Angalizo kwa wanaume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo kwa wanaume

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by sweetdada, Oct 17, 2012.

 1. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wanaume mnapaswa kuwapenda wake/wapenzi zenu pindi wanapokuwa wajawazito. Mwanamke mjamzito anahitaji upendo na ukaribu kutoka kwako maana anapitia hormonal changes nyingi ambazo hajawahi kuzipitia hiyo tu ni kazi tosha haitaji mapichapicha kutoka kwako.kuna mijianaume mingine ina roho chachuu sijawahi ona.

  Nimeleta mada hii hapa kwasababu kuna jirani yangu ni mjamzito wa miezi kama mitano hivi ila huyo mume sasa ni balaa, hataki kuongozana na mkewe,hataki kuguswa na mkewe,alishasitisha huduma ya unyumba tangu ana miezi mitatu,kila anapomuangalia anamwmabia "yani umekuwa mbaya hata huvutii" kisa kanenepa. mwanamke anashinda kulia tu.

  Jamani pendeni wake/wapenzi wenu wakiwa wajawazito.mtoto unataka afu unaleta zako, ulivyoingiza hiyo mimba ulidhani nini EBOO!!
   
 2. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Duh, mwanamme kama huyu kama mie ataishia na huyo huyo,tena hilo ndio GUME GUME kwanza nasikia mwanamke akiwa na mimba anakua mtamu kama nn huyo hajui ladha ya mwanamke anajitia kundini tuu....
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,332
  Likes Received: 2,636
  Trophy Points: 280
  Ukipenda boga inapaswa upende na ua lake...asante kwa angalizo...
   
 4. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  100% nakubaliana na ushauri, kwani ni vema kumwonesha upendo uliopindukia
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  kuna mtu aliwahi kuleta hizo habari hapa!
  ndo haya matatizo ya kuona kwa kuangalia sura!
   
 6. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Aaaaaaaaaahaswa
   
 7. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,472
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Mimi nilijifuza somo zuri kwa ticha mmoja. Hakuwa mwema sana wala mbaya sana kwa mkewe. Alikuwa na manyanyaso ya rejareja kwa mkewe lakini sio wakati wa ujauzito! Mkewe akiwa na mimba mume anaanza upya kumtongoza! Yaani anambembeleza, anamsaidia kazi, anawahi kurudi nyumbani, anatembea naye taratibu barabarani, anachat naye wanacheka, anamwambia jinsi anavyompenda,nk. Yaani hadi raha! Hapo anaweza kuzaliwa mtoto njiti kweli? Sidhani, LOL!
  Kwa hiyo wale wanaonyanyasa na kunyanyapaa wake zao wajawazito bila shaka wana ufinyu wa fikra na hawana upendo kwa wake zao. Wakati wa kuwa karibu wao ndio wanakuwa mbali. Hata ugonjwa ni hivyo hivyo wanawatelekeza.
   
 8. S

  Solarpanel JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ama kwa hakika Coral,hatok njiti ,unapata bongee haswa,
   
Loading...