Angalizo: Rais Samia kuwa makini na unayoyaacha leo, CHADEMA watayatumia kuibuka kisiasa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,250
2,000
Ndugu zangu,

Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano, Kazi iendelee!

Nianze na ziara yako kikazi nchini Kenya ambapo ulitilia mkazo sera ya "kufungua nchi" wengi wanaoshangilia wanataka ukosee ili wapate mtaji kisiasa huko mbeleni; pamoja na uungwana wa Mzee Kikwete huyo Kenyatta alishawishi Uganda na Rwanda kutengeneza genge lilioitwa "coalition of the willing" dhumuni kuu walitaka JK afungue nchi ikiwamo kukubali "single tourist visa". Zaidi, miaka hiyo tulishuhudia Wakenya wengi wakiajiriwa kwenye mahoteli yaliyopo Tanzania kwa kigezo kuwa wanajua "customer service". Vijana wa kitanzania walikosa ajira kutokana na nchi "kufunguliwa" na kutoa vibali vya ajira ovyo.

Suala la pili ni wachuuzi wadogo wadogo kwa jina maarufu Wamachinga. Hili suala lina historia ndefu tangu Serikali ya awamu ya pili ya Mzee Mwinyi hadi leo hii. Kuna kipindi Halmashauri, Manispaa na Majiji yaliajiri migambo na kazi yao kubwa ilikuwa ni kudhibiti Machinga na mama lishe. Udhibiti mbovu wa watu hawa ndio uliifanya CHADEMA ikapata mtaji kisiasa maeneo ya mijini kwani waliwaahidi endapo watawachagua basi watawapa uhuru kufanya shughuli zao na wataondoa migambo.

Hapa wanasubiri ukosee ili warudi kwenye umaarufu wao. Kimsingi Wafanyabiashara hawa wadogo wadogo hufuata maeneo yenye watu wengi ili kuuza bidhaa zao na kupata riziki. Moja ya suluhisho kuwaruhusu wafanye biashara baadhi ya mitaa/barabara na magari yasipite kabisa huko na kutenga barabara za kupita magari tu hapa wataalam wa serikali watasaidia jinsi ya kiboresha zaidi. Tujifunze kutoka nchi zenye idadi kubwa ya watu kama India, Nigeria nk.

Nimalize kwa kuendelea kukusisitiza usione CHADEMA wanakushangilia, wanataka ukosee na kisha wapate mtaji wa kisiasa kuibuka kwani wamezama. Sauti ya wengi sauti ya Mungu.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,787
2,000
Tribalism,Regionism on work,Hili Gang bila kulisambaratisha Mama atapata wakati mgumu sana kufikia Matamanio ya Watanzania,ni muhimu akaanza nalo coz limesambaa hadi huku JF kumtisha na kumharibia Move
Hilo kundi sawa ni hatari lkn kwakuwa tayari analijua tayari limeanza kusambaratika na wengine kurudi kwao rwanda.
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,233
2,000
Kusema za ukweli, tangu Wakenya walivyozuiliwa kuajiriwa kwenye mahoteli hapa Tanzania (esp kwenye eneo la waiters & waitresses) customer service kwenye mahoteli husika imeporomoka vibaya sana. Uswahili mtupu na nyodo kibao ndivyo vimetamalaki!
 

mapololo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
313
500
Binafsi naona niwakati mzuri sasa chadema wakicheza vizuri na kumsimamisha mgombea mzuri anaye kubalika Kama alivyo kubalikaga doctor slaaa 2025 wanachukua nchi asubuhi kweupeeeee,
Nasema hivi kwasababu kuu mbili,(1)Kanda ya ziwa kipindi Cha doctor ndiyo ilikuwa ngome kuu ya chadema na kiuhakisia ndiyo yenye watu wengi zaidi Tz,
2)Mpaka Sasa hivi Kuna zaidi ya mpasuko chama tawaka, yapo makundi zaidi ya Matatu Jambo ambalo naamini wote watawapigia Kira upinzani.
3)Yalisha tabiriwa na baba wa Taifa kuwa CCM isipo fanya vzr mwisho wake n 2020,
My take"Chadema muda ndiyo huu, utumieni vzuri"
 

wax

JF-Expert Member
Jun 14, 2015
5,557
2,000
Uuuuwwiiiiiiii uuuuwwiiiiiiii
Hichi kikundi cha kihuni ni cha kusarambatisha

Waungwana hawa wahuni tuwapinge kwa nguvu zote ni hatar Sana
 

Fahari

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,012
2,000
Swala la vibali vya kazi nisahihi vitolewe kwa kadri vinavyohitajika bila urasimu.Kama watanzania hawana skills zinazotakiwa katika kazi husika acha watu wengine wachukue hizo kazi,umezungumzia customer care,ni nani hajui kwamba watanzania tunafanya VIBAYA eneo hilo? Watanzania hatujui customer care,acha waletwe kutoka kokote duniani.
Kuhusu wamachinga,hali iliyopo haikubariki.Kila barabara "imevamiwa" na wachuuzi wamepanga bidhaa hadi barabarani,hii sio sahihi.Nadhani watu wawezeshwe na kushauriwa kurudi vijijini kufanya shughuli za kuzalisha mali kuliko kuwapumbaza na shughuli za uchuuzi mijini ambazo hazina tija endelevu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom