Ang'atwa korodani aking'ang'ania penzi

nickname

JF-Expert Member
Dec 20, 2009
544
250
Monday, 06 December 2010 08:41

Steven William, Muheza
MWANAUME mmoja ambaye ni mkulima, Selemani Abdallah miaka 47 amejeruhiwa sehemu zake za siri baada ya kung'atwa korodani na mke wake.

Tukio hilo, lilitokea juzi katika Kijiji cha Mindu Kata ya Mkuzi wilayani Muheza ambako anaishi na mke wake aliyefahamika kwa jina moja la Maria.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tanga, Jafari Mohamedi alisema mkulima huyo aling'atwa na mke wake usiku wakati na kwamba walikuwa wakigombana masuala ya mapenzi.

Mohamedi alisema chanzo kikubwa cha ugomvi huo, kimetokana na mwanaume huyo kudai mapenzi kwa mke wake usiku wakati amelewa.

Alisema mke wake alimnyima mapenzi akidai amechoka hawezi kufanya kitendo hicho na mume, lakini mume wake aliendelea kumlazimisha.


Mohamedi aliongeza kuwa mkulima huyo alimshika kwa nguvu mke wake ili ampe penzi, lakini walivutana na mke alipata nafasi na kumng'ata korodani mume wake na kulipasua moja.

Kutokana na hali hiyo mwanaume alipiga kelele ndipo watu walijitokeza na kumpeleka polisi Muheza mjini na kupewa PF3 na kupelekwa hospitali ya Teule kulazwa kwa ajili ya matibabu.

Baada ya taarifa hiyo, polisi walimkamata mwanamke huyo na kumfikisha katika kituo cha polisi kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo : Mwananchi
 

pierre

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
211
0
Mmh,jamaa anaaibisha.Mambo ya kung'ang'ania ni ya kizamani.Kwa nini asitumie busara zaidi na kubembeleza???Mwanamke tena mke wako ukimbembeleza atakubali tu.Ona sasa hukupewa ulichong'ang'ania na utauguza maumivu kwa muda mrefu na sina uhakika kama utakuwa tena fit.Imekula kwako Bw. Mohamedi,ungevumilia kidogo au ungefukuzia kwa muuza pombe aliyekuuzia ukatuliza leo ungekuwa fit na ndoa yako ingekuwa salama.

Pole sana kwa yaliyokukuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom