Angaliza hizi video zitakusaidia kuwa na mafanikio kibiashara au kuwa tajiri

changman

JF-Expert Member
Jul 26, 2011
229
90
Habari zenu. Mimi katika masomo yangu ya biashara nayosoma nimegundua kwamba wanadamu wanakuwa maskini kutokana na sababu mbalimbali mfano: jinsi ulivyolelewa, jinsi unavyoamini, mazingira unayoishi (mfano ukiwa ulaya ni rahisi kupata mikopo midogo midogo kuliko ukiwa tz), n.k. Sasa nimeona hizi videos niziweke humu ili kila mtu kivyake ajue ni kitu gani knamfanya asiwe na mafanikio. Lakini kama elimu zote zilivyo, ukijifunza kitu bila kuifanyia kazi hiyo elimu, ni bure. Ukijifunza then fanyia kazi huo ujuzi uliojifunza.

Tofauti kati ya mafanikio na utajiri.
Kila mtz siku hizi anawaza kuwa tajiri bila kuelewa kuwa ni rahisi sana kuwa na mafanikio kuliko kuwa tajiri. Kiwango cha utajiri na mafanikio kinatofautiana kulingana na nchi na nchi: mfano tz ukiwa na milioni 200 unaonekana tajiri lakini kwa marekani hio ni middle class. Sasa nini maana ya mafanikio? Kuwa na mafanikio ni ile hali ya kuweza kumudu zile gharama za msingi za kibinadamu mfano afya, chakula, sehemu bora ya kuishi, kuweza kugharamia elimu ya wanao, kuweza kumudu viburudisho na burudani, usafiri mzuri, n.k. Sasa utajiri ni kuwa na vitu kupita kiasi. Ukiwa na mshahara wa 100,000 shs kwa mwezi wewe ni maskini maana hautoshi kugharamia huduma za msingi. Ukilipwa shs. milion 2 kwa mwezi kwa tz wewe una mafanikio, wewe sio maskini. Ukilipwa milioni 100 kwa mwezi wewe ni tajiri. Sasa sio mbaya kufikiria kuwa tajiri, ni safi kabisa, sema tu unatakiwa kujua nini tofauti ya utajiri na mafanikio.

Napenda uangalie hizi videos zitakupa elimu nzuri sana na kukufanya ujiamini. Hata kama hujafika chuo kikuu, haimaanishi kwamba hautafanikiwa. Ni mabilionea na matajiri wangapi duniani na hata tz hawana elimu? jiulize. Jua pia kuwa na mafanikio na kuwa tajiri zote ni rahisi, ila inahitaji elimu sahihi, kujiamini na uvumilivu.

1. https://www.youtube.com/watch?v=Sz1SLOkIg0Q

2. https://www.youtube.com/watch?v=6MrwEgyNg6o

3. https://www.youtube.com/watch?v=VTMhOHuZZAw

4. https://www.youtube.com/watch?v=4ff8zukewIE

Mafanikio mema.
 
Natumia simu mkuu. Unaweza kunitajia majina ya hizo films? Nimehamasika sana kuzitafuta! Shukrani.
 
Alaaaa kumbe ni yule jamaa wa Rich dad poor dad.........mwisho wa siku korti inataka kumfilisi nasikia......ila mawazo yako mengine yanatia hamasa!
 
Tuko pamoja Changman, kama kuna wimbo ambao siku hizi kwangu mimi ni Hit song ni kumsikiliza huyu American Japanese- Kiyosaki, Rich Daddy, kama angeanzisha dhehebu la waabudio utajiri mimi ningekuwa msambazaji wa Injili yake! Afrika inatakiwa ianzishwe movement kuwahubiria watu habari njema hizi, za injili ya kusaka utajiri, watu wanapata pesa sana tatizo ni kule wanakozipeleka, ni mafundisho tunayoyakosa!

Niwie radhi kwa maelezo marefu saa zingine mimi nae mweeee!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom