Angalizo kwa Serikali ya awamu ya sita na CCM: Kustawi kwa awamu ya sita na CCM

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Kwanza nimshukuru Mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kuilinda nchi yetu

Naomba ieleweke hivi kila serikali iliyoko madarakani imechaguliwa na wananchi baada ya kuinadi ilani ya chama husika. Mwaka huu tunaomaliza nchi ilipitia kipindi kigumu sana kwa kuondokewa na Rais aliyechaguliwa na wananchi.Tushukuru katiba yetu pamoja na mapungufu yaliyopo iliweza kutuvusha salama. Rais aliyepo kulingana na katiba yetu indirectly ni yule aliyechaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura( labda kama makamu wa rais angekuwa anachaguliwa kivingine) .

Awamu ya sita kulingana na katiba ya JMT,ni mwendelezo wa awamu ya tano.ndiyo maana ,wabunge ni wale wale wa awamu ya tano, na mawaziri ukiondoa wale waliyochaguliwa na rais ( eg .waziri wa ulinzi) ni wale wale wa awamu ya tano waliyochaguliwa kihalali na wananchi kwa njia ya sanduku la kura.Hivyo ni vigumu sana kuitenganisha awamu ya tano na ya sita.Hili nina uhakika nalo na ndiyo maana hata hotuba za mwanzo za Mh Rais SSH ,alisema mwenyewe kuwa yeye na Hayati Magufuli ni kitu kimoja.labda kama alikuwa anadanganya.

Ustawi wa awamu ya sita na CCM kwa ujumla unategemea umoja imara kati ya watu waliyohudumu awamu ya tano( hawa ndiyo wenye ilani ya uchaguzi) na wanaohudumu awamu ya sita ( kwa njia ya katiba ya JMT).Ukiwatenganisha hawa watu unaleta mpasuko mkubwa na kusababisha ugumu wa kuistawisha awamu ya sita,maana kwa vyovyote vile awamu ya sita mizizi yake ni awamu ya tano.

Nimekuwa nikiona ushauri mwingi ukitolewa kwa Rais wetu mpendwa ati aachane na watu wa Magufuli( awamu ya tano) achaguwe wa kwake.ushauri huu ni wa hovyo sana.labda niwatahadharishe kuwa watu wa Magufuli siyo wa sukuma ( sukuma gung) kama mnavyotaka kuwaminisha watu .Mnaposema achague wa kwake mnataka awapate wapi? Wale kumi wa kuteuliwa na rais. OK.afanye hivyo.lakini ......

Chanjo ya corona imekuwa ikitolewa kwa kusuhasuha kwa sababu ya makosa yaliyofanywa na waziri baada ya kushindwa kuwaunganisha watu wa Magufuli na watu kwa rais Samia.na serikali ya awamu ya sita na CCM kwa ujumla itafeli vibaya ikiwa itashindwa kuwaunganisha watu wa awamu ya tano na ya sita. Awamu ya sita haiwezi kusavaivu bila watu awamu ya tano.hilo tusahau.

Nimemwona mh Rais akilalamika kuwa kuna watu ndani ya serikali wanafanya mambo ya hovyo na baadaye wanasema eti awamu ya sita inaleta mambo ya hovyo.Mambo ya hovyo yamesababishwa na awamu za nyuma then awamu ya sita inaangushiwa gari bovu.maneno haya yanatafakarisha sana.Ikiwa gari bovu ni awamu ya tano,hapa mama anakosea.

Yeye amehudumu awamu ya tano.mtasema alikuwa hasikilizwi.sawa. kama ni hivyo alishindwa kujiuzulu? Sikatai kuwa awamu ya tano walikuwepo watu wa hovyo.walikuwepo sana tu tena wengine walikuwa wanamuangusha hayati JPM na pengine walimshauri vibaya.tunaona mfano wengine wako gerezani.

Kinachotakiwa ni kuwa makini katika kuyarekebisha mambo ya hovyo yaliyojitokeza awamu ya tano.mfano ,ziko tetesi kwamba eti kulikuwepo uvunjifu wa katiba,mama arekebishe hapa.ziko tuhuma kuwa watu walikuwa wanabambikiziwa kesi,basi Mama asifanye hivyo.Tuhuma za kwamba kuna watu wanatekwa,kama ni kweli Mama asifanye hivyo.Mikutano ya vyama iruhusiwe kwa utaratibu mzuri.

Sasa tumeona mambo mengine mazuri yaliyofanywa na awamu ya tano yakiachwa kabisa .mifano iko mingi .Kipindi cha awamu ya tano,mwananchi akiingia ofisi ya umma alionekana bosi lakini hali hii inaanza kupotea.sasa hivi huko barabarani rushwa imeanza kutapakaa etc

Mama akitaka kufanikiwa sana na kuipaisha CCM afanye haya

1.Fuata ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.
2.Malizia miradi yote ikiyoanzishwa na awamu ya tano
3.Tusiwabugudhi watu wanaojiita watu wa Magufuli
4.Wasikilize wamachinga

5.Be careful kurekebisha Sera mbovu za awamu ya tano kwa sababu hata wewe ulikuwepo
Eg : swala la machinga,swala la watumishi hewa,swala la vyeti feki

6.Mradi wa bandari ya bagamoyo ,usubiri kwanza mpaka miradi mingine ikamilike.

7.Fanyia kazi mfumuko wa bei

8.Usifanye vita na watu wa Magufuli Bali wasikilize .utafanikiwa sana.kinyume chake utafeli sana na CCM kuaguka .
 
CCM ni ugoro mtupu hawana ridhaa ya wananchi bali walibaka na kunajisi mchakato mzima wa uchaguzi full stop.
 
Mama na Rais wetu hana namna zaidi ya kusema ukweli na ubovu wa mikataba aliyoikuta na ambayo haina maslahi kwa nchi .Tunajua kuna wahuni wanaoongozwa na Pole Pole kutaka kuamnisha watu kuwa kuna tawala ilikuwa ni takatifu wakati sio kweli .Mama tuko nyuma yako kwa hali yoyote ile.
 
Mama na Rais wetu hana namna zaidi ya kusema ukweli na ubovu wa mikataba aliyoikuta na ambayo haina maslahi kwa nchi .Tunajua kuna wahuni wanaoongozwa na Pole Pole kutaka kuamnisha watu kuwa kuna tawala ilikuwa ni takatifu wakati sio kweli .Mama tuko nyuma yako kwa hali yoyote ile.
Hapo tiari umeshakosea.mikataba mibovu wakati yeye alikuwa msaidizi wa Rais?acha uchonganishi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom