ANGALIZO!tuweni makini na maneno yaliyoandikwa kwenye nguo zetu kama yana maana nzuri.

Tajirimsomi

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
4,632
2,000
Habari ndugu zangu watanzania,naamini ni siku nzuri poleni na stress mbalimbali kuhusu maisha ila yote ni katika kuhakikisha maisha yanasonga mbele.

Nimekuja na mada apo juu tuweze kushare mawazo niliyonayo juu ya hilo.Nimekuja na hii mada maana mwenzenu yamenikuta bwana.

Uwa Nina tabia ya kuvaa nguo za mitumba na nazipenda sana siwazi kuziacha ila navaaga mitumba quality. Kuna T-shirt yangu moja nzuri uwa napenda sana kuivaa nikiwa nyumbani nilinunuaga kwa machinga ina sentensi mbili za kingereza nyuma na mbele,ayo maneno nilikuwa sijawai kujishughulisha kuyasoma na kujua maana yake sasa Leo wakati naifua ndo akili zikanituma kuyasoma ayo maneno duh nimejuta kuyafahamu nimekuta ni bonge la matusi na mipasho ya kike akiyamungu nimejuta sana na nguo nimeitupa.

Angalizo:nawashauri ndugu zangu tuwe makini na nguo zenye maandishi ikiwezekana tuachane nazo kabisa
f2216ba41680c6a2afb4b7dc59d735c4.jpg
29ba5e6fd597f9d464ea51ff4436c62d.jpg
 

Erickford4

JF-Expert Member
May 22, 2017
1,139
2,000
Ndio uwe unasoma na kuelewa maana yake.. Mimi sivai nguo bila ya kuielewa maana ya maandishi yaliyoandikwa.. ndio maana sipendi nguo zenye maandishi ya kichina maana sijui kilichoandikwa
 

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,139
2,000
Hahaha!. Mimi siyo mshabiki wa Nguo zenye nembo na Maandishi.

Isipokuwa Jezi tu..... Nyingine zote zivai yenye maandishi yeyote.
 

dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,756
2,000
Uzuri.mmoja kati kumi ni watatu ndo wataelewa ulichovaa kimeandikwaje maneno mengine hayako waziwazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom