Angalizo kwa January na Mnyika kuh. Tanesco na Mgao wa Umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo kwa January na Mnyika kuh. Tanesco na Mgao wa Umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngaramu, Feb 16, 2011.

 1. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi ni mhandisi wa umeme niliewahi fanyakazi maeneo ya migodi. Kwa ufahamu wangu CHANZO CHA MGAO wa umeme ni migodi ya BUZWAGI na NORTH MARA. Migodi hii imeunganishwa kwenye grid ya taifa 2009/2010 bila kukamilika kwa mradi wa uwekezaji kwenye vyanzo kama mkataba/utaratibu ulivyotaka (ufisadi huu). Upungufu wa mvua ume-trigger tu hili tatizo. Kama hamuamini, toa LOAD ya hiyo migodi miwili muone! MY TAKE: KWA NINI WATZ WOTE TUBEBE MZIGO WA BARRICK GOLD?
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Duh!Kweli yawezekana???!!!!Kama nikweli kazi hipo kweli!!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  There is more to this mgao that what meets the eye. This means that the country economy is bleeding to please the interest of only one company. Only in tanzania
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sikuwahi kuwaza hili ... inawezekana
   
 5. k

  kayumba JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mhandisi ningeomba utuepe data kihandisi, hivi hiyo migodi inatumia MW ngapi?

  Angalizo:

  Matumizi ya umeme nchini yameongezeka sana, si kwenye migodi tu bali hata huku mijini. Majumba yameongezeka, viwanda vimeongezeka na bado mahitaji yanaongezeka. Mgao tutaendelea kuwa nao hata katika siku za usoni kama jitihada za makusudi hazitafanyika kuwa na umeme wa ziada.

  Ongezeko la mahitaji linakadiliwa kuwa 100MW kwa mwaka!
   
 6. n

  ngoko JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inawezekana Wabunge hawajui hii siri. hata hivyo walipaswa kuwa na plan ya kuwezesha kupatikana kwa umeme wa kutosha kutumika mpaka kwa wawekezaji hao.
   
 7. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ingawa sina takwimu kamili, lakini kuna ukweli ndani ya maelezo ya mtoa maada hata kama kachanganya na uwongo. Migodi ya dhahabu inatumia umeme mwingi sana. Binafsi mara yangu ya mwisho kufanya uchambuzi wa matumizi ya umeme kwenye mgodi mmoja [sitautaja hapa jamvini] ilikuwa zaidi ya 60MW. kipindi hicho huo mgodi haukuwa kwenye full swing. sijui migodi mingine lakini huo ni mmoja tu!. TAFAKARI KWA MIGODI YOTE. NA KWAMBA HIYO MIGODI IWE KWENYE MATUMIZI KWA 100%
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Makampuni yanayomiliki migodi yanachukua rasilimali zetu bure na tena tunawapa umeme ili watuibie na sisi tunalala giza, hatufanyi kazi kwa sababu hatuna nishati. Hivi kweli tunaviongozi? Mimi nasisitiza hawa watawala wetu wameasi nchi ni kazi yetu kuirudisha nchi yetu.
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kihandisi zaidi.

  endelea kutupatia siri mkuu. wengine wanajua TV ndo zinakula megawati (za Ngeleja, japo haelewi hata maana ya megawati)
   
 10. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du jamaa yangu naona una Data kamili, maana nimefuatilia link ya Tanesco kuhusu mgawo mkoa wa Mara sikuwaona hawa wachimbaji Barrick (Buzwagi au North Mara) katika hata mgawo naona wanapewa km wenzao katika mtaa wa 33KV
  Pia Power station kubwa km za Mtera, Zuzu (Dodoma), Morogoro Hale na Nyumba ya Mungu zina mita inayoonyesha umeme wote ulio-load katika Grid ya taifa hivyo wanaweza wasiliana na kuwanyima huko line ya Mwanza.
  Kuna mwana JF (Mwanamama) Mhandisi wa Tanesco akiiona hii thread anaweza tufungua Macho
  Km ni kweli bora Barricks waondoke maaha hata huo mrahaba hauisaidii Tanesco na Taifa
   
 11. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,972
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Caspian+Dowans= Danganyika(a.k.a shamba la Bibi)
   
 12. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tanesco nao si wanafanya biashara? Ni bora migodi ipate umeme ambao watalipa kwa wakati kuliko kuwapa wizara umeme ambao hawaulipii kwa wakati ingawaje jenereta zinajazwa mafuta kwa pesa taslim
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  wahandisi wa Ngeleja wako wapi? Au nao wamewekwa mfukoni kama boss wao?
   
 14. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh!!! you need to defend your post with technical datas, this is very interesting thread so dont get dissapeared
   
 15. b

  bulunga JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Barrick na Tanesco wana maktaba ambao waliwekeza katika infrustructure ya power line kwenda migodi ya Barrick, hapo ndo mtego ukaja kuwa watapata umeme come rain come sun, hatuwezi kuwanyima umeme barrick
   
 16. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  It is not the matter of defending, it's the matter of facts. For any mine (grand projects) to connect to national grid, there must be an equal investment in power production incured by the project. TANESCO is a govnt's entity which evaluates, negotiates and supervises these investments. I am very sure Tanesco and Barrick had this agreement. MY TAKE: WHERE HAS THIS POWER PRODUCTION INVESTMENT IMPLEMENTED?
   
 17. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi mteja mzuri zaidi ya hawa jamaa wa migodi....Nawalipa Tanesco hatakabla sijaanza kutumia umeme........LUKU
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  asante sana ... unfold story
   
 19. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Naomba nichangie kidogo katika mada hii. Moja ya eneo ambalo tuliliona kama ni mushkeli katika sekta ya madini (kamati ya Bomani) ilikuwa ni kukosekana kwa mahusianoi kati ya sekta ya madini na sekta nyingine za uchumi. Moja ya sekta hizi ni umeme. Mpaka mwaka 2009 migodi yote nchini isipokuwa Resolute ya Nzega walikuwa wanatumia umeme wanaozalisha wenyewe na ili tuzalishe ilikuwa tunawapa msamaha wa kodi kwenye mafuta. Mwaka 2008 peke yake msamaha wa kodi ya mafuta ilikuwa tshs 91bn!
  Ikaonekana kuwa ni muhimu TANESCO wapate soko hili la umeme ili wafaidike na soko la uhakika na pia economies of scale. Ndio Buzwagi na North Mara ikaunganishwa.
  Hawa wananunua umeme TANESCO na kulipa. Mgodi mkubwa kama Geita unatumia 27MW tu za umeme, Buzwagi ni Mradi mdogo na pia North Mara. Hawawezi kufika 500MW na hali ya mgawo ni zaidi ya 200MW.
  Hivyo, pamoja na kwamba migodi hii imeongeza mahitaji ya umeme, tatizo letu linabaki pale pale kuwa hatuna uzalishaji wa kutosha.
  Ni jambo la kujuvunia kuwa sasa tanesco wanauza umeme kwenye migodi. Lengo letu liwe kuhakikisha migodi yote inapata umeme tanesco ili kucreate linkages na hivyo kuwezesha tanesco kupata soko la uhakika. Vile vile hii inapunguza misamaha ya kodi na udanganyifu kwenye kodi na inaokoa fedha za kigeni zitumikazo kununu mafuta nje na hivyo kuathiri urari wetu wa Biashara.

  Tatizo la mgawo wa umeme ni changamoto ya uzalishaji wa umeme na lazima tuongeze generation. Sidhani kwamba hili ni tatizo na kampuni moja kupewa umemne na tanesco kwani tanesco inahitaji sana wanunuzi wakubwa wa umeme ili iweze kupata fedha za kusambaza umeme maeneoa ambayo hayana faida kubwa.
   
 20. Ngaramu

  Ngaramu JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  INFRASTRACTURE! !!! MKATABA WAO SIO POWER LINE PEKEE, NIPAMOJA NA PRODUCTION PLANTS.. (ndio sababu naona harufu ya UFISADI hapa). Come rain come sun Barrick lazima wapate umeme, sio waTZ kwanza.
   
Loading...