Angalizo muhimu kuhusu uteuzi wa Dr. Magufuli wizara ya ujenzi

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
826
Wiki hii ilikuwa tena wiki ya vicheko kwa watanzania, wakiwa na matumaini mapya kwa mpambanaji aliyerejea tena wizara ya ujenzi kujenga mabarabara toka Mtwara hadi bukoba ili siku moja mtanzania aweze kusafiri na gari dogo tola Mtwara hadi Bukoba. Bahati nzuri mpambanaji huyu anarudi wizarani hapao wakati bado takribani km 100 tu barabara zinazoitaji lami ahadi hiyo itimie.

Barabara izo ni ile inayotoka Somanga karibu na daraja la Mkapa hadi karibu na Nangurukuru huko Lindi (km 60), na mkiwa huko Singida kama km30 na ushee. Ni vema tunaomfahamu Magufuli tukawapa watanzania angalizo mapema, kuwa wasitegemee mengi kwa mtu huyu ambaye ni mojawapo ya haambiliki wa hapa Tanzania

Magufuli ni mojawapo ya mawaziri wachache ambao mpaka leo hajaweka msimamo wake wazi wazi kama yupo nasi au yupo na mafisadi, wakati akina Sitta na wengine wakipigana bila kuangalia maslahi yao yeye hatujui yuko wapi, leo na akina Lowasa, kesho na Kikwete na pengine mwisho kabisa kama mpambanaji dhidi ya wazembe serikalini.

Maamuzi mengine ya Magufuli yamelitumbukiza taifa katika hasara kubwa kama lile la uvuvi haramu, taifa limelipa mabilioni kama gharama za kuhifadhi samaki wale na haijulikani nini mastakabali wetu kuhusu kesi ile ya wavuvi haramu.

Alipokuwa wizarani hapo ujenzi alikuwa ni mtu asiyeshaurika, yeye na media kila wakati pasipo stahili

Baadhi ya maamuzi tata yaliyogharimu taifa ni kuhusu lile la kuuza nyumba za serikali, ambalo hata leo taifa linajutuia. upo ukweli kuwa alihusika kugawa nyumba hizo hata kwa vimada wake jambo amballo linatilia shaka uadilifu wake.

Kubwa zaidi ni ile rushwa aliyokuwa akipewa kupitia taasisi nyeti kama SUMA JKT, upo ushahidi wa kimazingira kuwa mara nyingi alipindisha maamuzi ya bodi za zabuni ili kuwapa wabia wake suma jkt kazi. mojawapo ni zile nyumba za seriakali za Mbweni ambazo nyie ni mashahidi kuhusu uozo ule mtupu. Inasemekana kuwa yeye huwa Salamakulla mlungula kupitia taasisi nyeti kama hizi na hilo amekuwa akitamba wazi wazi, labda ndo maana mafisadi wenzake akina Masha nao wakajifanya kuwa usalama wa taifa katika ule wizi wa EPA na green.

Magufuli ni mbinafsi wa kutupa, na hili linadhihirisha jinsi alivyokuwa tayari kushinikiza makao makuu ya mkoa mpya wa Geita kupelekwa wilayani kwake chato. naambiwa kuwa aliwahi kupindisha miradi ya kitaifa ya barabara ipite wilayani kwake Chato, na kama haitoshi aliwahi hata kulazimisha national housing wajenge nyumba zao huko Chato bila kuzingatia maslahi ya kibiashara

HUYU NI MAGUFULI, NAANDIKA HAYA LEO LAKINI ANGALIZO KUU NI KUWA WATANZNIA MSITEGEMEE TIJA TOKA KWA HUYU MTU, ILA UKASUKU WA KUKARIRI UREFU WA BARABARA
 
unampaka matope ili asifanye kazi kwa ufasaha unaonekana wewe ni mongo mtupu,angekuwa rais angevutia kwa watanzania kama anavyojitahidi kuritumikia njimbo lake ipasavyo,makufuli ni mchapa kazi.sio kama we unaka kuchonga tu hapa,
 
Huyu Magufuli tusimfanye malaika, kuna watu hapa kila tuhuma dhdhi ya Magufuli wanaikataa na kuita watoaji wazushi. Ingekuwa ni tuhuma kuhusu watu wengine mngeshangilia. Mi sijaona uadilifu wa Magufuli. Magufuli ni kama Mrema, wao wanatumia vyombo vya habari, kujitangaza huku nyuma wanaiba. Huyu Magufulu hatutakaa tumsamehe kwa kuuza nyumba za serikali kwa vigogo. Nyumba ya Masaki yenye thamani ya Tshs 500m inauziwa kigogo kwa Tshs 3m na kwa mkopo wa miaka kumi. Kama angekua muadilfu, angepinga. Na kama tunavyojua, maamuzi yanafanywa na baraza la mawaziri na kama unapinga jiuzulu, hakuna uadilifu wowote. Sina chuki binafsi nae ila nachukia watu wanapomgeuza malaika, kwa kuwa tuu anajua kutumia vyombo vya habari kwa kuuma na kupuliza
 
unampaka matope ili asifanye kazi kwa ufasaha unaonekana wewe ni mongo mtupu,angekuwa rais angevutia kwa watanzania kama anavyojitahidi kuritumikia njimbo lake ipasavyo,makufuli ni mchapa kazi.sio kama we unaka kuchonga tu hapa,
It is true mkuu. Mbona yeye haelezi alichowafanyia watanyania ktk nafasi aliyonayo
 
wiki hii ilikuwa tena wiki ya vicheko kwa watanzania, wakiwa na matumaini mapya kwa mpambanaji aliyerejea tena wizara ya ujenzi kujenga mabarabara toka mtwara hadi bukoba ili siku moja mtanzania aweze kusafiri na gari dogo tola mtwara hadi bukoba. bahati nzuri mpambanaji huyu anarudi wizarani hapao wakati bado takribani km 100 tu barabara zinazoitaji lami ahadi hiyo itimie. barabara izo ni ile inayotoka somanga
karibu na daraja la mkapa hadi karibu na nangurukuru huko lindi (km 60), na mkiwa huko singida kama km30 na ushee.
ni vema tunaomfahamu magufuli tukawapa watanzania angalizo mapema, kuwa wasitegemee mengi kwa mtu huyu ambaye ni mojawapo ya haambilikis wa hapa tanzania

magufuli ni mojawapo ya mawaziri wachache ambao mpaka leo hajaweka msimamo wake wazi wazi kama yupo nasi au yupo na mafisadi, wakati akina sita na wengine wakipigana bila kuangalia maslahi yao yeye hatujui yuko wapi, leo na akina lowasa, kesho na kikwete na pengine mwisho kabisa kama mpambanaji dhidi ya wazembe serikalini.
maamuzi mengine ya maguufuli yamelitumbukiza taifa katika hasara kubwa kama lile la uvuvi haramu, taifa limelipa mabilioni kama gharama za kuhifadhi samaki wale na haijulikani nini mastakabali wetu kuhusu kesi ile ya wavuvi haramu.

alipokuwa wizarani hapo ujenzi alikuwa ni mtu asiyeshaurika, yeye na media kila wakati pasipo stahili

baadhi ya maamuzi tata yaliyogharimu taifa ni kuhusu lile la kuuza nyumba za serikali, ambalo hata leo taifa linajutuia. upo ukweli kuwa alihusika kugawa nyumba hizo hata kwa vimada wake jambo amballo linatilia shaka uadilifu wake.

kubwa zaidi ni ile rushwa aliyokuwa akipewa kupitia taasisi nyeti kama SUMA JKT, upo ushahidi wa kimazingira kuwa mara nyingi alipindisha maamuzi ya bodi za zabuni ili kuwapa wabia wake suma jkt kazi. mojawapo ni zile nyumba za seriakali za mbweni ambazo nyie ni mashahidi kuhusu uozo ule mtupu.inasemekana kuwa yeye huwa salamakulla mlungula kupitia taasisi nyeti kama hizi na hilo amekuwa akitamba wazi wazi, labda ndo maana mafisadi wenzake akina masha nao wakajifanya kuwa usalama wa taifa katika ule wizi wa epa na green ...

magufuli ni mbinafsi wa kutupa, na hili linadhihirisha jinsi alivyokuwa tayari kushinikiza makao makuu ya mkoa mpya wa geita kupelekwa wilayani kwake chato. naambiwa kuwa aliwahi kupindisha miradi ya kitaifa ya barabara ipite wilayani kwake chato, na kama haitoshi aliwahi hata kulazimisha national housing wajenge nyumba zao huko chato bila kuzingatia maslahi ya kibiashara

HUYU NI MAGUFULI, NAANDIKA HAYA LEO LAKINI ANGALIZO KUU NI KUWA WATANZNIA MSITEGEMEE TIJA TOKA KWA HUYU MTU, ILA UKASUKU WA KUKARIRI UREFU WA BARABARA

Kila mwanadamu anaudhaifu wake, viongozi wengi wamefanya mambo kwa kuangalia nafsi zao kwanza. Kuna PM mmoja alisomba nguzo za umeme kutoka Morogoro na kuzipeleka kwake, huyo huyo alilazimisha NHC kujenga nyumba ktk makao ya wilaya yake ambayo alilazimisha imegwe toka wilaya ya jirani, bado akalazimisha wilaya hiyo ndogo iwe na ofisi za NSSF enzi hizoooo.

Vipi na huyu aliyetaka kulazimisha Uwanja wa ndege Arusha, au aliyehamisha uamuzi wa kuipa Mby Tech hadhi ya chuo kikuu na kupeleka Arusha? Kama barabara ilipita Chato na Chato kuna Watz,kuna ubaya gani. Tukichimba sana udhaifu wa mtu hatutapata mtu hata mmoja.
 
Kila mtu ana udhaifu wake

kama mgufuli aliye pewa sifa enzi za mkapa alikuwa na mapungufu 50 basi kwenye utawala wa kikwete mgufuli ana zaidi ya 150.

Though I admire Magufuli am sure he will not be the same magufuli of Mkapa's era. Siasa za maji taka na mtandao zimemchfua kuliko uchafu wake halisi.
 
watanzania ndivyo tulivyo!TUNASIFIA WEEEEH,tukiulizwa tunasifia kwa lipi tunakuwa wakali.hakuna MTU ALIYEPENDWA HII NCHI KAMA KIKWETE.leo hii yako wapi?!Kama mtu amekuwa mbunge,waziri ndani ya CCM kwa miaka zaidi ya kumi HE IS NOT CLEAN AT ALL.only a fool would think that.
MAGUFULI is just a famous politician posing as capable and clean.If he is indeed,he should have nothing to do with CCM.
 
Mhh hakiwezi kikakubalika kila kitu anachofanya magufuri kumbuka yule ni binadamu kama wewe vile hatuna viongozi wengiwazuri safiiiiiiiii kivile kama uonavyo malaika ila ukweli magufuri anajitaidi pita wizara zote alizopita zile rushwa rushwa zinakuwa zinakoma na watu wengi akishafika wanajua hakuna kula tena sasa wbongo hampendi
 
Watanzania ni kusifiana na kupongezana tuu. Nawashangaa wanaomtetea huyu Magufuli kama vile ye malaika. Kinachonifurahisha inapokuja kwa Magufuli wanasema kila binadamu ana upungufu wake, mbona ikija suala la Lowassa, na mafisadi wenzake hamsemi kila mtu ana udhaifu, acheni hoja za kijinga.Huyu Magufuli yupo kwenye mtandao wa CCM, atabadili mbinu tuu kwa kukaririr barabara na kusema sana ila mwishowe ni kuwa rudisha nyumba za serikali mlizouziana nyie vigogo.
 
Tutake tusitake Dr. Magufuli ni mtendaji anayepaswa kuheshimika na kila mtanzania kwa kazi alizolifanyia taifa hili, hivyo vingine ni vitu vya kawaida kwa binadamu. Mkwete anajenga Ikulu msoga, NHC wamejenga nyumba chalinze ambazo hata hazina wakazi bado hatulioni hilo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
Mwikimbi,
Kama kawaida ya nyimbo za Rap, yabidi mengine tuelewe mazingira yako kabla ya kukubali unayoyasema. Ni mengi yasiyofaa toka kwa Magufuli ambaye ni sehemu ya CCM. Ni kawaida yao. Lakini wewe umeaandika kama wakili wa shetani wa Vatican. Hukuwa na haja ya lolote jema alilofanya.

Kweli hata la samaki unalitaja zima zima kama Rostam aliyeguswa? Tangu lini kesi zikaamuliwa kwa kufuata thamani ya fedha? Kweli kumfunga kibaka wa kariakoo unaweza ukaieleza kuwa na thamani gani!

Naona kama kurudi kwa magufuli wizara hiyo inayoeleweka kwa rushwa, imekuwa kama mshale wa sumu kwa watumishi wa wizara. Kwa nini?
 
Mbuzi hulia chakula pale alipofungiwa hili utake usitake hata ukipewa wewe utatafuna tu. Cha muhimu hata km anatafuna lakini mambo kimaendeleo yanaonekana wazi wazi na hayo ndio tunataka.

Ipo mifano mingi midogo midogo tu ya kimaisha ambayo tunaona hata ktk michango midogo midogo tunaona, mfano michango ya harusi, watu wanaramba kiasi, lakini harusi zinafana vile vile.
Au mfano mama anapewa pesa ya matumizi ya ndani kwa chakula, lakini yeye anapindisha bajeti na kwenda kununua vitu vyake binafsi.
Au, mwanafunzi anapewa nauli na mzazi wake, lakini yeye anaamua kutembea na kutumia pesa aliyopewa kwa matumizi mengine . n,k

sasa hapa nataka kusema kuwa vijitabia hivi havijaanzia ukubwani, tangu utotoni na ndiyo tunashuhudia kila pahala kuna udanganyifu.

tatizo ni pale unapuvuka kiwango cha kulitia hasara taifa. yaani ukosefu wa maadili unaozungumziwa umetokanana na tabia ya mtu tangu akiwa mtoto hali ambayo imeendelezwa hadi ukubwani

tuangalie maendeleo, tukitaka kiongozi ambaye hatafuni hata senti moja labda tutafute malaika waje kutuongoza, jambo ambalo haliwezekani.
 
wiki hii ilikuwa tena wiki ya vicheko kwa watanzania, wakiwa na matumaini mapya kwa mpambanaji aliyerejea tena wizara ya ujenzi kujenga mabarabara toka mtwara hadi bukoba ili siku moja mtanzania aweze kusafiri na gari dogo tola mtwara hadi bukoba. bahati nzuri mpambanaji huyu anarudi wizarani hapao wakati bado takribani km 100 tu barabara zinazoitaji lami ahadi hiyo itimie. barabara izo ni ile inayotoka somanga
karibu na daraja la mkapa hadi karibu na nangurukuru huko lindi (km 60), na mkiwa huko singida kama km30 na ushee.
ni vema tunaomfahamu magufuli tukawapa watanzania angalizo mapema, kuwa wasitegemee mengi kwa mtu huyu ambaye ni mojawapo ya haambilikis wa hapa tanzania

magufuli ni mojawapo ya mawaziri wachache ambao mpaka leo hajaweka msimamo wake wazi wazi kama yupo nasi au yupo na mafisadi, wakati akina sita na wengine wakipigana bila kuangalia maslahi yao yeye hatujui yuko wapi, leo na akina lowasa, kesho na kikwete na pengine mwisho kabisa kama mpambanaji dhidi ya wazembe serikalini.
maamuzi mengine ya maguufuli yamelitumbukiza taifa katika hasara kubwa kama lile la uvuvi haramu, taifa limelipa mabilioni kama gharama za kuhifadhi samaki wale na haijulikani nini mastakabali wetu kuhusu kesi ile ya wavuvi haramu.

alipokuwa wizarani hapo ujenzi alikuwa ni mtu asiyeshaurika, yeye na media kila wakati pasipo stahili

baadhi ya maamuzi tata yaliyogharimu taifa ni kuhusu lile la kuuza nyumba za serikali, ambalo hata leo taifa linajutuia. upo ukweli kuwa alihusika kugawa nyumba hizo hata kwa vimada wake jambo amballo linatilia shaka uadilifu wake.

kubwa zaidi ni ile rushwa aliyokuwa akipewa kupitia taasisi nyeti kama SUMA JKT, upo ushahidi wa kimazingira kuwa mara nyingi alipindisha maamuzi ya bodi za zabuni ili kuwapa wabia wake suma jkt kazi. mojawapo ni zile nyumba za seriakali za mbweni ambazo nyie ni mashahidi kuhusu uozo ule mtupu.inasemekana kuwa yeye huwa salamakulla mlungula kupitia taasisi nyeti kama hizi na hilo amekuwa akitamba wazi wazi, labda ndo maana mafisadi wenzake akina masha nao wakajifanya kuwa usalama wa taifa katika ule wizi wa epa na green ...

magufuli ni mbinafsi wa kutupa, na hili linadhihirisha jinsi alivyokuwa tayari kushinikiza makao makuu ya mkoa mpya wa geita kupelekwa wilayani kwake chato. naambiwa kuwa aliwahi kupindisha miradi ya kitaifa ya barabara ipite wilayani kwake chato, na kama haitoshi aliwahi hata kulazimisha national housing wajenge nyumba zao huko chato bila kuzingatia maslahi ya kibiashara

HUYU NI MAGUFULI, NAANDIKA HAYA LEO LAKINI ANGALIZO KUU NI KUWA WATANZNIA MSITEGEMEE TIJA TOKA KWA HUYU MTU, ILA UKASUKU WA KUKARIRI UREFU WA BARABARA

Hebu tupe reference basi......................watu wanapomsifia Magufuli huwa wanalinganisha na utendaji wa waheshimiwa wengine waliopita Wizara hiyo ya Ujenzi................NB: sisemi kuwa ni better devil.....isipokuwa ni lazima tukubali kuwa........Magufuli ni mchapa kazi na ni moja ya nguzo muhimu sana kwa Majambazi CCM............

Pili ni lazima utambue kuwa Magufuli amefika hapo alipo kupitia Majambazi CCM.....serikali ni ya CCM maamuzi yake yanafuata sera za majambazi CCM..........

Juzi tumeona Mh Zitto akielezea tofauti zake na kitendo cha "walk out" from Chadema.................kwa hiyo Zitto aondoke CDM na ajiuzulu nafasi zake za uongozi!!.............

Hivi jamani tunaelewa maana ya neno Demokrasia kweli............?
 
Tutake tusitake Dr. Magufuli ni mtendaji anayepaswa kuheshimika na kila mtanzania kwa kazi alizolifanyia taifa hili, hivyo vingine ni vitu vya kawaida kwa binadamu. Mkwete anajenga Ikulu msoga, NHC wamejenga nyumba chalinze ambazo hata hazina wakazi bado hatulioni hilo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
aliyejenga nyumba za national housing pale chalinze ni magufuli katika harajati zake za kujikomba kw akikwete. yetu macho, nawapa miezi sita kila mmoja wenu atamchoka magufuli
 
Mi hata muongee nini, sintauona ubora wa Magufuli mpaka atapoomba radhi ya kugawana nyumba za serikali
 
Mi hata muongee nini, sintauona ubora wa Magufuli mpaka atapoomba radhi ya kugawana nyumba za serikali

Ndani ya CCM kama kuna aliye msafi na awe wakwanza kumtupimwenzake jiwe! ""MAGUFULI SIO MALAIKA!! kila mwaCCM anauzaifu wake, tumwache tuone anawafanyia nini watazanzania kwa muhula huu wa lala salama.:smiling:
 
Kama John Pombe Magufuli si msafi basi kwa kzazi hiki hakuna wa kumfikia katika wote walio CCM. Ni busara tu kutambua hakuna mwanadamu aliyemkamlifu. lakini napenda kusema Magufuli ameonyesha uzalendo kila Wizara anapofanya kazi. Hata pale anapoanguka mimi hua nampongeza kwa kuwa anadhamira safi. Hongera magufuli.
 
Back
Top Bottom