Anglophone Vs Francophone Africa: Harufu ya mpasuko wa kisiasa ndani ya Umoja wa Afrika (AU)

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316

Anglophone Vs Francophone Africa: Harufu ya mpasuko mkubwa wa kisiasa ndani ya umoja wa Africa (AU) baina ya mataifa yanayozungumza lugha ya Kiingereza na yale ya Kifaransa.​


images (1).jpg

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu JamiiForums.

UTANGULIZI: MZOZO WA ANGLOPHONE - FRANCOPHONE NCHINI CAMEROON
=====
Maeneo yanayozungumza Kiingereza kwa muda mrefu kaskazini magharibi na Kusini magharibi mwa nchi ya Cameroon ina wakazi ya 20% ya idadi ya watu wote wa nchi ile.

Kura ya maoni iliyokuwa inaungwa mkono na umoja wa mataifa (UN) kufuatia uhuru wa mnamo mwaka 1960 ilishindwa kuwapa Anglophones fursa ya kuunda nchi yao huru.

images (2).jpg

Ingawa waliahidiwa kiwango fulani cha uhuru chini ya mfumo wa shirikisho, nguvu zilihamia katika mji mkuu unaotawaliwa na watu wanaozungumza Kifaransa, Yaounde, mnamo mwaka 1972.

Kumekuwa na "Tatizo la Anglophone" la kutengwa huko nchini Cameroon tangu wakati huo. Maandamano ya amani yalianza mnamo mwaka 2016, wakati ambapo serikali ililazimisha walimu na majaji wanaozungumza Kifaransa kufanya kazi katika shule na mahakama za Anglophones, na mchakato maalum wa kimfumo wa kuua sheria za utetezi wa haki za binadamu.

images (3).jpg

Vikundi vya kimataifa vya haki za binadamu visivyo na ubaguzi vinaamini kuwa serikali ilijibu kwa kutumia nguvu kubwa kuzidi kiasi.

NIGERIA: MBABE WA AFRIKA (AFRICAN POWERHOUSE) ANAYEZUNGUMZA KIINGEREZA LAKINI AMEZUNGUKWA NA NCHI ZA KIFARANSA
=====
Malengo ya kisiasa ya Nigeria katika medani za kimataifa, yanahitaji ujuzi na maarifa ya lugha ya Kifaransa kwani ndiyo lugha namba mbili rasmi ya UN, AU, n.k.

Nigeria kwa hivyo, inachukuliwa kama nchi kubwa yenye ushawishi zaidi katika siasa za Afrika haswa katika ECOWAS na AU, kwa sababu ya hili, Kifaransa kinapaswa kujulikana kwa raia wa Nigeria.

Lugha ya Kifaransa ni muhimu nchini Nigeria kwa sababu majirani zake wote ni nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa na kwa maingiliano na mawasiliano bora na nchi hizi, Nigeria na raia wake wanapaswa kusoma na kuzungumza vema Kifaransa.

Serikali ya Rais wa zamani hayati Saniabacha iliona umuhimu wa Nigeria kuzungumza Kifaransa wakati mnamo mwaka 1996, alipotamka Kifaransa kama lugha ya pili rasmi kwa Nigeria.

Kwa bahati mbaya, tamko lile limebaki kwenye makaratasi kwani sera hiyo haikutekelezwa kamwe.

SASA MPASUKO WA ANGLOPHONE - FRANCOPHONE WAVAMIA RASMI UMOJA WA AFRIKA (AU)
=======
Haijawahi kukubaliwa hadharani, lakini mgawanyiko kati ya anglophones na francophones bado wakati mwingine unaikabili Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa.

Katika picha hapo chini, rangi la blue ni nchi za "Francophone" na kijani ni zile za "Anglophone"

images.jpg

Kwa mfano kama mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi wa AU - kwa wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama - swali kuwa lililokuwa linaulizwa ni kama suala hili litajirudia tena.

Au itakuwa ni kadi ya ushindi mikononi mwa wagombeaji kutoka katika vikundi vya wanachama wanaozungumza lugha ndogo ndani ya AU? Nchi za Anglophone na francophone zinaunda theluthi mbili ya nchi wanachama wa AU. Lugha zingine rasmi za AU ni pamoja na Kireno na Kiarabu.

Mara nyingi maamuzi muhimu ndani ya taasisi hii yanaathiriwa na mienendo kati ya vikundi hivi viwili vya lugha. Ushindani mzito wa nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya AU (AUC) mnamo mwaka wa 2012 ilifufua mgawanyiko huu, ambao wengi walitarajia ungekuwa umeisha kwa wakati ule.

images (4).jpg

Ushindi wa Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika Kusini dhidi ya kiongozi aliyakuwa madarakani kwa wakati ule ndugu Jean Ping ulionekana na wengine kama ushindi kwa Afrika ya waongea Kiingereza juu ya Afrika ya francophone.

Ukweli kwamba nyadhifa kuu mbili katika taasisi - mwenyekiti na naibu mwenyekiti - zilikuwa zinashikiliwa na raia wa Afrika Kusini na Kenya zilisaidia sana kutilia mkazo mtazamo huu.

Walakini mtu anaweza kuhoji umuhimu wa mgawanyiko huu katika Afrika ya sasa. Kama taasisi mama ya AU, Shirika la Umoja wa Afrika (OAU), liliundwa haswa kupigana dhidi ya ngome za mwisho mwisho za ukoloni, inaonekana ni hali ya kushangaza kwamba mgawanyiko kati ya wanachama wake unatokana na bara kugombewa upya na wakoloni wake wa zamani.

Soma Pia:

(1) FOR GREAT THINKERS: Is Africa still a dark continent or a crucial partner in sustaining a better world?

(2) AFRIKA BARA GIZA: Were there xenophobic attacks against black foreigners or just diplomatic and political standoff between South Africa and Nigeria?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Tusisahau kuwa Ufaransa inachukiwa asilimia fulani ya pesa za kodi Kwa kila nchi aliyoitawala.

Kwa ufupi nchi za Africa za Francofone zinalipa Kodi kwa mfaransa Kwa kuwatawala.

Dunia ina mambo Wazungu kizungu zungu.
 
Mnaiharibu Nchi kwa kufikiri ni kikundi fulani tu cha Watu ndicho wenye uwezo wa kutawala Wengine.

Tangu mmetishiwa kuwekwa VIKWAZO kumekuwepo Propaganda nyingi kwenye mitandao kuhusu Nchi za Ulaya

Kuwanyima Watanzania haki yao ya kuamua ni dhambi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM.

Wapeni Uhuru na haki Wananchi waamue wanachokitaka, wanachokipenda, huo ndio Uzalendo.

Ukiongelea kuhusu Francofone na Anglofone Sisi haituhusu hayo Matatizo ameshayamaliza NYERERE alipotangaza kuwa Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote

Msiturudishe nyuma.
 
Tusisahau kuwa Ufaransa inachukiwa asilimia fulani ya pesa za kodi Kwa kila Nchi aliyoitawala..

Kwa ufupi nchi za Africa za Francofone zilipa Kodi kwa mfaransa Kwa kuwatawala..

Dunia ina mambo Wazungu kizungu zungu..
Aisee 😂 😂
 
Tusisahau kuwa Ufaransa inachukiwa asilimia fulani ya pesa za kodi Kwa kila Nchi aliyoitawala..

Kwa ufupi nchi za Africa za Francofone zilipa Kodi kwa mfaransa Kwa kuwatawala..

Dunia ina mambo Wazungu kizungu zungu..
Acha masihara mkuu, Mfaransa analipwa kwa kuwatawala wa Africa miaka hyoo.
 
Mnaiharibu Nchi kwa kufikiri ni kikundi fulani tu cha Watu ndicho wenye uwezo wa kutawala Wengine..

Tangu mmetishiwa kuwekwa VIKWAZO kumekuwepo Propaganda nyingi kwenye mitandao kuhusu Nchi za Ulaya

Kuwanyima Watanzania haki yao ya kuamua ni dhambi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM..

Wapeni Uhuru na haki Wananchi waamue wanachokitaka,wanachokipenda,huo ndio Uzalendo ..

Ukiongelea kuhusu Francofone na Anglofone Sisi haituhusu hayo Matatizo ameshayamaliza NYERERE alipotangaza kuwa Tanzania ni nchi osiyofungamana na upande wowote..

Msiturudishe nyuma..
Wewe nae unaropoka tuu, nenda kwenye majukwaa yenu ya Lissu na Magufuli huko
 
Wew nae unaropoka tuu, nenda kweny majukwaa yenu ya lissu na magufuli huko
Uhuru, Umoja, Haki kwa wote ndio misingi ya utawala Bora, ndio misingi ya maendeleo katika nchi

Mawazo ya Wengi ni mtaji kwa Taifa..

Bahati nzuri najitambua, mimi sio mpenzi wala mwanachama wa Chama chochote cha Siasa

Mimi ni Mtanzania

Nchi za Afrika chini ya jangwa la Sahara, hakuna Siasa Kuna kuoneana

Waafrika Sheria wanazitunga Wenyewe wazipinga Wenyewe

Wanauwana kwa sheria waliozitunga Wenyewe
 
Wonders shall never end in Africa...
Ufaransa inaitegemea Chad kinishati, Bila Chad Ufaransa haina Umeme, Bila Umeme Nchi haiwezi kwenda..

Utafikiria haya ninayokwambia ni uongo lakini hizo habari nimezipata kwa mshika fedha wa Balozi fulani katika kitengo cha Misaada kwa Nchi za Afrika..

Afrika tunaiendesha Ulaya kwa Mambo mengi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom