ANGALIZO: JF inahitaji wachambuzi wabobezi

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Ninatambua kua kuna mada ambazo kimsingi hazitakiwi kuachwa tu humu kutokana na kukosa sifa kilingana na Regulations za JF, pia natambua kua kuna threads ambazo zinaunganishwa kutokana na mfanano wa mawazo ya watoa mada.

Tatizo ni kwamba mara nyingi unakuta kuna Mada mbili tofauti hata hazina mfanano wa kimawazo lakini zinawekwa na kuunganishwa pamoja, hii inasababisha hata msomaji kukosa hamu ya kukisoma kitu na kukielewa juu ya utofauti wake.Unakuta Mada ya leo inaunganishwa na ile ya mwezi uliopita, sasa kama kuna kitu gani kipya pamoja ufanano wake na ni kitu gani msomaji anapata hasa?

USHAURI

Wataalam wa IT na habari tu hawatoshi kuchambua masuala ya kisiasa,watumike wabobezi wachambuzi wazuri wanaojua kutofautisha mambo ya aina mbalimbali, sio kuunganisha kitu cha muda mrefu na cha leo maana huko ni kumnyima msomji kupata kitu kipya.
 
Hili kila siku nishalisema!
mods hawana uwezo wa kuchambua kila kitu kiasi kwamba wanaharibu JF kabisa
Mtu umetoa mtazamo wako wa tofautu kuhusu tukio flani ambalo limepita wao hulijumuisha tu huko wanakojua!

Kwa hili nitaendelea kuomba mods wa Jf wahakikiwe tu sio kila mods ni mchambuzi!
 
Back
Top Bottom