Angalizo: Watu wa Mbeya mnaoishi Mbeya Mjitathimini mienendo yenu kinidhamu inalichafua Jiji, ipo siku jiji litafutwa

Kikwava

JF-Expert Member
Sep 6, 2015
1,741
1,069
Husika na kichwa Cha habari hapo juu.

Tofauti na ilivyo kwenye majiji mengine Kama vile Dodoma, Arusha, Tanga na kwingineko Ila tabia na matendo ya watu wa Mbeya kwa wageni na kwa miundombinu ni hatari mno kwa usitawi wa amani na maendeleo ya jiji Hilo la Mbeya. Haya yafuatayo ndo yanakichafua Jiji la Mbeya;

1. Wizi wa Solar za taa za barabarani, haya mambo yanafanywa na wenyeji na hutaona tabia hizi hata kwenye Halmashauri tu.

2. Kuwashambulia wageni hasa wale wanakuja kwa ajili ya kufanya matamasha. Tumeona juzi hapa msanii akirushiwa makopo ya maji bila sababu, hii inachafua taswira ya Jiji la Mbeya, baadae wasanii watakuwa hawaji

Pia, Soma: Wasafi Festival Mbeya hali imekuwa tete. Zuchu akimbia Jukwaa

Yapo mengi sana yakuorodhesha hapa lakini kwa leo naomba niishie hapo ili nipate muda wa kuyajadili haya.

NB: Hizo tabia zikiendelea ipo siku jiji la Mbeya litafutwa na kuwa halmashauri ya Mji mdogo, tunawaomba viongozi wetu endeleni kutoa adhabu Kali kwa wote wanaolichafua jiji, pia hizo taa za barabarani wekeni doria kuzilinda.
 
Tangu nifanyiwe ubaguzi wa kidini huo mkoa sina habari nao , siwezi kuwachukia maana wengine ni marafiki zangu ...Nimeona baadhi ya rafiki zangu wanaunga mkono huo upuuzi.
Itakua ulikutana na wasafwa, wale wana ubaguzi hata kwa mtu asie wa kabila lao.
Sasa kama ni muislam, umetoka mkoa mwingine na ni kabila jingine aloo hamna rangi utaacha kuona.
 
Inawezekana kweli wamekosea? Lakini nani anafurahishwa na tabia za wasanii kuhusishwa husishwa na Ushoga? Au wewe unafurahishwa?

Kukataliwa kupo kwenye maisha, sio kila mara utapendwa, lazima ujifunze kupitia makosa na ubadilike....

Kuhusu kufutwa jiji, nafikiri umekurupuka, mji unachukua muda sana kujengeka mpaka kuwa jiji, kulishusha jiji ghafla kua mji maana yake uvuruge hii mifumo yoye isiwepo 👇👇
Screenshot_20240930-063452.png
 
Back
Top Bottom