Angalizo juu ya dawa ya kuoteshwa na Bikira Maria huko Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalizo juu ya dawa ya kuoteshwa na Bikira Maria huko Arusha

Discussion in 'JF Doctor' started by Lawkeys, Mar 19, 2011.

 1. Lawkeys

  Lawkeys JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 1,110
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ukikubali ukweli huu, utakuwa huru.

  1. Mtu akifa hawezi kabisa kuwasiliana na walio hai

  Mungu aliwambia Adam na Eva mkila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya mtakufa hakika, Mwanzo 2. Shetani akamwambia Eva, mkila hamtakufa hakika Mwanzo 3.

  2. Waliokufa hawajui neno lolote, kumbukumbu lao limetoweka, Mhubiri 9:5.

  3. Habari ya Bikira Maria na watakatifu wengine kuenndelea kuwa hai, inapingana na maandiko. Hilo ni moja ya mafundisho ya uongo yalioingizwa kanisani na Wakatoliki, Wakolosai 2:8, Daniel 7:25,

  4. Uongo huo umefungua njia kwa ibada za wafu na kupitia wafu, na shetani na mapepo yamekuwa yakijitokeza katika sura ya marehemu, nakuwakeuza watu kumwelekea Mungu. Ndio maana utasikia Nyerere kanitokea, sijui Bikira Maria au mtakatifu flani, huu ni uongo. Pepo alimtokea Sauli katika Sura ya Samwel, wakati Samweli aliisha kufa, Samwel 28.

  5. Ukifahamu hili utakuwa huru, hakuna ataykudanganya kwamba kaoteshwa dawa na Bikira Maria. Labda Pepo Mchafu. Hakuna ushahidi wowote wa kimaandiko wa kupalizwa kwa Maria. Hakuna cha pagatory, soma uelewe upate kuwa huru. 2 Wathesalonike 2:7-12. Hakuna maombezi kupitia wafu aka watakatifu, ni kupitia Yesu tu!! 2 Timotheo 2: 5

  6. Biblia haijipingi, andiko lolote linalozungumzia kuishi baada ya kifo, humaanisha kuishi baada ya kuja kwa Yesu ambaye atawafufua watakatifu na watamlaki mawinguni. Ukisikia yesu amekanyaga ardhi hii, usijisumbue, huyo ni yesu feki, cosmic Christ, Yesu wa kweli hatagusa ardhi, bali tutamlaki mawinguni.

  7. Sikashifu dini wala imani ya mtu. Anayekashfu ni yule, anayepindisha maandiko na kuwasingizia watu waliolala mauti kuwa wamewatokea.
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  kwa wakristo waliowengi ni vigumu sana kuelewa kama babu anafanya ushirikina, kwa vile biblia hawaisomi na wengine kwa vile wapo kidunia zaidi hata wakiisoma wapo tayari kupindisha misitari ya biblia. Sasa mwingine huyo anajiita nabii naye kaoteshwa chague pa kwenda.shetani atawachezeeni akili sana mpaka mtakoma.
   
 3. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hata nyie hamsomi vizuri Mungu pia hutumia ndoto katika kufunulia watu mambo mfano kwani yusufu alifuniliwaje kuwa atakuwa juu ya ndugu zake ambapo ilitokea huko misri,Mungu anatumia njia mbali mbali kufikisha ujumbe kwa watu wake,
   
 4. n

  ntobistan Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mamb ya dini sio ya kubishaniana.Mungu awe nanyi amen
   
 5. h

  hoyce JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Muda na nguvu ulizotumia (kukosoa/kashifu) imani ya wakatoliki kama ungevitumia kuitangaza imani yako na madhehebu yako vingeweza kusaidia sana kuendelea na kukubalika. Hata siku moja hutasikia mkatoliki anayejua imani yake akipoteza muda kukosoa imani za wengine badala ya kutangaza yake. Ndio maana kanisa limesimama licha kushambuliwa kila kona. Kila kanisa jipya linaloanza linatafuta waumini kwa kuponda mafundisho ya kanisa katoliki. Lakini ukweli utabaki pale pale kuwa pamoja na biblia kuna maandishi mengine ya kimapokea ambayo wakatoliki wanayaamini, ambayo wewe na wenzako hamyataki, mmelazimisha akili yenu kubaki tu kwenye biblia, pamoja na kutambua maneno haya; 'Yohana 21:25, Kuna na mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu, ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitambu vitakavyoandikwa.'

  Baadhi ya hayo mambo ndo yamo kwenye vitabu vya kimapokeo vya kikatoliki. Na haya wezi kupatikana kwenye haya madhehebu yanayoibuka leo.
   
 6. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sijakuelewa babu wa Loliondo hakusema kama ameoteshwa na bikira Maria nadhani unachanganya na huyu jamaa wa Rombo hebu weka sawa kauli yako,Loliondo nilikwenda na wakati ule tuliweza kuongea na kumuuliza maswali,kwa masikio yangu ni kwamba ameoteshwa na mungu na si bikira maria,weka sawa kauli yako ulimsikia mwenyewe au unasikia kupitia third parties.
   
 7. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  kwa huyu babu, yetu macho...suburi tuone, kama ni jambo la Mungu litadumu na litaendelea kuwa jema, lakini kama si jambo la Mungu litaishia pabaya sana na watz wengi wameshajitia kitanzi, watalia na kusaga meno. mi siwashauri watu waende kwa huyu babu..
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa jamvini tunahusika na masuala ya uchambuzi wa masuala yanayohusu elimu dunia; masuala ya imani ya mtu si mahala pake.Hata hivyo Biblia yenyewe haijawahi kusema kwamba ina ufafanuzi wa kila jambo humo ndani; ukisoma Jn 21:25 utaona mtume huyo anakili ya kwamba kama mambo yote aliyoyasema na kuyafanya Yesu Kristo yangeliandikwa dunia ingelijaa vitabu vyake, Hii ndiyo maana mbali na biblia kanisa katoliki linakubali pia mapokea mbali mbali.
   
 9. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,194
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Sitoamini huyo anaedai ameoteshwa na Bikira Maria hadi kanisa litoe kauli elekezi!

  Ila Mwanangu naomba nikuulize;
  Biblia na KANISA ni nani mzazi? Ndio sababu Biblia inasema "Mafundisho yote aliyo fundisha Yesu yangeandikwa tusingeweza kubeba kitabu hicho...."

  Bwana Yesu uhai wake wote hapa duniani hakuwahi kuisoma Biblia kama ilivyo leo
  Ndipo alipo liachia mamlaka Kanisa Na kusema; " ...Mtakalo fungua/kufunga duniani limefunguliwa/limefungwa Mbinguni.

  Hivyo basi ukae ukielewa kwamba si Biblia pekee ni Neno la Mungu bali Biblia ni ufunguo wa nyumba yenye vyumba vingi.

  Bila kanisa biblia ungeipata wapi?
  Usipende kuponda mafundisho ya Kanisa kwa kutumia mistari ya Biblia hicho ni kiburi cha UZIMA!
  Kumbuka andiko linaua bali Roho yahuisha.
   
Loading...