mgoloko
JF-Expert Member
- Jun 25, 2016
- 4,806
- 3,996
Nakupongeza Mkuu wa Mkoa Dar Bwana Paul C. Makonda kwa kupewa ekari 1500 kwa ajili ya uanzishwaji wa viwanda vidogovidogo.
Angalizo langu kwako, chunga sana usije kumwingiza Rais wetu kipenzi kwenye kashifa kubwa itakayoyumbisha nchi yetu. Soma ripoti ya CAG ya 2015/2016 juu ya kampuni hiyo iliyokupa ardhi kigamboni. Nasisitiza soma ripoti ile mkuu. Lakini usiishie hapo tu, soma sheria ya umiliki ardhi kwa mzawa na mgeni. Ukishindwa muone Waziri husika.
Usije kujikuta Mh Makonda unatumiwa kutakatisha haramu kuwa halali bila kujijua ama ukijua vema.
Na Yericko Nyerere
=======
Paul Makonda amekabidhiwa hekari 1500 za ardhi kujenga Viwanda “Dar es Salaam Industrial Area”.
Posted on February 21, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amekabidhiwa hekari 1500 za ardhi katika eneo la Lingati Kisarawe 2 Wilayani Kigamboni jijini Dsm litakalotumika kujenga Viwanda vidogo vidogo na vyakati litakalojulikana kama Dares salaam Industrial Area.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa hekari hizo na Mkurugenzi wa Azimio Estaste inayomiliki maeneo mengi ya Uwekezaji hususan Viwanda katika wilaya ya kigamboni Bw,Mohamed Iqbar amesema hekali hizo zitagawanywa katika makundi ya uwekezaji viwanda vidogo na vyakati,Ufugaji wa mifugo ikiwemo ng’ombe na mbuzi lakini pia kilimo.
Amesema baada ya kukamilika utaratibu wa Upimaji eneo hilo litatengwa katika makundi matano ambapo wajasilimali kutoka wilaya zote za jiji la dsm wenye nia ya kuwekeza watakabidhiwa maeneo hayo kwa utaratibu utakaopangwa.
Hata hivyo makonda ametoa tahadhari kwa wale wananchi wazalendo wanaojitolea kwa ajili ya jamii.
Mkurugenzi wa Azimio Estate inayomiliki maeneo hayo amesema ameamua kutoa ardhi hiyo kwa Mkuu huyo wa mkoa wa dsm kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais John Magufuri katika kuhakikisha tanzania inaelekea katika ujenzi wa viwanda.
Chanzo: Channel Ten
==========
.......New Updates.......
Lukuvi: Nitamchukulia hatua mfanyabiashara aliyempa Makonda ardhi kwa ajili ya Viwanda
Iqbar ni mtaalamu mkubwa wa dili chafu na ni mtu mjanja sana na akitoka nje ya TZ anajulikana kwa jina lingine sio hili tunalolijua sie