Angalizo: Tusianze kutukana kuwa wapinzani wananunuliwa au Rais anataka kuua upinzani

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
7,999
2,000
Mama Samia anachapa kazi sana, hili lipo wazi na Mimi nikiwa mmoja wa vijana wake wanaomkubali kupindukia ninataka kuweka angalizo.

Maana Kuna vijana humu kutoka ule mtaa Wana matamanio yao Ila yasipotimizwa huanza kutukana, HII HAITAKUBALIKA.

Maana wanapenda Sana kuishi kwa matamanio ambayo wakati mwingine hayawezekani. Walianza kutamani baraza la mawaziri livunjwe, wakaja kutamani Mara Raisi akienda kuhutubia bunge atalivunja. Na walikuwa serious kabisa kuwa bunge litavunjwa.

Hivyo ni vema kuwapa aangalizo maana Wana matusi sana, uteuzi utapoanza msianze kusema anaua upinzani mara hivi Mara vile.

Uteuzi wa upinzani ulipofanyika kwa Anna Mghwira, kitila na wengine kipindi hicho walianza kufurahia Ila baadae walianza kulialia.
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,019
2,000
Kwania njema aliyokuwanayo,na mabadiliko aliyoamua kuyafanya anaweza kuthibitisha nia njema aliyokuwa nayo anaweza kupata imani ya watu kwa kiwango cha kuridhisha.
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,813
2,000
Kwa mtu anayejua siasa nikweli anawaweaken wapinzani, mfano Mbowe ateuliwe kuendesha idara fulani halafu ifail unadhani atapata wapi nguvu ya kuikosoa gavamenti? Kila mtu atamuuliza pale kwako mbona kuna abcd,ni mbinu za medani mkuu, japo kujenga nchi ni jukumu letu sote.

NB:Unatekeleza ilani ya sisiemu, ikifail mnafail wote
 
Kukata tamaa mwiko,ili mradi nia no kuona hali ya mambo inabadilika kweli,sii kwa propaganda au hila.
 
Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,813
2,000
Kukata tamaa mwiko,ili mradi nia no kuona hali ya mambo inabadilika kweli,sii kwa propaganda au hila.
Shida siyo yeye, system iliyopo je ipo tayari? Kama tu wale wanaoitwa wamekatwa mikia hawapendwi sana ndani ya sisiemu pending wanapopata teuzi, what do you expect from opposition side? Pia kwa namna serikali ilivyo ni ngumu kuiepucha na chama, mfano RC automatic anaingia mikutano ya ndani ya chama cha sisiemu.......kifupi kunakaugumu fulani kutenganisha chama na gavamenti sevanti
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
9,272
2,000
We jama kama sigara kali
Muache mama atengeneze umoja wa kitaifa uliouliwa na mwendazake
Tofauti ni kwamba mama atachukua hata upinzani bila kuhonga au kumnunua kama alivyofanya mwendazake
 
MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
3,791
2,000
Nina mashaka makubwa sana na motive hii.
Kwa siasa za kwetu hapo hakuna nia njema bali lengo kuu ni kudhoofisha upinzani.
Utendaji wa serikali yetu hauwezi kumpa fursa sawa waziri mwenye kadi ya Chadema na Waziri wa CCM.
Hii ni calculated move ambayo watu myopic hawawezi kuona kilichojificha.
Uzuri ni kuwa pinzani ni imani.
 
Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
5,019
2,000
Shida siyo yeye, system iliyopo je ipo tayari? Kama tu wale wanaoitwa wamekatwa mikia hawapendwi sana ndani ya sisiemu pending wanapopata teuzi, what do you expect from opposition side? Pia kwa namna serikali ilivyo ni ngumu kuiepucha na chama, mfano RC automatic anaingia mikutano ya ndani ya chama cha sisiemu.......kifupi kunakaugumu fulani kutenganisha chama na gavamenti sevanti
Ugumu uko hapa,teuzi zinapo egemea ukada,ambapo mtindo wa kulindana ni mkubwa utendaji ukiegemea mirengo ya kiitikadi na matamko na maelekezo ya kisiasa,haya yakikoma tutaweza kusonga mbele .
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
580
1,000
Naona labda Mama anataka kutumia hiyo smart-trick kuzidi kupunguza kabisa nguvu ya upinzani, lakini akumbuke vyama hivyo ni muhimu siku zote ktk mfumo wa vyama vingi, kumsaidia kama check and balance katika utendaji wa serikali yoyote.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
42,576
2,000
Mama Samia anachapa kazi Sana, hili lipo wazi na Mimi nikiwa mmoja wa vijana wake wanaomkubali kupindukia ninataka kuweka angalizo.
Maana Kuna vijana humu kutoka ule mtaa Wana matamanio yao Ila yasipotimizwa huanza kutukana, HII HAITAKUBALIKA.
Maana wanapenda Sana kuishi kwa matamanio ambayo wakati mwingine hayawezekani. Walianza kutamani baraza la mawaziri livunjwe, wakaja kutamani Mara Raisi akienda kuhutubia bunge atalivunja. Na walikuwa serious kabisa kuwa bunge litavunjwa.
Hivyo ni vema kuwapa aangalizo maana Wana matusi Sana, uteuzi utapoanza msianze kusema anaua upinzani mara hivi Mara vile.
Uteuzi wa upinzani ulipofanyika kwa Anna mghwira, kitila na wengine kipindi hicho walianza kufurahia Ila baadae walianza kulialia.

Jiwe alikuwa anafanya biashara ya Utumwa.
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
191,348
2,000
Tuwaache waendelee mapambio siku wakishtuka tayari wameshapoteza credits za maana
 
Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
697
1,000
Kwa mtu anayejua siasa nikweli anawaweaken wapinzani, mfano Mbowe ateuliwe kuendesha idara fulani halafu ifail unadhani atapata wapi nguvu ya kuikosoa gavamenti? Kila mtu atamuuliza pale kwako mbona kuna abcd,ni mbinu za medani mkuu, japo kujenga nchi ni jukumu letu sote.

NB:Unatekeleza ilani ya sisiemu, ikifail mnafail wote
Lakini Rais Alisema kama mteuliwa ana vigezo vya elimu nzuri,na weledi na Hana makandokando yanayohatarisha usalama wa Taifa atamteua tuu bila kujali itikadi,jinsia au kabila
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom