Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi utafukuliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ili apate kupewa maziko mazui, kwa mujibu wa chama chake cha Unita kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Savimbi aliuawa na vikosi vya serikali tarehe 22 Februari mwaka 2002 na kuzikwa siku iliyofuatia kwenye mkoa ulio mashariki wa Moxico.
Wiki sita baadaye Unita walisaini makubaliana ya amani na serikali na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 27.
Kiongozi wa sasa wa chama cha Unita Isaias Samakuva, alitangaza kuwa mwili wa Savimbia utafukuliwa baada ya kukutana na rais Joao Lourenco kwenye mji mkuu Luanda siku ya Jumatano.
Mapema mwezi huu aliilaumu serikali kwa kumnyima Savimbi maziko Mazuri.
Jonas Savimbi ni nani?
Jonas Savimbi alizaliwa tarehe 3 Agosti mwaka 1934 huko Munhango mkoa wa Bié, mji mdogo kwenye reli ya Benguela na kulelewa Chilesso mkoani humo.
Alikuwa kiongozi wa siasa kisa kwa siaia na jeshi mabaye laizniajsa na kuongoza chama cha cha National Union for the Total Independence of Angola (UNITA).
UNITA kwanza waliendesha vita vya msituni dhidi ya utawala wa wareno kati ya mwaka 1966 na 1974 na kisha kikapigana na chama cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA) wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi wakati wa kifo cha Savimbi kwenye mapigano na vikosi vya serikali mwaka 2002.
Utotoni mwake Savimbi alisemea shule za kiprotestanti lakini pia na kwenye shule za kikatoliki.
Akiwa na umri wa miaka 24 alipata msaada wa kwenda kusomea nchini Ureno. Huko alimaliza masomo ya sekondari.
Baadaye alikuja kuwa na uhusino na wanafunzi kutoka Angola na koloni zingine za Ureno ambao walikuwa wanajiandaa kuanzisha vita dhidi ya ukoloni na kufanya pia urafiki na chama cha kikomunisti nchini Ureno.
Alijuana na Agostino Neto ambaye wakati huo alikuwa akisomea udaktari na ambaye alikuja kuwa kuwa rais wa chama cha MPLA na rais wa kwanza wa Angola.
Chanzo: BBC Swahili