Angalizo: Rais Samia kuwa makini na unayoyaacha leo, CHADEMA watayatumia kuibuka kisiasa

Ndugu zangu,

Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee!

Nianze na ziara yako kikazi nchini Kenya ambapo ulitilia mkazo sera ya "kufungua nchi" wengi wanaoshangilia wanataka ukosee ili wapate mtaji kisiasa huko mbeleni; pamoja na uungwana wa Mzee Kikwete huyo Kenyatta alishawishi Uganda na Rwanda kutengeneza genge lilioitwa "coalition of the willing" dhumuni kuu walitaka JK afungue nchi ikiwamo kukubali "single tourist visa". Zaidi, miaka hiyo tulishuhudia Wakenya wengi wakiajiriwa kwenye mahoteli yaliyopo Tanzania kwa kigezo kuwa wanajua "customer service". Vijana wa kitanzania walikosa ajira kutokana na nchi "kufunguliwa" na kutoa vibali vya ajira ovyo.

Suala la pili ni wachuuzi wadogo wadogo kwa jina maarufu Wamachinga. Hili suala lina historia ndefu tangu Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Mwinyi hadi leo hii. Kuna kipindi Halmashauri, Manispaa na Majiji yaliajiri migambo na kazi yao kubwa ilikuwa ni kudhibiti Machinga na mama lishe. Udhibiti mbovu wa watu hawa ndio uliifanya CHADEMA ikapata mtaji kisiasa maeneo ya mijini kwani waliwaahidi endapo watawachagua basi watawapa uhuru kufanya shughuli zao na wataondoa migambo.

Hapa wanasubiri ukosee ili warudi kwenye umaarufu wao. Kimsingi Wafanyabiashara hawa wadogo wadogo hufuata maeneo yenye watu wengi ili kuuza bidhaa zao na kupata riziki. Moja ya suluhisho kuwaruhusu wafanye biashara baadhi ya mitaa/barabara na magari yasipite kabisa huko na kutenga barabara za kupita magari tu hapa wataalam wa serikali watasaidia jinsi ya kiboresha zaidi. Tujifunze kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu kama India, Nigeria nk.

Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi sauti ya Mungu.
Tunawapelekea moto. Sukuma gang mtajua hamjui.
 
Dhumuni la chama cha siasa ni kushika dola
Mkuu sio hilo tu kuna madhumuni mengi tu ndani ya plitical party,tunachotaka wananchi ni kuwa na uhuru wa haki na kuishi kwa mujibu wa kisheria zilizomo kikatiba sio kuwa na one powerful human being kutuamulia mwenendo wa maisha yetu,Pls mkuu tumuunge mkono our President (personal sio mpenzi kabisa wa ccm)ila President Samia ameonyesha kuwa Tanzania belongs to everyone one sio wateule wachache,viva president Samia viva!!!
 
Uhuru wenye mipaka na wajibu

Kamanda karibu CCM tujenge nchi,acha kulia lia
Kwishaaaaaaaa habari zenu nyinyi mashetani wa kisiasa.

Mlitawala nchi kwa chuki na fitina na kujiona kuwa nyinyi ndiyo bora kuliko wenzenu .

Hii leo mnalialia kisa mama kuamua kuongoza nchi kwa misingi ya haki na umoja wa kitaifa.
 
Ndugu zangu,

Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee!

Nianze na ziara yako kikazi nchini Kenya ambapo ulitilia mkazo sera ya "kufungua nchi" wengi wanaoshangilia wanataka ukosee ili wapate mtaji kisiasa huko mbeleni; pamoja na uungwana wa Mzee Kikwete huyo Kenyatta alishawishi Uganda na Rwanda kutengeneza genge lilioitwa "coalition of the willing" dhumuni kuu walitaka JK afungue nchi ikiwamo kukubali "single tourist visa". Zaidi, miaka hiyo tulishuhudia Wakenya wengi wakiajiriwa kwenye mahoteli yaliyopo Tanzania kwa kigezo kuwa wanajua "customer service". Vijana wa kitanzania walikosa ajira kutokana na nchi "kufunguliwa" na kutoa vibali vya ajira ovyo.

Suala la pili ni wachuuzi wadogo wadogo kwa jina maarufu Wamachinga. Hili suala lina historia ndefu tangu Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Mwinyi hadi leo hii. Kuna kipindi Halmashauri, Manispaa na Majiji yaliajiri migambo na kazi yao kubwa ilikuwa ni kudhibiti Machinga na mama lishe. Udhibiti mbovu wa watu hawa ndio uliifanya CHADEMA ikapata mtaji kisiasa maeneo ya mijini kwani waliwaahidi endapo watawachagua basi watawapa uhuru kufanya shughuli zao na wataondoa migambo.

Hapa wanasubiri ukosee ili warudi kwenye umaarufu wao. Kimsingi Wafanyabiashara hawa wadogo wadogo hufuata maeneo yenye watu wengi ili kuuza bidhaa zao na kupata riziki. Moja ya suluhisho kuwaruhusu wafanye biashara baadhi ya mitaa/barabara na magari yasipite kabisa huko na kutenga barabara za kupita magari tu hapa wataalam wa serikali watasaidia jinsi ya kiboresha zaidi. Tujifunze kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu kama India, Nigeria nk.

Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi sauti ya Mungu.
Umesahau katiba mpya wanasema sio muhimu kwao sisi tutaibuka na ilo
 
Back
Top Bottom