Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos amepata upingamizi wa kisheria kutoka kwa kundi la wanasheria wa nchini humo kufuatia uteuzi wa bintiye kuwa kiongozi wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Sonangol.
“Uteuzi huu ni kinyume cha sheria na tutaomba utenguliwe. Sheria iko upande wetu katika hili” alisema mwanasheria David Mendes.
Wanasheria hao walisema watapeleka suala hilo katika sehemu tatu tofauti. “Waraka mmoja utapelekwa kwa Mkuu wa nchi ambae ni rais mwenyewe, tutapeleka waraka mwingine kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tutafungua shauri Mahakama kuu ili kupata zuio mara moja."
Rais Jose Eduardo dos Santos alifanya uteuzi huo kupitia mamlaka yake kama rais na kutangaza siku ya Alhamisi.
Mara tu baada ya uteuzi huo, Chama kikuu cha Upinzani cha Angola National Union for the Total Independence of Angola (UNITA) kilikemea uteuzi huo kikiita kitendo hiko cha upendeleo.
Binti wa Rais, Bi. Isabel dos Santos, almaarufu kama “Princess” ni mwanamke tajiri kuliko wote barani Africa na anashikilia nafasi ya nane kwa ujumla. Utajiri wake unakadiriwa kuwa dola za kimarekani Bilioni 3.3 kwa maelezo ya jarida la Forbes.
Binti huyo wa Rais mwenye umri wa miaka 43 anamiliki shea ya 25% katika kampuni kubwa kabisa ya mawasiliano nchini humo, Unitel pamoja na benki ya BIC.