Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,479
- 119,307
Nauliza tu.
Na nauliza kwa nia njema kabisa.
Hivi rais angekuwa Lowassa, kupitia chama chochote kile, iwe CCM au CHADEMA, mnadhani angekuwa hata na uthubutu wa kuyafanya kama haya anayoyafanya rais Magufuli, kwa mintarafu ya hizi taarifa za tume ya kuchunguza mchanga wa madini?
Nani humu anayeamini kwa moyo wote kabisa kwamba Lowassa angeweza kuyafunua mambo ambayo kwa kweli yanaiweka CCM pabaya?
Nani humu anayedhani kuwa huyo poster boy wa ufisadi Tanzania angekuwa na uhalali wa mamlaka ya kimaadili kufanya kama anavyofanya sasa rais Magufuli?
Najua wengi wenu humu mnampinga Magufuli.
Pamoja na mapungufu yake, mimi naamini historia itakuja kumhukumu katika mwanga ulio chanya kwa kuwa rais mzalendo na mwenye uchungu na Tanzania.
Kama Kikwete watu mshaanza kumkumbuka basi sina kabisa shaka lolote lile kuwa hata Magufuli naye atakumbukwa vizuri tu.
Haya sasa kazi kwenu nyie wafia vyama na ukabila. Rusheni kejeli na tuhuma zenu kuwa mimi ni CCM na mkabila.