ANGALIZO: NECTA, mnahujumiwa na maafisa elimu. Badilisheni mfumo wa kuwapata wasimamizi wamitihani

Honest One

JF-Expert Member
May 12, 2017
235
274
Kwa kweli nia ya dhati ya mheshimiwa Rais ya kunyoosha nchi inahujumiwa sana na watendaji wake. Leo napenda kuonesha madhaifu ya NECTA kutokana uzoefu wangu.

i) Usimamizi wa vituo vya mitihani umegeuka kuwa madili ya maafisa elimu na wafanyakazi wa halmashauri. Wasimamizi wanapatikana kwa kujuana,rushwa ya pesa na ngono. Shule za binafsi wanajichagulia kabisa wa kusimamia vituo vyao(hapo mtajua nini huwa kinafanyika). Ukitilitimba ni mkubwa sana hapa

ii)Usahishaji wa mitihani ya kidato cha pili yanayofanyika ni yaleyale lakini kibaya zaidi hadi wafanyakazi wasio walimu wanasahisha mitihani kama vile masekretari. Hii imetokea hapa Biharamulo ndo mitihani ya kidato cha pili ya mkuo wa Kagera iliposahihishiwa.


Ni ngumu sana kwa Mh. Rais kusafisha nchi hii. Hivyo basi NECTA badilisheni namna ya kuwapata hawa wasimamizi na wasahihishaji mitihani ya taifa,mnachezewa michezo michafu sana. Mitihani inaibiwa kama kawaida pia.
 
NECTA wange design electronic system ya kuwachagua wasimamizi na wasahihishaji kutoka kwenye database maalumu
 
Back
Top Bottom