Angekuwa anawependa kweli, angewaachia katiba muitakayo

dustless

JF-Expert Member
Oct 21, 2016
796
710
Siasa ndo maisha ya kila siku hususani kwa nchi za dunia ya tatu. Siasa zinaamua watu walale milango wazi ama watengeneze mageti ya vyuma na mbwa wakali.

Vile vile zinapelekea watu wale wasaze na wawekeze ama wachumie tumbo. Na ukwel ni kwamba injini ya siasa bora ni katiba bora ingawa pia inatengemea na dereva chombo chenyewe.

Ninachojaribu kufikiri ni kwamba mpaka tumefika hapa wamepita wanne, na kila mmoja kazitumia ngwe zote mbili kikamilifu, hakuna hata mmoja aliyepunjwa muda wake.

Dosari za katiba zilibainika mapema kabisa tangu dereva wa kwanza alipokuwa kwenye usukani, na uzuri hata yeye mwenyewe alikiri kwa kinywa chake. Lakini cha ajabu alishuka na kukabidhi usukani kwa mwingine bila hata kumwaga oil.

Mwingine akafuata na mwingine pia akapita mule mule , kilometa zikazidi kuvuka kiwango kinachotakiwa na harufu ya kuungua gari ikaanza kusikika.

Alipokuja wa nne, abiria wakaanza kupiga kelele tunakufaa, gari inaungua. Alichokifanya dereva alishuka akapima oil na akacheki injini kweli imechemka mbaya.

Akaanza mikakati ya kushusha injini na kuweka mpya, abiria wakatofautiana kauli, kila mmoja kaja na lake.

Kilichofanyika hapa, oil ilibadilishwa na safari ikasonga kwa injini ile ile ya zamani.

Dereva alipofika kituo cha kubadilishana, kampa mwingine, kama kawaida naye akashika usukani.

Kutazama pembeni, akaona alama ya barabarani imemruhusu kutembea zaidi ya hamsini. Bila hiana naye kakanyaga moto na safari inaendelea.

Je ni nani hasa wa kunyooshewa kidole?
 
Jk alichomoa kipengele cha Serikal 3 tu lakin Mengine Mengi aliyaacha Kama Yalivyo lakin kwa Unyumbu wao wakafuata ushauri wa Prof Lipumba wakasusia Mchakato lakin Jk akiwa anakabiliwa na Upinzani ndan ya Chama chake alivumilia na akaahidi tupige kura ya Maoni ili Kazi iwe imekwisha lakin tukalishana Ujinga kukataa na haya ndo Matokeo. Fursa ya Mbowe kuandika Historia kaipoteza
 
Mkuu Pohamba, japo umetumia maneno makali kujenga hoja yako lkn kuna madini katikati ya maandishi yako.

kama wapinzani wangejua, wangekubaliana na katiba pendekezwa ya jk ambayo ilikuwa na mambo mengi ya msingi japo siyo yote.

lkn walau taifa lingekuwa limejaribu kumbadili mbwa kuwa mbuzi kasoro mkia. halafu baada ya muda tungeuondoa mkia.
 
Mkuu Pohamba, japo umetumia maneno makali kujenga hoja yako lkn kuna madini katikati ya maandishi yako.

kama wapinzani wangejua, wangekubaliana na katiba pendekezwa ya jk ambayo ilikuwa na mambo mengi ya msingi japo siyo yote.

lkn walau taifa lingekuwa limejaribu kumbadili mbwa kuwa mbuzi kasoro mkia. halafu baada ya muda tungeuondoa mkia.
We unakuja kwenye point.
 
Back
Top Bottom