Angalizo: Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo hufanana na dalili za magonjwa ya moyo

Nyie watu nyieeeee, juzi tu mimi nimetoka hospitali kumuona cardiologist, nimefanya ultrasound ya moyo, EKG na Echo kwa ajili ya haya haya ma vidonda ya tumbo, nilipata maumivu makali kifuani na kupata shida ya kupumua, nikaenda local dispensary nikaambiwa ni angina au symptoms za heart attack....

Nilipanic nyie.... lol, kwenda kwa cardiologists naambiwa sina tatizo lolote, vipimo viko safi kabisa, Akanambia hivyo ni vidonda vya tumbo.... Nimepewa dawa mzigo hapa, nahisi nafuu kiasi but nikila tu nahisi vichomi tumboni.
Hii hali ilinisumbua sana mwanzoni nilikuwa najua nina ugonjwa wa moyo, ila sasaivi nadunda tu.. Adi nimeizoea najua kabisa nikila maharage au dagaa usiku lazima niumwe kifua upande wa kushoto sina wasiwasi
 
Mm pia ninatatizo la kifua kinauma mpk upande wa mgongoni,nimeshapima moyo Mara mbili majibu yako vizuri.nimepimwa h.pyrol Mara 4kipimo kimoja ndio kiluandika positive lkn vitatu vikaandika negative...
vipi dada ulipona?
 
ni ipi hiyo mkuu

Hua sielewi mtu ana solution ya jambo flan then hasemi! It’s pure evil in limited view,sio kila kitu ni fursa! Vingine you do for karma and that’s it. Anyway anza na hiyo baking soda-hiyo ni base itaenda kunetralize acid mwilini km walivyoandika hapo juu wengine!
 
Hua sielewi mtu ana solution ya jambo flan then hasemi! It’s pure evil in limited view,sio kila kitu ni fursa! Vingine you do for karma and that’s it. Anyway anza na hiyo baking soda-hiyo ni base itaenda kunetralize acid mwilini km walivyoandika hapo juu wengine!
hiyo nimeshatumia sana mkuu lakini bado
 
Hongera kwa dr maana mi ninateseka Mpaka leo hii na tumbo linajaa gest mnoo nimetumia dawa Mpaka nimechoka
Nlikua na hilo tatzo kwa mda mrefu ,kuna Mzee mmoja yupo mwanza alinipatia dawa za asili mwaka jana saiv nipo Safi kabsa,,,
 
Mm pia ninatatizo la kifua kinauma mpk upande wa mgongoni,nimeshapima moyo Mara mbili majibu yako vizuri.nimepimwa h.pyrol Mara 4kipimo kimoja ndio kiluandika positive lkn vitatu vikaandika negative.

Pia ninashida ya ganzi ktk vidole vya miguu.nimekunywa sana dawa za hospital nakaribia miaka miwili wananiambia utakuwa mishipa Mara madonda ya tumbo maana utrasound nikipigwa iko vizuri.badae wakasema utakuwa oparation 3 za uzazi nikizofanyiwa.

Sasa ndio nimeanzisha kubanwa kifua kunamuda chini ya maziwa km kunawaka Moto siwezi kunywa soda tumbo linajaa hlf najamba sana mpk najishangaa. Nimezunguka mahosptal na Sina bima mpk nimemkabidhi Mungu tu
Kama tumbo linajaa basi ni rahisi. Tengeneza mchanganyiko wa limao, tangawizi na kitunguu swaumu, chemsha kisha kunywa. Kiasi ni kikombe kimoja cha chai. Fanya hivyo kila jioni kabla ya kula. Baada ya wiki moja utapata majibu. Kumbuka mchanganyiko huo hutengeneza alkaline solution inayokwenda kupunguza wingi wa acid tumboni. Pia kama una tatizo la kufunga chòo yaani constipation, nalo litaisha kabisa.
 
Watu wana shida humu wewe unakuja kukenua kenua humu,majukwaa ya kunenua mbona yapo mengi
Shida zako sasa unataka kunifia mimi? Jingaa kabisa

Btw nilikuquote wewe au kiherehere na kuwashwashwa kwako ukadandia gari kwa mbele?

Peleka uswahili na stress zako kuleee
 
Habari zenu

Nimeona niwashirikishe hili kwa sababu watu wengi mmekuwa mkipoteza fedha nyingi kujitibu maradhi ambayo hayapo miilini mwenu kutokana na madoctor wengi kutokuwa na weledi wa kutosha kubaini ugonjwa halisi unaomsumbua mtu

Story yenyewe

Mwezi uliopita baada ya kufanya kazi kwa mda mrefu huku nikiwa sijala chochote baada ya kumaliza kazi mida ya jioni gafla nilisikia maumivu makali ya kifua upande wa kushoto yaani sehemu ya moyo, na maumivu hayo yaliambatana na kifua kubana wakati nikivuta hewa kwa ndani kifua upabde wa kushoto kinabana

Baada ya kupita siku mbili nikidhani hali itapotea ndio ikawa inaendelea maumivu yakatoka upande mmoja wa kifua hadi mwingine huku nikipumua kwa shida, na maumivu hayo yalizidi wakati nikitoka kula baada ya masaa mawili nilazima nipumue kwa shida yaani kifua kinabana nikivuta pumzi ndani

Nikaona niende hospitali moja ya hapa mtaani nikalipia kila kitu kwaajili ya kumuona dr, kufika baada ya kumuelezea kila kitu, yule dk akaanza kwa kunipima presha na kuniuliza historia ya tatizo au kama kuna mtu mwingine alikuwa na hili tatizo kwenye familia

Hivyo moja kwa moja yule dr akaniambia kuwa dalili nilizokuwa nazo ni moja ya dalili za heart attack, au magonjwa ya pumu na nimonia na akaniambia kuwa kwa vile hospitali yao haina vifaa vya kupima moyo na magonjwa mengine ya kifua akanishauri niende kwenye hospitali kubwa zenye hivyo vipimo

Kweli nikatafuta hospitali moja kubwa nikaingia kwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kama nilivyo elekezwa na baada ya kumpa maelezo kuwa ninahisi nna ugonjwa wa moyo, alitabasam akaniuliza kuwa nna uhakika gani kama nna tatizo la moyo wakati sijawahi pima?

Akaniuliza kama nlishawahi kusumbuliwa na presha cz mda ule alipima blood preassure yangu akakuta ipo vizuri tu, nikamwambia sijawahi kusumbuliwa na presha. Hata siku moja, na mapigo yangu ya moyo yapo kawaida tu

Basi ikabidi yule dk anipime vipimo vyote vya moyo na kiwango cha cholesterol kwenye dam, ili ahakikishe kwanza kama tatizo linatokea huko, na hapo nilichezea zaidi ya laki moja kupima vipimo vyote

Baada ya vipimo yule dk akaniambia huna tatizo lolote la moyo wala kifua akaniambia kuwa tatizo nilolo nalo ni ACID REFLUX, akaniambia kuwa nna tatizo la ACID kuwa nyingi tumboni kutokana na kutokula kwa muda mrefu au kutumia vyakula ambavyo vinaacid nyingi

Akaniambia kuwa hiyo acid hupelekea kitu kinachoitwa HERT BURN ambacho acid hupanda juu na kuathiri upande wowote wa kifua na mfumo wa upumuaji, kisha akaniambia kuwa dalili za HEART BURN watu wengi hukosea na kuzifananisha na dalili za shambulio la moyo kwanu hufanana sana

Hivyo akaniambia kuwa tatizo nililo nalo limesababishwa na kukaa mda mrefu bila kula na kupelekea acid kuunguza tumbo na kupanda juu hadi kifua kubana hivyo akaniambia tatizo nililo natakiwa nitumie dawa za kupunguza hiyo acid

Dr akaniambia kuwa wala hamna shida ya kutumia dawa za ant-acid za hospitali, yeye akanishauri niende dukani nikanunue kitu kinaitwa baking soda ambayo ina mchanganyiko wa sodium bicarbonate

Dukani huuzwa shilingi 400 tu akaniambia nichote kijiko kimoja then nichanganye na maji alafu ninywe asubuhi na jioni wakati wa kutoka kulala akaniambia nisitumie vyakula ambavyo vinapromote acid kama ndizi, machungwa nyanya na maharage hadi hali itakapo kaa sawa.

Baada ya kutumia ndani ya siku nne tu ile hali ikapotea na kifua kikaachia nikawa fresh kabisa

Hivyo ni vyema utakapoona tatizo lolote kwenye kifua au upande wa moyo usipende kulichukulia moja kwa moja kama ni dalili za magonjwa ya moyo au kifua, dalili nyingi huwa zinasababishwa na vidonda vya tumbo au ACID REFLUX
Mimi tatizo langu la acid ni hlo hlona nilitumia muongozo wa daktar nikakaa sawa sahv nimejifungua sasa chakula king ni ndizi kwangu Kwa hii miez ya mwanzo na tatizo naona linataka kujirud nifanyeje na ninanyonyesha ?
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom