa (Mkanyageni-CUF).

There were reports of high-level meddling during the parliamentary probe on Richmond, with the committee warning at one point that some testifying witnesses faced the risk of perjury for deliberately misleading the investigation.

A government procurement watchdog has also issued an official report saying the process that eventually led to the awarding of the contract to the US-based Richmond Development Company was interfered with by high-level government officials.

According to the report by the state-run Public Procurement Regulatory Authority (PPRA), Richmond was awarded the contract despite having already been disqualified as incompetent by the Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO).

The parliamentary inquiry into the Richmond affair followed dissatisfaction voiced by many MPs over the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB)?s declaration last May - after conducting its own investigation - that the deal was ’’clean.’’
 
Hawa wabunge wa CCM wameshaona raia hatuwafagiliii baada ya lile sakata la zitto kuonekana walitetea zaidi maslahi ya chama kuliko Taifa,sasa wameanza kuamuka. Wasiwasi wangu ni watakapoitwa kwenye kikao cha chma walazimishwa wakubaliane na hoja kwa kuzingatia msimamo wa chama,je wataendelea kusimama hivyo hivyo.
 
Mbunge atamani afe mapema

2008-02-04 09:20:04
Na Restuta James, Dodoma

Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene (CCM), ameomba afe mapema kukwepa fedheha itakayolikumba taifa kufuatia raslimali zake kumilikishwa wageni.

Aidha, amesema wananchi hugeuzwa watumwa na serikali kufanywa kuwa `house girl na house boy.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati wa semina ya wabunge ya kujadili miswada ya sheria ya nishati inayolenga kutunga sheria ya umeme na ya petroli.

Akizungumza kwa maandishi katika ujumbe aliomtumia Mwenyekiti wa semina hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, ukiwa ni mchango aliokusudia kutoa, alisema anatamani kufa mapema ili asione aibu hiyo itakayoletwa na kubinafsisha sekta muhimu na raslimali za nchi ukiwemo umeme.

``Nikipiga picha ya Tanzania ijayo nachanganyikiwa sipati picha Watanzania wenzetu watakavyokuwa, tumeuza viwanda, madini sasa tunauza vinu vya umeme tumewauzia wageni ambao watakuwa wanagonganisha glasi za mvinyo na serikali ikiwa `house boy na house girl` wananchi nao wakibakia kuwa watumwa`` ilisema sehemu ya ujumbe huo uliosomwa na Dk. Mwakyembe.

Alitaka serikali ibaki na vinu na vyanzo vya kuzalisha umeme na wawekezaji waruhusiwe kusambaza.

Katika semina hiyo ambapo wabunge walizungumza kwa ukali, kujiamini na kufoka, Naibu Spika Bi. Anna Makinda, alianza kuwakosoa wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwemo wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), Kamishna wa Nishati na Mwanasheria waliotoa utangulizi wa maelezo ya miswada hiyo akisema hakuna cha `maana` walichowasilisha.

Alisema wabunge wanataka kujua sheria mpya za umeme na petroli zitawanufaisha vipi wananchi na tofauti zitakazorekebisha hali ilivyokuwa zamani na kwamba maelezo hayo hayajatolewa.

Aliwaponda maofisa hao kwa kuonyesha picha za video zisizoelimisha na kuwaonya kuwa hayo si masuala wabunge waliyoyategemea.

Kamishna wa Madini Bw. Bashiri Mrindoko alionyesha video iliyozungumzia ufanyaji wa biashara haramu za mafuta kwenye vituo vya mauzo.

Kwa upande wake Mbunge wa Vunjo, Bw. Alloyce Kimaro (CCM) alisema Wizara ya Nishati na Madini imepoteza sifa na haina hadhi ya kuzungumza na wabunge ina kashfa nyingi kama za IPTL, Richmond, Songas na Net Group Solutions.

IPTL ni mwekezaji wa Malaysia aliyeingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha umeme wa dharura wa dizeli ambaye analipwa Sh. bilioni tatu kila mwezi bila kujali anazalisha umeme au lah hata kama mabwawa makubwa ya Mtera na Kidato yamejaa maji jambo linalolalamikiwa kuwa ni kumtajirisha mwekezaji mgeni kupitia mikataba `mibovu`.

Kwa upande wake, Mbunge wa Muheza, Bw. Mtangi (CCM), aliiponda TANESCO kuwa iko taabani imelazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) na kuhoji kama iko taabani hakuna haja ya kuleta muswada mwingine wa kuruhusu wawekezaji kushindana na mgonjwa aliye karibu kukata roho.

Semina hiyo iliahirishwa na mwenyekiti wa kikao Dk. Mwakyembe baada ya wabunge kukataa Naibu Waziri wa wizara hiyo Bw. William Ngeleja kuifunga.
 
Changa la macho tu... Cant u see the bigger picture? Reshuffle is coming na kila Mbunge (CCM) ana matumaini ya "kukumbukwa" na ili "ukumbukwe" lazima "ubwake" kidogo.... Hah hah another goli la kisigino!
 
Sidhani kama hili ni goli la kisigino kama unavyodai. Ninavyodhani mimi haya ni matokeo ya wananchi kuzomea mawaziri na wabunge wao, kwamba wabunge na mawaziri wasipokomaa sasa basi huenda wakarushiwa mawe na mchanga huko majimboni kwao mara wamalizapo kikao hiki, kwani makali ya umeme na bei za vitu mbali mbali zimefikia mahali pabaya pasipovumilika.
 
Kama wana uthubutu huo kwanini wasiongee hayo ndani ya Bunge lenyewe badala yake huko vipembeni kwenye semina?

We wont take them serious until the stand on the main chamber and speak out, otherwise ni usanii at best!
 
Sawa mkuu Masatu, ngoja tuone maendeleo ya mijadala ya mikataba. Kama huu ni usanii tutawananga hapahapa mchana kweupe. Ila nasikia Lowassa kawaita chemba, huenda "anawafunda nidhamu ya chama"!
 
Sawa mkuu Masatu, ngoja tuone maendeleo ya mijadala ya mikataba. Kama huu ni usanii tutawananga hapahapa mchana kweupe. Ila nasikia Lowassa kawaita chemba, huenda "anawafunda nidhamu ya chama"!

Si unaona sasa mkuu... wakitoka huko wote wanaufyata, anyway lets wait and see lakini Im really not convinced...
 
Mbunge atamani afe mapema
2008-02-04 09:20:04
Na Restuta James, Dodoma

Mbunge wa Kibakwe, Bw. George Simbachawene (CCM), ameomba afe mapema kukwepa fedheha itakayolikumba taifa kufuatia raslimali zake kumilikishwa wageni.

Aidha, amesema wananchi hugeuzwa watumwa na serikali kufanywa kuwa `house girl na house boy.

Alisema hayo jana mjini hapa wakati wa semina ya wabunge ya kujadili miswada ya sheria ya nishati inayolenga kutunga sheria ya umeme na ya petroli.

Akizungumza kwa maandishi katika ujumbe aliomtumia Mwenyekiti wa semina hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, ukiwa ni mchango aliokusudia kutoa, alisema anatamani kufa mapema ili asione aibu hiyo itakayoletwa na kubinafsisha sekta muhimu na raslimali za nchi ukiwemo umeme.

``Nikipiga picha ya Tanzania ijayo nachanganyikiwa sipati picha Watanzania wenzetu watakavyokuwa, tumeuza viwanda, madini sasa tunauza vinu vya umeme tumewauzia wageni ambao watakuwa wanagonganisha glasi za mvinyo na serikali ikiwa `house boy na house girl` wananchi nao wakibakia kuwa watumwa`` ilisema sehemu ya ujumbe huo uliosomwa na Dk. Mwakyembe.

Alitaka serikali ibaki na vinu na vyanzo vya kuzalisha umeme na wawekezaji waruhusiwe kusambaza.

Katika semina hiyo ambapo wabunge walizungumza kwa ukali, kujiamini na kufoka, Naibu Spika Bi. Anna Makinda, alianza kuwakosoa wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwemo wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), Kamishna wa Nishati na Mwanasheria waliotoa utangulizi wa maelezo ya miswada hiyo akisema hakuna cha `maana` walichowasilisha.

Alisema wabunge wanataka kujua sheria mpya za umeme na petroli zitawanufaisha vipi wananchi na tofauti zitakazorekebisha hali ilivyokuwa zamani na kwamba maelezo hayo hayajatolewa.

Aliwaponda maofisa hao kwa kuonyesha picha za video zisizoelimisha na kuwaonya kuwa hayo si masuala wabunge waliyoyategemea.

Kamishna wa Madini Bw. Bashiri Mrindoko alionyesha video iliyozungumzia ufanyaji wa biashara haramu za mafuta kwenye vituo vya mauzo.

Kwa upande wake Mbunge wa Vunjo, Bw. Alloyce Kimaro (CCM) alisema Wizara ya Nishati na Madini imepoteza sifa na haina hadhi ya kuzungumza na wabunge ina kashfa nyingi kama za IPTL, Richmond, Songas na Net Group Solutions.

IPTL ni mwekezaji wa Malaysia aliyeingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha umeme wa dharura wa dizeli ambaye analipwa Sh. bilioni tatu kila mwezi bila kujali anazalisha umeme au lah hata kama mabwawa makubwa ya Mtera na Kidato yamejaa maji jambo linalolalamikiwa kuwa ni kumtajirisha mwekezaji mgeni kupitia mikataba `mibovu`.

Kwa upande wake, Mbunge wa Muheza, Bw. Mtangi (CCM), aliiponda TANESCO kuwa iko taabani imelazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) na kuhoji kama iko taabani hakuna haja ya kuleta muswada mwingine wa kuruhusu wawekezaji kushindana na mgonjwa aliye karibu kukata roho.

Semina hiyo iliahirishwa na mwenyekiti wa kikao Dk. Mwakyembe baada ya wabunge kukataa Naibu Waziri wa wizara hiyo Bw. William Ngeleja kuifunga.

SOURCE: Nipashe
 
Mbunge atamani afe mapema
2008-02-04 09:20:04
Na Restuta James, Dodoma

``Nikipiga picha ya Tanzania ijayo nachanganyikiwa sipati picha Watanzania wenzetu watakavyokuwa, tumeuza viwanda, madini sasa tunauza vinu vya umeme tumewauzia wageni ambao watakuwa wanagonganisha glasi za mvinyo na serikali ikiwa `house boy na house girl` wananchi nao wakibakia kuwa watumwa`` ilisema sehemu ya ujumbe huo uliosomwa na Dk. Mwakyembe.

SOURCE: Nipashe

jealous-fisherman.jpg
 
Back
Top Bottom