#COVID19 Angalizo: Polisi wasipochukua tahadhari tutaanza kushuhudia vifo mahabusu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwa namna tunavyoambiwa covid ipo na kwa ukweli kwamba binadamu ndiye kiumbe Mwenye risk yakupata huu ugonjwa na kwa kuzingatia kamatakamata isilo na legal facts inayoendelea upo uwezekano tukashuhudia wafuasi wa vyama vya siasa wakifariki au mahabusu wengine wakifariki Jambo ambalo siamini kama ndugu zetu polisi watabaki salama. Mfumo ulivyokaa hakuna wakumtetea mwenzake na hakuna mwenye hati miliki na kesho yake hivyo mtetezi wako wa leo ni mtumbuliwa wa kesho.

Tunaweza tukadhani Hali inayoendelea Sasa hivi yakamata kamata imesanifiwa vizuri na wataalam wa security lakini tukasau kwamba nafsi moja inayopotea mikononi mwa dola ulia for years. Mfano mzuri ni akwilina innocent lady who was fighting for future but suddenly she was killed without any sababu, unaamini aliyehusika na kifo kile huko alipo ana amani? Kama ana watoto unaamini watakwepa adhabu ya kosa la mzazi wao? Mahakamani it's fine itakuachia huru, RPC atakulinda lakini uhai wa mtu siyo baina ya RPC na Mungu wala wewe na favour ya Mahakama. Uhai wa mtu ni baina ya Mungu na wanadamu walioshiriki.

Nimejaribu tu kuwakumbusha kwamba amkula kiapo chakupambana na Watanzania wasio na hatia, may be mateso ya 2015-2020 waliyopata watu nchini ndiyo yaliyopelekea vifo vinavyotokea Sasa nchini vikihusisha waliopewa dhamana yakusimamia nafsi zetu hapa nchini ( who knows). Farao alipata mapigo mengi akiwa hai lakini hakubadilika, yamkini na viongozi wetu wanatwaliwa ikiwa ni ishara kwamba wanaobaki wasipochukua taadhari may be huko tuelekeako yatatupata mabaya zaidi.

Ni vigumu kuamini kama wanaoongooza nchi huu ndio upeo wao au Kuna namna shetani amewamiliki, tunapoteza viongozi hata kuzika hatujazika jamaa na marafiki wameshamsau then tunaamini tupo normal? Tunalo jukumu lakuomba viongozi wa kweli wa dini watuombee msamaha. Giza Ni kubwa Sana, Polisi unakaa na binadamu siku 78 bila kesi ya msingi, unakaa na mtu mwenye full address 7 dys bila charge, unakaa na viongozi wa kisiasa 14dys then unawaachia na mnaamini Hali ipo shwari?

Kwamba mfumo mzima wa serikali pamoja na covid hatujaona Kama Hawa watu tunawasubject kwenye risks za magonjwa, nchi yangu madaraka yamekuwa matamu kuliko nafsi za watu. Waambukizane magonjwa ndo furaha yenu? Mungu aishiye anaweza akawatendea miujiza wakaishi lakini wale waliokabidhiwa ving'ora na sanitizer, na masks na kila aina ya mbinu wakatwaliwa. Niwatie moyo ndugu mlio na watuhumiwa wasio na hatia mahabusu, Mungu atawalinda na watatoka salama.
 
Back
Top Bottom