Angalizo: Wanaoishi mabondeni Dar, hamieni Milimani sababu mafuriko yanakuja

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,621
Points
2,000

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,621 2,000
Habari wakuu,

Itakuwa ni aibu kwa watu wa Dar kulalamika kwamba godoro, hela, tv, viti nk kwamba vimesombwa na maji ya mafuriko.

Natumia jukwaa hili kuwaomba na kuwasihi hameni mabondeni, hamisheni vitu vinavyobebwa na maji. Pangeni kwa muda milimani pasipo na mafuriko.

Pili, wale wenye magari, usipite kwenye maji ya mafuriko. Subiri hadi maji yapungue uvuke salama, madaraja na barabara nyingi haviko salama. Ni aibunkwa dereva msomi gari lake kubebwa na maji kisa analazimisha kupita.

Tatu msiguse nyaya za tanesco zilizo lala njiani wala kuzisogelea.

Msitupe maji taka au taka ngumu kwenye mitaro.

Serikali andaeni sehemu maalum ya kupokea wahanga wa mafuriko kila Wilaya.

Hii mvua inayokuja sio ya kumruhusu mtoto mdogo aende shule mwenyewe hasa za chekechea.

Serikali andaeni dawa za magonjwa ya mlipuko. Mia
 

Forum statistics

Threads 1,381,202
Members 526,018
Posts 33,792,359
Top