Angry MPs reject Karamagi’s Energy petrolium Bill

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,229
662
Angry MPs reject Karamagi’s Energy, Petroleum Bill

MEMBERS of Parliament refused unanimously Friday to listen to Energy and Minerals Minister Nazir Karamagi and his team of resource persons at a seminar convened to discuss The Electricity Act, 2007 and the Petroleum Supply Act, 2007.

The MPs demanded almost angrily to see the report of the probe team on the controversial Richmond contract before they discuss the bills which they said “would not help this country’s economy” anyway. Mr George Simbachawene (Kibakwe – CCM) was so irritated that he wrote a note to the seminar Charman, Dr Harrison Mwakyembe (Kyela – CCM), saying: “I wish to die soon so that I do not witness the plight of future Tanzanians who would not have electricity.”

He also wrote that future generations in this country would watch helplessly as so-called investors exploit their minerals. “These Tanzanians would the houseboys and girls in the homes of these rich foreign masters.” Energy Minister Karamagi walked out of the meeting head-down without being given chance by the incensed MPs to respond to their sentiments. Some legislators, who wished to remain anonymous, hinted that the current Bunge session would be stormy.

During emotional exchanges with the seminar chairperson, Ms Anne Malecela (Same East – CCM) charged that some people in government thought MPs were stupid. “This parliament is made up of upright men and women. There are no fools in here,” she said, adding that she suspected some high-placed people in government had impoverished Tanesco.

“We want to know exactly the reasons that brought on Tanesco’s critical financial problems. The company is in the Intensive Care Unit (ICU),” she said. Addressing Minister Karamagi, the Same East legislator banged her desk charging: We will not discuss your Bills even if we sit in here until tomorrow. Not even for four days.”

Dr Raphael Chegeni (Busega – CCM) demanded that privatization should be stopped.He said, “We have come to a point where privatization has thrown us into utter confusion and deeper poverty.” He told fellow legislators to refuse to be used as rubberstamps. “We should do what is expected of us by Tanzanians. Short of this we all should resign.”

Mr Said Amour Arfi (Mpanda Kati – Chadema) charged that the reasons that threw Tanesco into the ICU were political. He said some of the power supplies are located in uneconomic zones. He also demanded to know why Artumas used Tanesco power lines.

Mr Benson Mpesya (Mbeya Urban – CCM); Mr Abdulkarim Shah (Mafia – CCM); Mr Herbert Mntangi (Muheza – CCM); Mr Job Ndugai (Kongwa – CCM) and Mr Juma Killimbah (Iramba East – CCM) demanded separately that the seminar be closed. Mr Michael Laizer (Longido – CCM) did not see why MPs who hail from districts that do not have power were in the seminar. “Why should we discuss these Bills? Our districts do not have electricity. And what happened to rural electrification schemes?”

Mr Laizer told the chairman to close the seminar because the legislators were not in the mood to discuss anything substantial. Mr Hamad Rashid Mohamed (Wawi – CUF), criticized the Bills saying not enough effort had gone into their formulation. The Electricity Act, 2007 seeks to provide for the facilitation and regulation of generation, transmission, transformation, distribution, supply and use of electric energy for cross border trade in electricity and planning of rural electrification.

The Petroleum Supply Act, 2007 envisages making provisions for importation, exportation, transportation, transformation, storage and wholesale and retail distribution of petroleum and its products in a liberalized market.MP's should stand up to be counted forthwith.
 
Huku ndio kumkoma Nyani Giladi kwenyewe, wakiendelea kwa mwendo huu basi nadhani mawaziri wataamka na kuacha ubabaishaji.
 
Kama maneno haya ni ya kweli . Nasema kama maana nilikosa tukio hili basi wapongeza wabunge wote kwa pamoja na hasa walio simamia swala . Yaani Mwakyembe pamoja kuwa mwenyekiti wa Richmond bado alipoa tu kuitaka semina iendelee ? Ama kweli Ulaji mbaya . Nakumbuka mwaka ule alishangaa kwa nini viongozi wa CUF wasishitakiwe kwa kosa la Uhaini akapewa ulaji east Afrika .
 
Lunyungu,

Mwakyembe ameshamaliza kazi yake kwenye ile ripoti , ndio maana hawataki wabunge waione. Nashindwa kuelewa ni nchi gani hii ambapo wawakilishi wa wananchi (wabunge) wananyimwa access ya ripoti muhimu . Je wanasubiri Sitta arudi ndio wapewe hiyo ripoti ? Haya ni matusi makubwa kwa bunge lakini dhahidi wananchi wa Tanzania.
 
May be these Guys(sisiem MPs) have borrowed a leaf from Dr. Slaa and Kabwe. It is just a matter of time, the truth will manifest. I hope they will become more aggressive to other "Hot" issues, which are ruining the Country or be ready to face the consequence in 2010 Election. However, I congratulate them for a positive start.
 
Ingekuwa kila mwaka wabunge wanakomaa namna hii, nadhani miswada ya ajabu ajbau isingekuwa inapita, na nadhani nchi isingekuwa hapa ilipo kiuchumi, hoi taabani.
Sijui kama ghadhabu hizi za wabunge hao ni "NGUVU ZA SODA" ama za kudumu. Najua EL atawaita katika kamati ya chama na kuwafokea wabunge hao mahiri, nawaomba tu wakaze uzi hivyo hivyo.
 
Ingekuwa kila mwaka wabunge wanakomaa namna hii, nadhani miswada ya ajabu ajbau isingekuwa inapita, na nadhani nchi isingekuwa hapa ilipo kiuchumi, hoi taabani.
Sijui kama ghadhabu hizi za wabunge hao ni "NGUVU ZA SODA" ama za kudumu. Najua EL atawaita katika kamati ya chama na kuwafokea wabunge hao mahiri, nawaomba tu wakaze uzi hivyo hivyo.

Nina omba mjue kwamba ni baada ya makelel ya JF na baadhi ya mijadala ya watu wenye usongo kwenye TV prog za hapa nyumbani na Dr.Slaa na Zitto na watu kuanza kuwazomea na kuwatukana kwa uwazi ndiyo maana wachache wameanza kuamka . Wanawasikia wananchi wanayo yasema na hata Kenya wamejionea wenyewe so nadhani they are serious kama si danganya toto . Unajua madongo ya JF wanapekewa live wengine wana watoto wao humu humu na ndugu zao . Sasa JF ndiyo macho na masikio ya watanzania . JF baada ya akina Zitto ndiyo chombe pekee tunapo anika hata kama ni speculations mwishowe huwa ni ukweli sasa wanakwama kabisa . Tuendelee kukata issue kwa nguvu hapa tuache mchezo .
 
Nina omba mjue kwamba ni baada ya makelel ya JF na baadhi ya mijadala ya watu wenye usongo kwenye TV prog za hapa nyumbani na Dr.Slaa na Zitto na watu kuanza kuwazomea na kuwatukana kwa uwazi ndiyo maana wachache wameanza kuamka . Wanawasikia wananchi wanayo yasema na hata Kenya wamejionea wenyewe so nadhani they are serious kama si danganya toto . Unajua madongo ya JF wanapekewa live wengine wana watoto wao humu humu na ndugu zao . Sasa JF ndiyo macho na masikio ya watanzania . JF baada ya akina Zitto ndiyo chombe pekee tunapo anika hata kama ni speculations mwishowe huwa ni ukweli sasa wanakwama kabisa . Tuendelee kukata issue kwa nguvu hapa tuache mchezo .

Kwi kwi kwi!
Mkuu Lunyungu, nimecheka sana! Una maana watoto wa hao vigogo a.k.a mafisadi wakiona mama na baba zao wanapewa "ukweli" kutoka hapa kijini na wao wanawawakia maskani sio? Hii imeniacha hoi sana. Naomba tukaze uzi.
 
Things fall apart! The time we have been waiting for since indepence is here on our door steps. Thanks God you have eventually heard our prayers! Huu mwaka hautaisha kabla mabadiliko makubwa na ya kimsingi hayajatokea TZ! Let's wait and see.
 
naomba wasije wakamalizia na ule msemo wao wa kawaida,"naunga mkono hoja mia kwa mia"kwani wabunge wa ccm siku zote hawana mwamana na upinzani,au maswala yanayoihusu jamii wa walalahoi
 
Hivi ndugu zangu hamjajiuliza kwanini hizo kelele na passion zinaonekana kwenye "semina" na siyo Bungeni? Nawahakikishia kama ingekuwa ni Bungeni baada ya kupiga kelele hizo wangeulizwa kuhusu kuunga hoja wangesema "pamoja na hayo Mhe. Spika naomba kuunga mkono hoja". Hawana ubavu wa kumkoma nyani giledi Bungeni!! I don't care about the seminar.... wasimame Bungeni tuwahesabu.
 
Mzee wa Standard alisema kwamba ameacha miswada mingi sana ya kujadili, sasa naona miwili imepigwa chini! Wakikosa miswada ya kujadili wataahirisha kikao mpaka Mzee wa Viwango arudi????
 
Kama kweli wamedhamirai hayo wanayosema basi wayaongelee Bungeni ambako wanawawakilisha wananchi. Ila naona ni hatua postive kidogo hiyo inawezekana tunaelekea kuzuri maana walianza na kukomalia mkataba wa Container terminal na sasa wamekuja hii. Tusubiri tuone tunaelekea wapi.
 
Tutakuwa tunajidanganya kama tukitegemea lolote kutoka kwa wabunge. Bunge letu bado ni rubber stamp, halina ubavu wowote wa kuchallenge serikali, nimesikia pia kuwa wabunge wanamuogopa sana Lowassa, kama akisema tu msizungumzie hilo jambo hawatazungumzia, kama kweli wako honest wangejadili kwenye bunge na sio kwenye semina ya bunge. Serikali ikiamua kuwahonga wabunge kwa kuongeza marupurupu basi unaweza kushangaa wanakaa kimya na wanatuuza wananchi!
Labda Zitto anaweza kutambia kama kweli wabunge wanaweza kuiwajibisha serikali!
 
Atleast wameongea baada ya JF kuwapaka kwa saana. sasa kama wako serious waulizie rep[ort ya ATC na Mahujaji, na kinachoendelea sasa ATC kununua magari mabovu, na ukodishaji wa Ndege, je wana profile ya huyo anaye wakodisha? (Sijuii ndio George Hallack or What na kwanini wasikodishe kutoka kwa Manufacturers or Reputable Airliness, ndio haya haya ya Richmond ya Ndege sasa, hata hayo magari kwanini wasinunue kwa authorised dealers kama ni Toyota wapo authorised dealers wa magari mapya na Used.
Pili wasikubali kujadili chochote Mpaka Six arudi iliwampe na yeye Changa moto ya Kujali maslahi ya Taifa, badala ya Per Diem na uchwara wa kuimaraisha bunge, wakati uchumi wa nchi unayayuka.
Na akirudi wamuhoji kwa nini hakupanga safari wakati Bunge liko likizo?
 
Kazi kweli kweli at least wamejaribu isipokuwa nina doubt kama huu msimamo utaendelea hadi bungeni tofauti na ilivyotokea kwenye semina tunataka tunataka wamkome nyani giladi mbungeni sio kwenye semina.
 
Wabunge waicharukia serikali
na Peter Nyanje, Dodoma
KWA mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, wabunge kadhaa jana walipeleka ujumbe mzito serikalini, wakiutaka mhimili huo wa utawala kuacha kulitumia Bunge kama chombo cha kupitishia ajenda binafsi kwa maslahi ya watu wachache.
Wakizungumza katika semina ya wabunge iliyokuwa ikijadili miswada ya umeme na mafuta, wabunge hao walisema wakati umefika sasa kwa Bunge kukoma kuwa taasisi inayoweza kudhalilishwa na kutumiwa isivyo.

Kwa kauli moja, wabunge hao waliikataa miswada hiyo, huku mbunge mmoja akisema kuwa anatamani kufa, ili asije akaona jinsi Watanzania wa kesho watakavyoishi kwa dhiki, huku vinu vya umeme vikimilikiwa na wawekezaji.

Maneno hayo mazito yaliandikwa na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM) na ujumbe huo ulisomwa na aliyekuwa mwenyekiti wa semina hiyo, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM).

Katika ujumbe huo, Simbachawene alisema kuwa sheria zinazopendekezwa zinalenga kuviweka vinu vyote vya kuzalisha umeme mikononi mwa wawekezaji, huku serikali ikibakia kuwa ‘house boy’ au ‘house girl’ (watumishi wa kazi za ndani) na wananchi watumwa.

Alisema kuwa serikali imeuza viwanda vyote na madini na sasa inataka kuuza vinu vya kuzalisha umeme jambo ambalo litaipeleka nchi pabaya.

“Natamani nife ili nisije nikaiona hali hiyo,” alisema Simbachawene kupitia ujumbe huo uliosomwa na Dk. Mwakyembe huku wabunge wengine wakishangilia.

Kwa upande mwingine, suala la kusitishwa kujadiliwa kwa ripoti ya kamati teule ya Bunge kuhusu kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, nalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kuwapandisha wabunge hasira, kiasi cha kukataa kujadili miswada hiyo.

Wabunge wote waliochangia katika mjadala wa semina hiyo, walisema kuwa, hawawezi kujadili sheria mpya ya umeme, kabla hawajaiona ripoti hiyo ambayo inaweza kuwa inaonyesha matatizo yaliyomo kwenye sekta hiyo.

Mwishoni mwa semina hiyo, wabunge walimkatalia Dk. Mwakyembe kumruhusu Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kusema chochote, wakitaka waziri huyo akutane na kamati hiyo Jumanne, kutoa maelezo.

Aidha, wabunge hao walimtaka Dk. Mwakyembe, ambaye ni Makamu Mwenyekliti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, kuishauri Kamati ya Uongozi ya Bunge kuiondoa miswada hiyo katika shughuli za Bunge mpaka hapo itakapojadiliwa kwa kina na wadau na pia wabunge watakaipojadili ripoti ya Richmond.

Aliyeanzisha mjadala huo alikuwa ni Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), ambaye baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali kuhusu miswada hiyo, alimtaka mwenyekiti aiahirishe semina hiyo kwa sababu miswada hiyo haipaswi kujadiliwa mpaka pale wabunge watakapoijadili ripoti ya Richmond.

Hoja hiyo ilimfanya Dk. Mwakyembe asimame na kumwambia mbunge huyo kuwa semina hiyo haikuwa na mamlaka ya kuzuia miswada hiyo kuwasilishwa bungeni.

Muda mfupi baadaye, alisimama Mbunge wa Njombe Kusini, ambaye pia ni Naibu Spika, Anne Makinda (CCM) na kusema kuwa haoni maana ya semina hiyo kwa sababu kilichowasilishwa katika mada ni tofauti na kile ambacho wabunge walitarajia kiwasilishwe.

Akifafanua, Makinda alisema kuwa mada zilizowasilishwa hazina tofauti na maelezo ambayo mawaziri huwa wanayawasilisha bungeni wakati wanapowasilisha miswada mbalimabli ya sheria.

“Mimi si mjumbe wa Kamati ya Uwekezaji, lakini ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi. Tuliposhawishiwa tukubali kuiweka semina hii tulielezwa kutakuwa na maelezo ya ziada ambayo kwa kweli nimeshangaa sijayasikia,” alisema.

Hapo, wabunge wengi walipiga kelele wakimtaka Dk. Mwakyembe aiahirishe semina hiyo, lakini alifanikiwa kuwashawishi waendelee nayo na hivyo bila kutarajia kuwapa mwanya wabunge kueleza masikitiko yao kuhusu wizara hiyo na mtindo wa serikali kulitumia Bunge kama muhuri wa kupitisha mambo yake.

Katika kauli ambayo inaweza kumfanya Waziri Karamagi na timu yake yote kujiona wamepoteza imani mbele ya wenzao bungeni, Kimaro alisema kuwa wizara hiyo imepoteza sifa ya kuzungumza na wabunge.

Alisema kuwa wizara imepoteza sifa hiyo kwa sababu mambo inayoyafanya ni tofauti na yale yanayotarajiwa na ndiyo maana kila siku bei za umeme zinapanda na wawekezaji walioletwa katika sekta ya umeme wamekuwa na matatizo, akiwataja Net Group Solution, IPTL na Songas.

“Tubadilike wabunge, si kila serikali ikileta muswada tuukubali, tunaweza kuukataa na ndivyo tutakavyofanya sasa,” alisema Kimaro na kubainisha kuwa, miswada hiyo imelenga kuwanufaisha watu wachache.

“Kupitia sheria hii, tunataka kubinafsisha Tanesco kwa mlango wa nyuma, wananchi watatucheka, wananchi watatuchinja,” alisema.

Kwa upande wake, Anne Kilango Malecela (Same Mashariki-CCM) alisema kuwa, mbunge ni mtu mwenye akili timamu na akaeleza kuwa, kwa mara ya kwanza alishangazwa na mambo yaliyofanywa na Dk. Mwakyembe.

Mbunge huyo machachari alisema kuwa, wabunge wanaweza kusamehewa wakifanya kosa mara moja na wananchi, lakini wakifanya kosa kwa mara ya pili “tutaonekana stupid. Na Mbunge hapaswi kuwa stupid.”

Ilishaelezwa awali kuwa kifedha, Tanesco ilikuwa ICU (wodi ya wagonjwa mahututi) na Kilango alihoji nani ameifikisha Tanesco ICU kwa sababu kuna uwezekano kuwa mkono wa mtu ndio umeipeleka Tanesco hapo ilipo.

“Hatujaletewa ripoti ya Richmond, tunabariki mambo mengine. Hata utuweke hapa hadi kesho, hata tukae siku nne, muswada huu hatutaujadili.

“Wewe mwenyekiti unajua ni kwa nini Tanesco ipo katika hali hii, kwa sababu ‘umedeal’ na Richmond. Sisi hatujui. Tuletee Richmond tuijadili kwanza,” alisisitiza.

Raphael Chegeni (Busega-CCM) alisema umefika wakati sasa Bunge lifanye mambo ambayo wananchi wanatarajia kutoka kwake na kuwa wakati wa kuwa ‘rubber stamp’ (muhuri) wa kupitisha mambo ya serikali umepita.

Alisema kuwa Tanesco haikufika hapo ilipo kwa bahati mbaya, kwani imefikishwa kutokana na mikataba mibovu ukijumuisha Net Group Solution ambao waliingizwa kwa nguvu.

Chegeni alisema kuwa inashangaza kuwa wakati wanatokea watu kama Dk. Idris Rashid (mkurugenzi wa Tanesco) abaye alitaka kujiuzulu baada ya kuingiliwa kwenye kazi zake, masuala hayo hayawekwi wazi.

Akimwelekea Dk. Mwakyembe, Dk. Chegeni alisema kuwa hata wakati walipozunguka na tume yake ya Richmond (Dk. Mwakyembe alikuwa mwenyekiti wa tume hiyo) wananchi waliwazomea kiasi cha kuwaeleza ‘tunataka Rais wetu (Kabwe) Zitto (Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CHADEMA) azungumze nasi.’

“Sisi kama wabunge, tumekuwa ‘reduced into a stupid organisation’. Tuweke pembeni miswada hii, tuzingatie yaliyoko mezani. Kubinafsisha ovyo ovyo tukome... ATCL ni mfano, kila kitu tulichobinafsisha kimegeuka moto. Tufanye kitu ambacho Watanzania wanakitarajia kutoka kwetu,” alisema.

Dk. Willibrod Slaa alisema kuwa yeye hana tatizo na mabadiliko yanayopendekezwa katika miswada hiyo, isipokuwa anaona vigumu kujadili mabadiliko hayo wakati wabunge hawajapatiwa mpango mkuu wa nishati (Power Masterplan) ambao wameuomba tangu miaka mitatu iliyopita.

Alisema kuwa mpango huo ndio unawapa picha ya kuweza kujadili sheria inayopendekezwa na kuanza kuijadili hivi sasa ni sawa na kujadili kitu ambacho haukifahamu.

Dk. Slaa alisema muswada wa umeme unazungumzia ubinafsishaji katika sekta hiyo, lakini akaonyesha hofu yake kuhusu maandalizi yaliyofanywa ili kuratibu na kuhimili uwekezaji katika sekta hiyo.

Akitoa mfano, alisema kuwa wajanja waliutumia mwanya wa mpango wa Import Support kuanzisha makampuni hewa, na kwa ujumla, mpango huo umeigharimu serikali zaidi ya sh trilioni moja.

“Nina taarifa za uhakika kuwa mtu mmoja pekee aliandikisha kampuni hewa 35. Ikifika wakati nitataja majina. Bunge tunatumiwa kupitisha vitu kama muhuri bila sisi wenyewe kujua tunapitisha nini,” alisema.

Hamad Rashid Mohammed (Wawi-CUF), ambaye pia ni kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kuwa, serikali inapaswa kuiondoa miswada hiyo kwa sababu wabunge wameshaonyesha wasiwasi.

Alisema kabla ya kuileta upya, ni vema wizara na wadau wakakaa kitako na kufanya tathmini kuhusu misingi, hasa inayoitaka kuwepo kwa mabadiliko yanayopendekezwa kupitia sheria hizo.

“Miswada hii inazungumzia roho ya nchi katika uchumi na usalama. Tunaweza kesho na keshokutwa tukawa na umeme ambao serikali haina mamlaka nao,” alisema.

Mbunge wa Longido, Lekule Laizer, aliishangaa serikali kuleta muswada mwingine wa umeme wakati utekelezaji wa mpango wa kupeleka umeme vijijini unasuasua licha ya kupitishwa zamani.

Lekule alisema kuwa kuna uwezekano kuwa muswada huo ni shinikizo la watu walioiba fedha Benki Kuu (BoT) ambao wamezitumia kuanzisha kampuni hizo za kuzalisha umeme.

“Sijui ni zile fedha za BoT ndizo wameunda kampuni za kuja kuzalisha umeme? Kama wanaandaa, hatupo tayari kupokea muswada huu. Mwenyekiti funga semina tukutane bungeni,” alisema.

Zaidi ya wabunge 15 walichangia hoja hiyo na wote walikataa miswada hiyo kujadiliwa bungeni mpaka hapo aidha itakapopitiwa kwa kina na pia mpaka watakapoijadili ripoti ya Richmond.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/2/4/habari2.php
 
Keep It Up Ndugu Wabunge Mkikwaluzana Mara Tatu Namna Iyo Lazima Mambo Ya Kipumbavu Yatakoma Most May Come Back To Their Senses
 
Naomba maombi mawili kwa wanaJF:

1.Nimesikia kuwa wabunge wa ccm wanakutana faraghaa kujadili mada hizi nzito Richmond na Bot wakiwa chini ya waziri mkuu, je Kuna yeyote anayeweza kufuatilia kwa karibu ni nini kinatetwa.

2.Sita anakwenda marekani kwa safari ya ghafla sana kabla ya hoja nzito kujadiliwa,napata wasiwasi isije ndio ikawa safari ya kwenda kusema na Balali basi niwaombe wanaJF wa Marekani wajitahidi ku-monitor hiyo safari ili wajue kuwa wanaJF si wakubabaisha kama wao viongozi wanavyotubabaisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom