ANGALIZO: Wanaokwenda kumwona kichanga baada ya kuzaliwa ndiyo wanaoshika hatma yake (umaskini na mahangaiko, utajiri na furaha)

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wadau, poleni kwa kazi. Kuna utamaduni (nadhani kwa nia njema) mwanamke akishajifungua, wapo watu (hususan majirani tena wanawake) hufunga safari kwenda kumwona mtoto.

Katika 'ziara' hiyo wageni hao hubeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kumpa hongera mama (mzazi) kwa kupata mtoto ambaye inaaminika ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Zawadi hizo zinaweza kuwa, pea ya kanga, kitenge au hata chakula, kama vile unga, sukari n.k. wapo wenye uthubutu hata wa kununua vitu vya mtoto (kichanga) kama nguo, poda, besenj, sabuni, mafuta nk.

Lakini kwa mujibu wa mzee mmoja wa kimila toka Kabila la wamakonde aitwaye Maandazi Baridi, baadhi ya watu wanaokwenda kumwona kichanga ndiyo wanaobeba hatima ya maisha yake ya mbele.

Maandazi Baridi anasema: "Wengi wa wanaokwenda kumwona mtoto hushika vitu vya ushirikina mikononi mwao (akimaanisha uchawi). Wanamwona mtoto halafu wanamwachia 'uchawi' wao huku wakijifanya wao ni watu au majirani wema.

"Ndiyo maana unaweza kukuta mtoto anakua lakini hata mvuto, nyota wala mafanikio. Mwingine anakosa hata akili. Anasoma lakini hafiki popote. Umaskini unamjaa. Kijana akifikisha umri wa kujitegemea hana la maana, ni mahangaiko mwanzo mpaka mwisho mpaka anajuta kuzaliwa.

"Kwa wasiyojua haya watasema ni mipango ya Mungu. Lakini ukweli ni kwamba, baadhi ya watu wanaofika kumwona mtoto si wazuri. Wapo watu hawaamini uchawi. Lakini nasema, uchawi upo. Hata vitabu vya dini Mungu alisema uchawi upo ila alitaka wanadamu tusiufuate."

NINI KIFANYIKE?
Mwisho mzee Maandazi Baridi alishauri wanawake wanaotoka kujifungua, kutowapa watoto wao wageni wanaofika kuwaona kama wana wasiwasi nao.

Alisema: "Akija mtu kumwona mtoto, mkaribishe sebuleni, toka wewe, mtoto mwache chumbani. Lakini kubwa na zuri zaidi, ukishajifungua salama ukarudi nyumbani na mtoto wako, mwite kiongozi wa kidini (kwa imani husika) ili amweke mtoto mikononi mwa Mungu.

"Hata Yesu (kwa Wakristo) alipozaliwa, wazazi wake walimpeleka madhabahuni ili kumkabidhi kwenye mikono salama ya Mungu," alisema mzee huyo.
 
Hatima ya mtu iko kwenye personal choices zake mwenyewe. Acha kuudanganya umma wa Watanzania. Hivi sasa tunashughulika na hoja ya kudai Bi Mkubwa aachie ngazi 2025, sawa?
 
Back
Top Bottom