Anglophone Vs Francophone Africa: Harufu ya mpasuko wa kisiasa ndani ya Umoja wa Afrika (AU)

Mkuu,mimi ni mwafrika,haina haja ya mtu kueleza vipi wafrika weusi tulivyo,..

Ukweli uko wazi,...
Ukweli uko wazi, lakini pia ukweli si jambo rahisi kwa kila MTU kuufikia. Japo uko wazi ni kwa wawachache sana!
Nilishasema awali, Dunia imetamalaki VIINI MACHO kila kona. Usipojua hili hutaacha kujiona dhaifu sana, na yote hayo ni HESABU za watu.

Kila la heri.
 
Ukweli uko wazi, lakini pia ukweli si jambo rahisi kwa kila MTU kuufikia. Japo uko wazi ni kwa wawachache sana!
Nilishasema awali, Dunia imetamalaki VIINI MACHO kila kona. Usipojua hili hutaacha kujiona dhaifu sana, na yote hayo ni HESABU za watu.

Kila la heri.
Well written
 
Mimi nawaza tu ada ya mwanangu haijatimia. Inabidi aondoke na 1m muhula wa kwanza. Huyo ni form 2. Yule wa chuo nadaiwa 1.1m semister hii. Sijapunguza hata kidogo. Kulwa na doto wanahitaji 1.2m kule VETA.

Halafu watu Wana nafasi ya kujadili anglophone and francophone. Heri yenu.
Kama wewe hauna nafasi ya kujadili anglophone and francophone, usitupangie maisha. Kwani unatulipa pesa sisi tukiandika humu JF?
 
Shida ni kwamba hujataka kutafakari kujua Kusudio hasa la yule anayekuita wewe sub-human being, Ukapokea tu ukazibeba kama zilivyo na kuanza kuzieneza kwa wengine. Umenasa kwenye mitego yao, na wamekufanya ujisikie fahari na ukuu kujitusi.
Tena ni kujitusi kwa maneno mazito sana mkuu...
 
Shida ni kwamba hujataka kutafakari kujua Kusudio hasa la yule anayekuita wewe sub-human being, Ukapokea tu ukazibeba kama zilivyo na kuanza kuzieneza kwa wengine. Umenasa kwenye mitego yao, na wamekufanya ujisikie fahari na ukuu kujitusi.

Mwisho wa siku wewe ndio unayejiita majina mabaya, si wao tena.

Lubega haikuwa hoja ndio, hoja ni Mindset ya Unyonge na Uduni uliyonayo dhidi ya ngozi nyeusi. Nimesemea kukwepa kwako majukumu kwa kujiona si kamilifu, na kutaka kwako kuenenda vile wengine wafanyavyo.
Tabia ya kuenenda vile wengine wafanyavyo pasipo kuwa na fikra sahihi si jambo jema hata kidogo mkuu.
 
Sikubaliani nayo,lakini sina la kufanya,kwasababu tutaendelea kuitwa tu hayo majina kutokana na upumbavu na ujinga wetu..
Usijiite mpumbavu wala mjinga kwa maana kwa kufanya hivyo ndio unakuwa unampa adui fursa ya kukushambulia psychologically
 
Usijiite mpumbavu wala mjinga kwa maana kwa kufanya hivyo ndio unakuwa unampa adui fursa ya kukushambulia psychologically
Acha adui ashambulie mkuu,haiwezekani kuwa Afrika ndio continent tajiri kwa rasilimali lakini ndio continent lenye watu masikini dunia nzima
 

Anglophone Vs Francophone Africa: Harufu ya mpasuko mkubwa wa kisiasa ndani ya umoja wa Africa (AU) baina ya mataifa yanayozungumza lugha ya Kiingereza na yale ya Kifaransa.​



Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu JamiiForums.

UTANGULIZI: MZOZO WA ANGLOPHONE - FRANCOPHONE NCHINI CAMEROON
=====
Maeneo yanayozungumza Kiingereza kwa muda mrefu kaskazini magharibi na Kusini magharibi mwa nchi ya Cameroon ina wakazi ya 20% ya idadi ya watu wote wa nchi ile.

Kura ya maoni iliyokuwa inaungwa mkono na umoja wa mataifa (UN) kufuatia uhuru wa mnamo mwaka 1960 ilishindwa kuwapa Anglophones fursa ya kuunda nchi yao huru.


Ingawa waliahidiwa kiwango fulani cha uhuru chini ya mfumo wa shirikisho, nguvu zilihamia katika mji mkuu unaotawaliwa na watu wanaozungumza Kifaransa, Yaounde, mnamo mwaka 1972.

Kumekuwa na "Tatizo la Anglophone" la kutengwa huko nchini Cameroon tangu wakati huo. Maandamano ya amani yalianza mnamo mwaka 2016, wakati ambapo serikali ililazimisha walimu na majaji wanaozungumza Kifaransa kufanya kazi katika shule na mahakama za Anglophones, na mchakato maalum wa kimfumo wa kuua sheria za utetezi wa haki za binadamu.


Vikundi vya kimataifa vya haki za binadamu visivyo na ubaguzi vinaamini kuwa serikali ilijibu kwa kutumia nguvu kubwa kuzidi kiasi.

NIGERIA: MBABE WA AFRIKA (AFRICAN POWERHOUSE) ANAYEZUNGUMZA KIINGEREZA LAKINI AMEZUNGUKWA NA NCHI ZA KIFARANSA
=====
Malengo ya kisiasa ya Nigeria katika medani za kimataifa, yanahitaji ujuzi na maarifa ya lugha ya Kifaransa kwani ndiyo lugha namba mbili rasmi ya UN, AU, n.k.

Nigeria kwa hivyo, inachukuliwa kama nchi kubwa yenye ushawishi zaidi katika siasa za Afrika haswa katika ECOWAS na AU, kwa sababu ya hili, Kifaransa kinapaswa kujulikana kwa raia wa Nigeria.

Lugha ya Kifaransa ni muhimu nchini Nigeria kwa sababu majirani zake wote ni nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa na kwa maingiliano na mawasiliano bora na nchi hizi, Nigeria na raia wake wanapaswa kusoma na kuzungumza vema Kifaransa.

Serikali ya Rais wa zamani hayati Saniabacha iliona umuhimu wa Nigeria kuzungumza Kifaransa wakati mnamo mwaka 1996, alipotamka Kifaransa kama lugha ya pili rasmi kwa Nigeria.

Kwa bahati mbaya, tamko lile limebaki kwenye makaratasi kwani sera hiyo haikutekelezwa kamwe.

SASA MPASUKO WA ANGLOPHONE - FRANCOPHONE WAVAMIA RASMI UMOJA WA AFRIKA (AU)
=======
Haijawahi kukubaliwa hadharani, lakini mgawanyiko kati ya anglophones na francophones bado wakati mwingine unaikabili Umoja wa Afrika (AU) huko Addis Ababa.

Katika picha hapo chini, rangi la blue ni nchi za "Francophone" na kijani ni zile za "Anglophone"


Kwa mfano kama mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi wa AU - kwa wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama - swali kuwa lililokuwa linaulizwa ni kama suala hili litajirudia tena.

Au itakuwa ni kadi ya ushindi mikononi mwa wagombeaji kutoka katika vikundi vya wanachama wanaozungumza lugha ndogo ndani ya AU? Nchi za Anglophone na francophone zinaunda theluthi mbili ya nchi wanachama wa AU. Lugha zingine rasmi za AU ni pamoja na Kireno na Kiarabu.

Mara nyingi maamuzi muhimu ndani ya taasisi hii yanaathiriwa na mienendo kati ya vikundi hivi viwili vya lugha. Ushindani mzito wa nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya AU (AUC) mnamo mwaka wa 2012 ilifufua mgawanyiko huu, ambao wengi walitarajia ungekuwa umeisha kwa wakati ule.


Ushindi wa Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika Kusini dhidi ya kiongozi aliyakuwa madarakani kwa wakati ule ndugu Jean Ping ulionekana na wengine kama ushindi kwa Afrika ya waongea Kiingereza juu ya Afrika ya francophone.

Ukweli kwamba nyadhifa kuu mbili katika taasisi - mwenyekiti na naibu mwenyekiti - zilikuwa zinashikiliwa na raia wa Afrika Kusini na Kenya zilisaidia sana kutilia mkazo mtazamo huu.

Walakini mtu anaweza kuhoji umuhimu wa mgawanyiko huu katika Afrika ya sasa. Kama taasisi mama ya AU, Shirika la Umoja wa Afrika (OAU), liliundwa haswa kupigana dhidi ya ngome za mwisho mwisho za ukoloni, inaonekana ni hali ya kushangaza kwamba mgawanyiko kati ya wanachama wake unatokana na bara kugombewa upya na wakoloni wake wa zamani.

Soma Pia:

(1) FOR GREAT THINKERS: Is Africa still a dark continent or a crucial partner in sustaining a better world?

(2) AFRIKA BARA GIZA: Were there xenophobic attacks against black foreigners or just diplomatic and political standoff between South Africa and Nigeria?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Francophones wanamshikamano sana, ile 2012 JK alifanya umafia sana, haswa kupata kura za nchi za kusini MWA afrika, na nchi kama haswa Congo, Rwanda, Burundi, Mozambique na Angola.
Nchi za Anglophone hazina mshikamano imara na hiyo inatokana na kuwa nyingi ya hizo nchi marais wake wanafanya chaguzi na kubadilishana madaraka tofauti na nchi kama Cameroon, Congo Brazzaville, Chad nk
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom