Angalizo: Wanaoweka matangazo ya kutafuta Kazi

Mambo natafuta kazi ya ualimu kwa English Medium namba yangu ni 0714954609 nipo Arusha.Kwa masomo ya Mathematics,Civic and moral,Kiswahili,History
 
Naamn na mm umenigusa sana
Ndugu yangu ahsante wapo watu wanahoji kuliko kuangalia sababu kama nafasi ipo lazima nikupe kila kitu curriculum vitae(CV), application na Certificates cjui wanajua labda ni wa ujanja
 
Natafuta kazi ya librarian au records management kwa atakayeguswa plz weka comment hapo chini.
 
Lahe hotels ya Mwanza inahitaji mlinzi kutoka JKT,dereva,barman,chef,service/waiter na mhasibu,cashier mwisho wa maombi 4.11.2018- 0655290084

Mm nahitaji nafasi ya udereva ila nipo Dar es Salaam 0692410906 Milton mushi
 
Npo kuwa yeyote hapo kasoro dereva tu,elimu yangu n advanced diploma chamsingi mshahara tu
Lahe hotels ya Mwanza inahitaji mlinzi kutoka JKT,dereva,barman,chef,service/waiter na mhasibu,cashier mwisho wa maombi 4.11.2018- 0655290084
 
Natafuta nafasi ya Ualimu wa Chuo cha Ualimu,elimu ni Bachelor degree of Education,with Arts Masomo ni History Kiswahili ingawa ninauwezo wa kufundisha masomo mengine mawasiliano +255744189384
 
Jmn msaada ninatafuta kazi ya kuuza vitu supermarket,duka la nguo au stationary yyte ile nipo mwanza
Nmb-0675725932
 
Natfta kazi za hotelini na stationary, [ ninauwezo wa kutumia computer ipaswavyo na pia ni mpishi mzuri wa chapati ] namba zangu ni 0754064990 au 0717585596
 
thumb20.jpg


Salaam!

Ni muda sasa humu Jukwaani kumekuwa na mabandiko ya watu mbalimbali wakiomba kazi, zile za ujuzi mahususi na zile za jumla.

Baadhi ya wanaoandika wamekuwa wakitaja sifa zao, wengine wakitaja kwa upana na wengine kwa ufupi sana na wakati mwingine bila taarifa zozote zitakazomwezesha mwajiri kupata fununu za mtu anayetaka kumuajiri.

Kama ambavyo wanaoweka matangazo ya kazi waliaswa hapa: ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu nadhani ni wakati wa wanaoweka matangazo ya kusaka kazi pia tukazingatia vigezo kadha wa kadha.

Walau tangazo la kutafuta kazi liwe na vitu vifuatavyo:


  • Wasifu, kwa kuwa kanuni za JF zinalinda haki ya faragha, utambulisho uhusishe wasifu mwingine ISIPOKUWA majina. Mathalani, mwombaji anaweza kusema kuwa yeye ni kijana mwenye umri wa miaka XX anayepatikana eneo XY.
  • Elimu, hii inasaidia mtu ambaye anaomba kazi kuweka wazi elimu aliyonayo, iwe ya jumla au ya utaalamu mahususi. Waajiri au wenye kujua fursa za ajira wangependa kujua elimu aliyonayo mhitaji ili wamsaidie iwezekanavyo.
  • Uzoefu. Hiki ni kigezo kinachompa sifa za ziada mwombaji. Ni vema kusema kama umewahi kufanya kazi, semina ama kuhudhuria mafunzo fulani maalumu kwani itaongeza ushindani wa mwombaji.
  • Mapendeleo. Kutaja elimu na uzoefu pekee hakutoshi, ni vema muombaji/mhitaji akaweka wazi kazi, eneo, mazingira ya kazi ambayo anayapendelea pamoja na vitu vingine vya ziada. Kuandika kwa ujumla sana hupelekea wasio na nia njema kujibu kwa kejeli na dhihaka. Kuwa mahususi na kazi itakiwayo kutapunguza majibu mengi yasiyofaa kwa mwombaji.
  • Andiko lisiwe na nia ya kuvuta sana usikivu. Maandiko yenye uelekeo wa kulia-lia, kutangaza kuwa maisha ni magumu na hujui ufanyaje hakurahisishi harakati za kupata kazi. Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia uhitaji huo uliopitiliza kwa manufaa yao kiuchumi (utapeli) na hata kingono (hasa kwa mabinti).

Nawatakieni kila lililo jema katika harakati za kusaka ajira!
Tunashukuru kiongoz kwa kutuelimiisha
 

Similar Discussions

86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom