Angola yaondoa sheria inayokataza ushoga

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Bunge la Angola laondoa sheria inayokataza mahusiano ya jinsia moja
Jan 26, 2019 02:58 UTC
Katika hali ambayo, nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa zikipinga na kukemea mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja, Bunge la Angola limeifuta sheria ambayo ilikuwa inatafsiriwa kama inapinga mahusiano ya kimapenzi kwa watu wa jinsia moja.
Serikali ya nchi hiyo tayari imekataza ubaguzi dhidi ya watu kulingana na hali zao za mahusiano; yeyote anayemnyima mtu kazi au huduma kutokana na uhusiano wao wa kimapenzi anakabiliwa na hatari ya kufungwa jela kwa kipindi cha mpaka miaka miwili.
Angola ni koloni la zamani la tatu la Ureno barani Afrika kufuta sheria zinazokataza mahusiano ya watu wa jinsia moja, Visiwa vya Sao Tome na Cape Verde.
Nchi nyingi za Afrika zina sheria kali zinazopinga na kuukataza mahusiano ya kimapenzi ya watu wa jinsia moja.
Mapenzi ya watu wa jinsia moja yaliharamishwa nchini Uganda ingawa wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi ya jinsia moja nchini humo wanasema kuwa watu walio wapenzi wa jinsia moja wanastahili kuendelea na shughuli zao ikiwa watahitaji kufanya hivyo.
Aidha nchini Kenya, kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Itakumbukwa kuwa, mwaka 2006 Afrika ya Kusini ilikuwa nchi ya kwanza Afrika na ya tano duniani kuruhusu ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Madola ya Ulaya yamekuwa yakizishinikiza nchi za Kiafrika na kutishia kuzikatia misaada endapo zitawabughudhi watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Hata hivyo nchi nyingi za Kiafrika zinapinga mahusiano hayo zikisisitiza kuwa, ni kinyume na maumbile ya mwanadamu na kwamba, yanakinzana na utamaduni wa Mwafrika.

My take:Hii ni hatua mbaya sana......misaada inaiharibu africa si ajabu kusikia wametoa ili wapewe misaada kwa wingi.........Nchi ina utajiri wa mafuta kama angola but nothing...ni malofa tu kama sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata sisi tutaitoa tu Rais etu mtarajiwa kasha sema. Kwahiyo wenye marinda yenu yanayowashawasha mjiandae, 2020 full kufumuliana Mgonjwa wa taifa akishika usukani:p:p
 
Back
Top Bottom