Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee!
Nianze na ziara yako kikazi nchini Kenya ambapo ulitilia mkazo sera ya "kufungua nchi" wengi wanaoshangilia wanataka ukosee ili wapate mtaji kisiasa huko mbeleni; pamoja na uungwana wa Mzee Kikwete huyo Kenyatta alishawishi Uganda na Rwanda kutengeneza genge lilioitwa "coalition of the willing" dhumuni kuu walitaka JK afungue nchi ikiwamo kukubali "single tourist visa". Zaidi, miaka hiyo tulishuhudia Wakenya wengi wakiajiriwa kwenye mahoteli yaliyopo Tanzania kwa kigezo kuwa wanajua "customer service". Vijana wa kitanzania walikosa ajira kutokana na nchi "kufunguliwa" na kutoa vibali vya ajira ovyo.
Suala la pili ni wachuuzi wadogo wadogo kwa jina maarufu Wamachinga. Hili suala lina historia ndefu tangu Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Mwinyi hadi leo hii. Kuna kipindi Halmashauri, Manispaa na Majiji yaliajiri migambo na kazi yao kubwa ilikuwa ni kudhibiti Machinga na mama lishe. Udhibiti mbovu wa watu hawa ndio uliifanya CHADEMA ikapata mtaji kisiasa maeneo ya mijini kwani waliwaahidi endapo watawachagua basi watawapa uhuru kufanya shughuli zao na wataondoa migambo.
Hapa wanasubiri ukosee ili warudi kwenye umaarufu wao. Kimsingi Wafanyabiashara hawa wadogo wadogo hufuata maeneo yenye watu wengi ili kuuza bidhaa zao na kupata riziki. Moja ya suluhisho kuwaruhusu wafanye biashara baadhi ya mitaa/barabara na magari yasipite kabisa huko na kutenga barabara za kupita magari tu hapa wataalam wa serikali watasaidia jinsi ya kiboresha zaidi. Tujifunze kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu kama India, Nigeria nk.
Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi sauti ya Mungu.