Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu mwandishi wa habari, Angellah Kiwia na dereva Mohamed Rushaka, kulipa faini ya Sh. 800,000 au kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kukiri na kutiwa hatiani kwa kosa kujipatia pesa kwa njia ya vitisho.
Kadhalika washtakiwa hao wameamriwa kulipa fidia ya Sh. milioni 30 baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchibi (DPP) ya kukiri makosa dhidi yao.
Washtakiwa Kiwia na Rushaka wamefanikiwa kulipa fedha hizo na wameachiwa huru na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu.
Awali, mahakama hiyo iliwafutia hati ya mashtaka na kuwasomea hati mpya yenye mashtaka matatu.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya, aliiomba mahakama kufanyia mabadiliko hati ya mashtaka na katika makubaliano yaliyofanywa baina ya washtakiwa na DPP amewafutia mashtaka ya awali yenye makosa manne na kusoma hati mpya yenye kosa moja la kujipatia fedha kwa njia ya vitisho.
Wakili Komanya aliiomba mahakama kutoa adhabu kulingana na makubaliano yaliyoingiwa kati ya DPP na washtakiwa hao.
Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kati ya Machi Mosi na Machi 31, 2020 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia faida.
Katika shtaka la pili walidaiwa kutenda kosa la utekaji nyara kati ya Machi Mosi na Machi 31, 2020 katika Jiji la Dar es Salaam na kumteka Seleman Mohamed wakiwa na lengo la kumpeleka katika hatari ya kumuumiza.
Pia ilidaiwa katika shtaka la tatu wakiwa na lengo la kulipwa, walidai kiasi cha Sh. milioni 30 kutoka kwa Seleman Mohamed, huku wakimtishia kumuua.
Katika shtaka la nne la kutakatisha fedha, ilidaiwa kuwa washtakiwa hao katika tarehe zilizotajwa awali jijini Dar es Salaam, walijipatia Sh. milioni 30 kutoka kwa Mohamed, huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa tangulizi ya uhalifu.
NIPASHE