#COVID19 Angekubali Chanjo na kuchukua tahadhari mapema, mpaka leo huenda tungekuwa naye

Tupate funzo kupitia hili, Sio kwamba unapokua mkubwa kifedha/kimadaraka ni unaona kila mtu unamzidi akili, hapana Mungu alituumba akatupa akili akatubariki akatufanya tuishi kwa kutegemeana ili kutatua mambo mbali mbali ya duniani.

Mungu akawabariki wataalamu mbalimbali, watabibu, waalimu, wahasibu, wanajeshi, wanasayansi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wanamichezo nk.

Hawa wote tunaishi kwa kutegemeana ili maisha yasonge, mimi muhasibu nikiugua nitaenda kwa mtabibu, mwanajeshi akitaka kula ataenda kwa mkulima, mwanasiasa akitaka haki ataenda kwa wanasheria wamsaidie, mwalimu akipata tatizo la kiusalama ataenda polisi, polisi akitaka elimu atarudi kwa mwalimu, hivyohivyo kwa wote.

Inapotokea wewe umewadharau wenzio na kuona unaakili kuliko wote ndugu yangu unajidanganya.

Matabibu wamekwambia ukiwa na ugonjwa sugu tafadhari zingatia miongozo kwa usahihi maana upo kwenye risk kubwa, wewe kwa kiburi chako ukaona unacheo kikubwa na kuwadharau wengine ukijiona umewazidi akili matokeo yake utayaona.

Wewe mmoja huwezi kuwa mkemia, ukawa mtabibu, ukawa mwalimu, ukawa mchungaji, ukawa mfamasia, ukawa mwanasaikolojia tafadhali heshimu kada za wengine.

Ndugu yangu kufa kupo lakini na kufa kijinga kupo,
bibilia inasema usiwe mjinga kupita kiasi ukafa kabla ya siku zako

Mhubiri 7:17
Usiwe mwovu kupita kiasi;
Wala usiwe mpumbavu;
Kwani ufe kabla ya wakati wako?


Kwa maana hiyo ni kwamba sio kila mtu anaekufa basi ni wakati wake, wengine hufa kabla ya wakati kwa upumbavu.

Pengine ungeheshimu taaluma za watu ukachukua tahadhari mpaka leo tungekua pamoja tukiijenga Tanzania Mama,

Dharau na kibuli havijawai kumuacha mtu salama tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu

View attachment 1924317

CHANJO ZIMELETWA 1M, na mpaka leo kwa miezi miwili wamechanja laki nne tu

SIDHANI KAMA KARATA HII NI SAHIHI KWA CHADEMA KWA SASA.......................................WATU WAMEKUFA, NA WANAKUFA KWA MAGONJWA MBALIMBALI


COVID, hata leo hii, JPM style ndio inatumika na itatumika dunia nzima
 
Kuna wajinga wanaamini baada ya Covid ni hakuna magonjwa mengine yanayoua. Hata mleta mada ni mjinga mmoja wapo. Kingine Watanzania hawatishiki na huu ugonjwa, ndo maana hata dozi za chanjo mpaka sasa zimekosa watumiaji. Haiwezekani dozi milioni kwa idadi ya Watanzania zinakosa wadau wa kuzimaliza haraka.
 
Kuna msemo usemwao, "lisemwalo lipo kama halipo linakuja", hili jambo liliwahi kusemwa humu na kweli likaja kutokea just coincidentaly just by coïncidence kama mwaka 2014 mimi niliposema ... Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na kweli ikaja kutokea kweli.

Ukweli ni "liandikwalo ndilo liwalo". Maisha yote ya binadamu au mwanadamu, yanapangwa na Mungu na unakuwa umeandikiwa kila kitu ile siku unazaliwa. Hivyo mapito yako yote yanakuwa yaliisha pangwa hadi utakuwa nani, utakufa lini na utakufaje, ni Mungu tuu ndiye anayejua.

Malaika mtoa roho, Iziraeli, humpitia kila mwanadamu mara Saba mara sabini daily ili ukifika muda wako, asipitishe hata nukta moja ya sekunde.
Hivyo kila mtu atakufa muda ule na kifo kile alichoandikiwa. Na ikitokea siku yako na saa yako haijafika, hata utendewe vipi, haufi, mfano mzuri ni tukio la shambulio la Tundu Lissu, kikawaida risasi moja tuu inatosha kuitoa roho ya binadamu, Tundu Lissu amepigwa risasi 16, ili auwawe, na kweli zote zimempata lakini hakufa, Jee unajua sababu ni kwanini hakufa?. Sababu ni moja tuu, saa yake ilikuwa haijafika.

Uhai ni kazi ya Mungu na kifo ni kazi ya Mungu, kila mtu atakufa siku ile, saa ile na kifo kile alichoandikiwa. Hii hoja yako kuwa angekubali chanjo na kuchukua hatua, angekuwepo, sio hoja ya kweli, hata kama angekubali chanjo na kuchukua hatua zote, kama saa yako uliyoandikiwa imefika, ni saa imefika, na unakwenda.

P
Tupe reference Basi ya uliyoyaandika
Mleta uzi ka refer muhubiri 7:17
 
hapo ndio huwa nashangaa exposure za wabunge wetu hawa mbn ht facebook unakutana na explanations nyingi tu kuhusu chanjo na barakoa, kukataa hii chanjo sio issue ila sababu ya kukataa ndio issue coz mwngine ana sababu ambazo ht wataalamu wanazikiri ila mwingine ni kwasababu ya ujinga wake tu kuhusu maswala ya jinsi gani chanjo infnya kazi
Nakubaliana na wewe mkuu.

Hoja ujibiwa kwa hoja sio viroja,serikali inakwepa kujibu
 
Hakuna tofauti yeyote! Ni porojo tu!

Wewe kama unaiona hiyo tofauti nioneshe!
Tofauti ipo. JPM aliamini katika task force, aliamini pia katika njia tofauti na zinazotumika sasa za kupigana na covid.
 
Njia za sasa ni zipi zilizoleta tija?
Nimeongelea uwepo wa utofauti wa kimaamuzi sijazungumzia tija, Uwepo wa tija au la ni suala la namna unavyopambanua mambo na kiwango cha umuhimu maamuzi unavyokipima.
 
mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, binafsi sizipendi kabisa serikali za ma CCM, lakini huyu bibi 'kiroboto' kwenye hili la kupambana na Covid kwa sehem kubwa ametimiza kile alicho paswa kukitimiza tena kwa muda mfupi tuu aliokalia kiti…….
Kipi alichofanya? Kuleta chanjo?

Niambie amefanya nini cha tofauti kupambana na corona ukiacha hiyo michanjo
 
Nimeongelea uwepo wa utofauti wa kimaamuzi sijazungumzia tija, Uwepo wa tija au la ni suala la namna unavyopambanua mambo na kiwango cha umuhimu maamuzi unavyokipima.
Maamuzi yapi aliyofanya ambayo wewe umeyaona ni ya tofauti? Hebu yataje hapa
 
Maamuzi yapi aliyofanya ambayo wewe umeyaona ni ya tofauti? Hebu yataje hapa
Fuatilia hotuba za viongozi wako crimea,

Maamuzi ya kuchukua mapapai, kuyapa majina ya binadamu na kuyapima corona na kuhitimisha kuwa wananchi waondoe hofu ya corona maana hata mapapai yana corona, kama chanjo ya corona zingekuwa na ufanisi basi kungekuwa na chanjo za kansa, malaria n.k, hizo ni baadhi ya kauli zake ila kwa usahihi zaidi wa alichokuwa akihubiri fuatilia hotuba zake.
samia yeye kaja na maamuzi ya kuchanja mwenyewe na kuhimiza watu wachanje.
 
Fuatilia hotuba za viongozi wako crimea,

Maamuzi ya kuchukua mapapai, kuyapa majina ya binadamu na kuyapima corona na kuhitimisha kuwa wananchi waondoe hofu ya corona maana hata mapapai yana corona, kama chanjo ya corona zingekuwa na ufanisi basi kungekuwa na chanjo za kansa, malaria n.k, hizo ni baadhi ya kauli zake ila kwa usahihi zaidi wa alichokuwa akihubiri fuatilia hotuba zake.
samia yeye kaja na maamuzi ya kuchanja mwenyewe na kuhimiza watu wachanje.
Ok.. Hayo yalikuwa ha Magu na kwa mujibu wenu yalishababisha mkafa sana!
.
Haya niambie maamuzi ya awamu hii ni yapi yaliyosababisha msife sana?
 
Ok.. Hayo yalikuwa ha Magu na kwa mujibu wenu yalishababisha mkafa sana!
.
Haya niambie maamuzi ya awamu hii ni yapi yaliyosababisha msife sana?
Nimeshakueleza, naongelea utofauti wa maamuzi ya viongozi hawa wawili.

Matokeo ya maamuzi waliyochukua, madhara au mafanikio mm sijayaongelea, hilo ni suala lako wewe na upeo wako wa kupambanua mambo.
 
Mbona mnakwepa kumjibu GWAJIMA? Ukichanjwa barakoa ya nini?
Majibu yameshatolewa ,ni wewe na na huyo ndugu yako ndio hamuelewi.
Ng'ombe anapelekwa kwenye maji,, kunywa au kutokunywa ni uchaguzi wale.
 
Nimeshakueleza, naongelea utofauti wa maamuzi ya viongozi hawa wawili.

Matokeo ya maamuzi waliyochukua, madhara au mafanikio mm sijayaongelea, hilo ni suala lako wewe na upeo wako wa kupambanua mambo.
Hata mimi naongelea hayo maamuzi yao hasa ni yapi si uyataje?
 
Hata mimi naongelea hayo maamuzi yao hasa ni yapi si uyataje?
Umerudi mwanzo.

Maamuzi JPM: Kupima mapapai na kuyakuta na corona, kutangaza corona hakuna, kusisitiza umuhimu wa tiba mbadala n.k

Maamuzi samia: Kuchanja, kusisitiza watu wachanje.

Upimaji wa madhara na faida za maamuzi ya viongozi hawa wawili ni juu yako na uwezo wako wa upambanuaji mambo.
 
“tumeombea tanzania na corona hakuna”

hili neno mpaka leo ndio niliichukia ccm
 
Back
Top Bottom