Angalizo: Wanaoweka matangazo ya kutafuta Kazi

Rugby Union

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
402
248
thumb20.jpg


Salaam!

Ni muda sasa humu Jukwaani kumekuwa na mabandiko ya watu mbalimbali wakiomba kazi, zile za ujuzi mahususi na zile za jumla.

Baadhi ya wanaoandika wamekuwa wakitaja sifa zao, wengine wakitaja kwa upana na wengine kwa ufupi sana na wakati mwingine bila taarifa zozote zitakazomwezesha mwajiri kupata fununu za mtu anayetaka kumuajiri.

Kama ambavyo wanaoweka matangazo ya kazi waliaswa hapa: ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu nadhani ni wakati wa wanaoweka matangazo ya kusaka kazi pia tukazingatia vigezo kadha wa kadha.

Walau tangazo la kutafuta kazi liwe na vitu vifuatavyo:


  • Wasifu, kwa kuwa kanuni za JF zinalinda haki ya faragha, utambulisho uhusishe wasifu mwingine ISIPOKUWA majina. Mathalani, mwombaji anaweza kusema kuwa yeye ni kijana mwenye umri wa miaka XX anayepatikana eneo XY.
  • Elimu, hii inasaidia mtu ambaye anaomba kazi kuweka wazi elimu aliyonayo, iwe ya jumla au ya utaalamu mahususi. Waajiri au wenye kujua fursa za ajira wangependa kujua elimu aliyonayo mhitaji ili wamsaidie iwezekanavyo.
  • Uzoefu. Hiki ni kigezo kinachompa sifa za ziada mwombaji. Ni vema kusema kama umewahi kufanya kazi, semina ama kuhudhuria mafunzo fulani maalumu kwani itaongeza ushindani wa mwombaji.
  • Mapendeleo. Kutaja elimu na uzoefu pekee hakutoshi, ni vema muombaji/mhitaji akaweka wazi kazi, eneo, mazingira ya kazi ambayo anayapendelea pamoja na vitu vingine vya ziada. Kuandika kwa ujumla sana hupelekea wasio na nia njema kujibu kwa kejeli na dhihaka. Kuwa mahususi na kazi itakiwayo kutapunguza majibu mengi yasiyofaa kwa mwombaji.
  • Andiko lisiwe na nia ya kuvuta sana usikivu. Maandiko yenye uelekeo wa kulia-lia, kutangaza kuwa maisha ni magumu na hujui ufanyaje hakurahisishi harakati za kupata kazi. Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia uhitaji huo uliopitiliza kwa manufaa yao kiuchumi (utapeli) na hata kingono (hasa kwa mabinti).

Nawatakieni kila lililo jema katika harakati za kusaka ajira!

 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri wenye kujenga, na kuelimisha maana kweli wengi wetu tunatafuta kazi na pengine tunakosa kazi kwasababu hatutoi taarifa zetu za kutosha ama tunaomba kazi kwakuorodhesha changamoto za maisha zinazotukabili.

Hakika soko la ajira nchini inachangamoto kubwa sana ikiwa na wahitimu wengi kutoka vyuo vikuu nchini na vyuo vingine vidogo vidogo, hivyo sisi kama Watanzania wenye nia njema na wenzetu na nchi yetu kwa ujumla, tusaidiane kwa hili hasa kwa hali na mali, ili kuweza kuendeleza uchumi wetu na ustawi wa nchi yetu kwa ujumla.

Chonde chonde kwa wote watakao fanikiwa kuona meseji hii kila mmoja kwa nafasi yake, awaze kutoa mchango wake kwa hili, kwani nchi ikiendelea mafanikio ni kwa wote sio kwa wachache.

Mungu awabariki wote:angry:
 
asante kwa ujumbe mzuri mdau,na nikweli point ya mwisho watu wengi tunapenda kuitumia tukidhani itaturahisishia kupata kazi kumbe inaweza kua point of weakness au kuwa faida kwa waajiri au matapeli wasio na nia nzuri,mimi mwenyewe hapa bado ni muhanga wa ajira
 

Similar Discussions

86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom