Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,592
- 29,712
Ninaandika kwa lugha nyepesi pia rahisi kueleweka.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 ni kipimo muhimu sana kwa kukubalika kwa chama/ viongozi wa Chama kwa wananchi. Kuna mambo muhimu CCM inapaswa kuangalia kama tathmini ya kukubalika kwake hivi sasa
1. Mwitikio wa wapiga kura
Pamoja na hamasisho kutoka kwa viongozi wa kitaifa lakini mwitikio wa wapiga kura umekuwa chini ya asilimia 10. Wengi waliojitokeza ni wale essential staff ambao wapo accountable hata kama nafsi haitaki.
2. Ukimya wa vyama shindani
Ilitarajiwa labda kungekuwa na vurugu hapa na pale wakati wa uchaguzi lakini vyama vya upinzani waliwaasa wanachama na wafuasi wao kuwa na utulivu wasubiri tamko la viongozi wao. Hii ni dalili kwamba kuna jambo linapikwa ambalo linaweza kuathiri siasa za CCM na si serikali.
3. Kukubalika kwa washindi
Kuanzia ndani ya chama, mchakato wa uteuzi umeacha majeraha na kutokuwa na mshikamano kwa wanachama ambao wanaamini uteuzi uligubikwa na sintofahamu na mbinumbinu nyingi hivyo baadhi ya wagombea hawakubaliki na wengi ndani ya chama, pia wengi kutokubalika kwa wananchi.
4. Upinzani ndani ya CCM kuongezeka
Makundi yaliyoasisiwa na hasa kielekea 2020, kutasababisha athari kubwa kwenye kujenga mshikamano ndani ya chama hivyo kupelekea neema upande wa vyama pinzani ambapo makundi yatakayoathirika wataunga mkono upinzani ushinde maeneo mengi na nafasi za juu.
5. Misaada / mikopo kupungua.
Nchi wahisani wanatumia Demokrasia kama kigezo kikuu cha kutoa misaada au mikopo hiyo. Huwezi kukwepa kigezo cha ukuaji wa demokrasia unapoomba support kutoka kwa mabeberu. Hivyo tunaweza kama nchi kuanza kubanwa kwenye miradi mikubwa na serikali kukwama kuendeleza miradi hiyo kwa kukosa misaada au mikopo hiyo.
6. Fallen Angels (mwenye akili na afahamu)
Mabeberu wanaweza kuongeza espionage activities ili kusaidia makundi ayanayoweza kuathiri mshikamano wa nchi kwa maslahi ya mabeberu hivyo tunakuwa hatarini kama.nchi kwani vyombo vya mabeberu vikianza kutushughulikia tutakiwa na wakati mgumu sana. Wanazo media na tools za kuwasaidia...
Nimetoa maoni kwa lugha rahisi.
Je wewe mwanaJF mwenzangu una maoni gani ya kuongezea?