Angalizo wenye magari Coco Beach | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo wenye magari Coco Beach

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sikiolakufa, May 31, 2011.

 1. s

  sikiolakufa JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Napenda kuchukua fursa hii kutoa angalizo wa wananchi wanaoenda ufukwe wa coco beach kwa mapumziko. kuna kundi la askari wa jeshi la polisi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya kiharifu na unyanyasaji kwa wananchi wanaoenda kupunga upepo pale. Taarifa zinasema kwamba mara kwa mara raia wema wamekuwa wakivamiwa na askari hao na kutolewa nje ya magari yao wakituhumiwa kufanya mapenzi ndani ya gari. Askari hao wamekuwa wakiondoka na watu wanaowatuhumu kufanya mapenzi na kuwatishia kwamba watawapeleka mahakamani kama hawatatoa kitu kidogo( rushwa). Watu wengi niliobahatika kuongea nao ni wahanga wa kadhia hii. Askari hao huwa wanashirikiana na vijana wenye pikipiki ambao huvizia wananchi hao na kuwapora pesa. Je hivi kuwa ndani ya gari ni kosa? mimi ninavyofahamu kisheria kuna kosa linaloitwa indecent exposure lakini kama mtu uko faraghani na mwezio hilo ni kosa? Je hao askari polisi ambao hutembea na gari aina ya starlet....ina rangi damu ya mzee na nyeusi kwa nini wanafanya unyanyasaji huo? kwa nini wanaacha kukamata majizi makubwa kama EL na RA na wananyanyasa wananchi maskini? Kova kazi itakushinda sasa
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,426
  Likes Received: 22,345
  Trophy Points: 280
  unyanyasaji huu utakoma lini?
   
 3. p

  pointers JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  polisi hawa wamekuwa na njaa sana.........
   
 4. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Juzi kuna dada aliuliwa palepale coco beach.hawa mapimbi badala ya kufanya patrol wao wanahangaika kutafuta rushwa,....
   
 5. s

  sawabho JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika kama Starlet ni gari ya polisi kwa maana ya kwamba Serikali hainunui gari za namna hiyo, ina maana hiyo ni gari yao binafsi. Sasa inakuwaje wanatumia gari binafsi kutekeleza majukumu ya Serikali, nani anawalipa mafuta wanayotumia? Ndio hiyo rushwa ili uachiwe baada ya kukutwa umefanya ubunifu wa kubadilisha mazingira ya kuongea na wako mpendwa. Kama wanachukua rushwa, nao ni wahalifu. Piga mawe hiyo starlet.
   
 6. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Hiyo kitu ni kweli kabisa wanaJF msiipuzie kuna askari wanabuni miradi na kuwanynyasa wananchi. Coco beach pale ni public beach lakini watu tutapaogopa sasa
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,594
  Likes Received: 5,775
  Trophy Points: 280
  Jamani tusiwaseme sana hawa watu pengine sie ndie tumwakaribisha
  ni kweli huuu uchafu wa uzinzi upo..binafsi nilishaangalia kwa macho yangu gari la pemben yangu tena wanawakamata wanafunzi na si wenye akili zao...ukienda pale na gfriend wako umekaa kwenye gari tu awawezi kukusumbua kirahsi unless
  wanamtaka demu wako...ila ukweli watanzania uchafu huu upo na labda nikufichue mpaka walioleta hao polis=i kuna kigogo wa mtoto wa polisi aliliwa kule beach na picha zikasambazwa ..mzazi kilimuuma sana sana akaamua kudeal na hao wanaojiita vidume vya mbegu ....nafikiri wacha waendelee sema kama una ushahdi uko na mkeo ama rafki yako wanakuaj tu gafla hapo kazi ipo.....
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Chukulia amemkamata, ampeleke wapi?
  think and jibu.
   
 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Nina mashaka na u-polisi wao, huenda siyo polisi hawa bali ni vibaka. One of my friends alimpulizia mtu wa namana hiyo insect spray machoni jamaa alikimbia kama mbwa koko- learn self defence tactics hakuna zaidi.
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Kama tunachanganya mada vile!: niorodheshee nonspuriously kile ambacho hao akina EL+RA wamekwiba. Orodha hii itanisaidia sana.
   
 11. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mwaka jana kamishna wa polisi alipiga marufuku kukamatwa au kusingizia raia hivyo vitendo
  kama vimefanyika ndani ya gari.Wanachofanya ni kinyume cha sheria.
  Next time ikikutokea usiwape hela,omba wakupeleke kituoni.
  Watakacho fanya watapanda gari lako,wakijidai wankupeleka kituoni.
  Mkifika jirani na kituo na bado unakataa kutoa hela,watakuachia.
   
Loading...