Angola, Mali zatoka 4-4 AFCON

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
LUANDA, Angola

WENYEJI wa fainali za Mataifa ya Afrika, Angola, usiku wa kuamkia leo, walishindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani baada ya kutoka sare ya mabao 4-4 na Mali.
Mechi hiyo ya ufunguzi, ilishuhudiwa Angola wakipata mabao manne ya haraka na kuwafanya Mali wachezaji wa tahadhari kubwa huku wakishambulia kutafuta mabao.

Mali ambao walizitumia vizuri dakika 11 za mwisho baada ya kuwa nyuma kwa mabao 4-0, kusawazisha mabao hayo na kuwafanya Angola wabaki midomu wazi.

Wenyeji walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kwa kichwa na Flavio, wakati Gilberto na Manucho kila mmoja alifungwa kwa mkwaju wa penelti.

Lakini, Mali wakitoka nyuma wakati Seydou Keita alipoifungia timu hiyo bao la kwanza kwa shuti la karibu.

Frederic Kanoute aliongeza bao la pili kwa kichwa dakika mbili baadaye kabla ya Keita kufunga bao la tatu na Mustapha Yatabare kumalizia bao la dakika za mwisho za mchezo huo na kuufanya mji wa Luanda kuwa kimya.

"Sare hii kwangu ni sawa na kufungwa, hii ni mara ya kwanza kwangu, sijawahi kuona tangu kuanza kwangu kufundisha mpira," alisema Manuel Jose.

"Tulistahili kushinda mechi hii, lakini tuliamka wakati muda umekwenda,” alisema kocha wa Mali, Stephen Keshi

"Mpira wa miguu Afrika unajifunza barabarani, tunavipaji, lakini maarifa ni kidogo.

Flavio aliifungia Angola bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 36 na kuongeza lingine dakika ya 42 kwa shuti kwa kuunganisha mpira wa krosi wa Mabina.

Mali walifanya makosa na kuwaruhusu Angola kufunga mabao mawili ya penalti yaliyofungwa na Gilberto na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Hull, Manucho.

Mashabiki wengi wakati wakiondoka uwanjani hapo huku wakishangilia ushindi wa mabao 4-0, lakini wachezaji wa Angola walishindwa kulinda mabao yao na kuwaruhusu Mali kusawazisha.

Kiungo anayekipa Barcelona , Keita aliifungia Mali bao la kwanza dakika 79, Kanoute anayechezea timu ya Sevilla aliiongezea bao la pili .

Keita na Yatabare walizima furaha za Angola kwa kila mmoja kufunga bao dakika za mwisho za mchezo na kumrejeshea furaha kocha wao, Stephen Keshi.
 
Angola waliliridhika na mafanikio kabla ya mwisho wake, kocha akakosea pia kufanya substituion na matokeo yake wakamwangusha Rais wao na Mke wake walokuwa wanashaingilia muda wote wa mchezo,Looh Poor Angola you are like your brother Tanzania with Taifa Starz!!
 
What a come back!! Ingekuwa fainali ingekuwa Historia kubwa sana hata hivyo jamaa wamefanya maajabu!!
 
Back
Top Bottom