Angalizo: Rais Samia kuwa makini na unayoyaacha leo, CHADEMA watayatumia kuibuka kisiasa

Waliofurahi na kushangalia miaka kadhaa nyuma sasa ndio vinara wa kulia na huzuni ni ajabu na kweli
 
Jenga hoja kamanda
Kwishaaaaaaaa habari zenu nyinyi mashetani wa kisiasa.

Mlitawala nchi kwa chuki na fitina na kujiona kuwa nyinyi ndiyo bora kuliko wenzenu .

Hii leo mnalialia kisa mama kuamua kuongoza nchi kwa misingi ya haki na umoja wa kitaifa.
 
Binafsi naona niwakati mzuri sasa chadema wakicheza vizuri na kumsimamisha mgombea mzuri anaye kubalika Kama alivyo kubalikaga doctor slaaa 2025 wanachukua nchi asubuhi kweupeeeee,
Nasema hivi kwasababu kuu mbili,(1)Kanda ya ziwa kipindi Cha doctor ndiyo ilikuwa ngome kuu ya chadema na kiuhakisia ndiyo yenye watu wengi zaidi Tz,
2)Mpaka Sasa hivi Kuna zaidi ya mpasuko chama tawaka, yapo makundi zaidi ya Matatu Jambo ambalo naamini wote watawapigia Kira upinzani.
3)Yalisha tabiriwa na baba wa Taifa kuwa CCM isipo fanya vzr mwisho wake n 2020,
My take"Chadema muda ndiyo huu, utumieni vzuri"
yupi unaona anafaa kusmamishwa
 
Sawa kamanda
Kusema za ukweli, tangu Wakenya walivyozuiliwa kuajiriwa kwenye mahoteli hapa Tanzania (esp kwenye eneo la waiters & waitresses) customer service kwenye mahoteli husika imeporomoka vibaya sana. Uswahili mtupu na nyodo kibao ndivyo vimetamalaki!
 
CCM itaendelea kutawala kamanda
Ikiendelea kutawala kwa misingi ya kuheshimu katiba, kutawala kwa kuheshimu haki za binadamu na ikiongozwa na rais anayejali na kuheshimu watu wake bil ubaguzi haina tatizo.

Kayafa aliiharibu nchi tukaishi kama tupo gisenyi kwenu.
 
Watu wenye fikra hasi, hawana msaada wowote kwa Taifa.

Coliation of the Willing iliundwa kwa sababu ya tatizo la Magufuli la kutotaka kushirikiana na nchi wanachama wa EAC.

Rais Samia, upo kwenye njia sahihi. Chukua mawazo ya watu positive. Hawa negative people, achana nao.
 
Tupo hapa miezi ijayo na mama yenu msipige mayowe tu,mwenyewe kakiri majizi yameanza kutamalaki
 
Ndugu zangu,

Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee!

Nianze na ziara yako kikazi nchini Kenya ambapo ulitilia mkazo sera ya "kufungua nchi" wengi wanaoshangilia wanataka ukosee ili wapate mtaji kisiasa huko mbeleni; pamoja na uungwana wa Mzee Kikwete huyo Kenyatta alishawishi Uganda na Rwanda kutengeneza genge lilioitwa "coalition of the willing" dhumuni kuu walitaka JK afungue nchi ikiwamo kukubali "single tourist visa". Zaidi, miaka hiyo tulishuhudia Wakenya wengi wakiajiriwa kwenye mahoteli yaliyopo Tanzania kwa kigezo kuwa wanajua "customer service". Vijana wa kitanzania walikosa ajira kutokana na nchi "kufunguliwa" na kutoa vibali vya ajira ovyo.

Suala la pili ni wachuuzi wadogo wadogo kwa jina maarufu Wamachinga. Hili suala lina historia ndefu tangu Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Mwinyi hadi leo hii. Kuna kipindi Halmashauri, Manispaa na Majiji yaliajiri migambo na kazi yao kubwa ilikuwa ni kudhibiti Machinga na mama lishe. Udhibiti mbovu wa watu hawa ndio uliifanya CHADEMA ikapata mtaji kisiasa maeneo ya mijini kwani waliwaahidi endapo watawachagua basi watawapa uhuru kufanya shughuli zao na wataondoa migambo.

Hapa wanasubiri ukosee ili warudi kwenye umaarufu wao. Kimsingi Wafanyabiashara hawa wadogo wadogo hufuata maeneo yenye watu wengi ili kuuza bidhaa zao na kupata riziki. Moja ya suluhisho kuwaruhusu wafanye biashara baadhi ya mitaa/barabara na magari yasipite kabisa huko na kutenga barabara za kupita magari tu hapa wataalam wa serikali watasaidia jinsi ya kiboresha zaidi. Tujifunze kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu kama India, Nigeria nk.

Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi sauti ya Mungu.
Shida yako wivu na roho mbaya imekukaa Sana.
 
Ndio maana Chadema inawakimbiza cccm imewafanya nyie mazezeta hamtaki kupambana na maisha Dunia ya leo mambo hayaji kwenye kisahani lazima kupamba asee ndio maana wengi wenu hamjamaliza wa jiwe maana alitumia bunduki kuwapa vyeo poleni sana SAMIA anatia akili

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi
Yaani MATAGA mko so desperate! Mara Chadema wanapinga kila kitu, Leo Chadema wanasapoti mnageuka tena, eti watatumia kama mtaji wa kisiasa, ulitaka watumie kama mtaji wa Nini? Wa bangi? Pumbavu zako. Jiwe ameshapumzika, mkubalini Samia
 
Back
Top Bottom